3080; Mwili na mazingira.
Rafiki yangu mpendwa,
Tunaweza kuona tuna mambo mengi sana ambayo tunakabiliana nayo kwenye safari yetu ya mafanikio makubwa.
Lakini kiuhalisia, mambo hayo yote yamegawanyika kwenye makundi makubwa mawili; mwili na mazingira.
Mapambano ya kwanza kwetu ni ya kimwili.
Miili yetu ni kikwazo cha kwanza kwetu kuyafikia mafanikio makubwa tunayoyataka.
Kikwazo cha mwili kinatokana na mambo makubwa matatu;
Moja ni uvivu wa mwili kutokutaka kufanya mambo magumu. Huu unavukwa kwa kuusukuma mwili kufanya yale yanayotakiwa kufanyika.
Mbili ni tamaa ya mwili kutaka kupata vile inavyotamani, ambavyo huwa ni vya anasa na vinavyopingana na kile mtu anataka. Hii inavukwa kwa kuwa na udhibiti kwa mwili.
Tatu ni uchovu na udhaifu wa mwili unaotokana na afya kutokuwa imara. Hii inavukwa kwa kujenga afya imara.
Kushinda vikwazo vya mwili pekee haitoshi kupata ushindi tunaoutaka.
Kwani kuna watu wanatumia miili yao vizuri, lakini bado hawafanikiwi.
Hiyo ni kwa sababu wanakuwa wameshindwa kushinda vikwazo vya mazingira.
Mazingira yamekuwa kikwazo kikubwa kwa watu wengi kupiga hatua kubwa kwenye maisha yao.
Kuyashinda mazingira ni mapambano mengine ambayo yapo kati yetu na mafanikio tunayoyataka.
Kwenye mazingira kuna vikwazo vikubwa vitatu vya kuvuka ili kufanikiwa.
Moja ni kufuata mkumbo. Sisi binadamu ni viumbe wa kijamii na tunapenda kuiga yale ambayo wengine wanayafanya. Lakini hilo ni kikwazo sana kwenye mafanikio makubwa. Kwa sababu ukifanya kile wanachofanya wengine, utaishia kupata matokeo wanayopata, ambayo huwa siyo matokeo bora.
Mbili ni njia za mkato za kufanikiwa. Kuna njia nyingi za mkato za kupata mafanikio ambazo huwa zinapigiwa debe sana. Ni rahisi kushawishika kutumia njia hizo, lakini matokeo yake huishia vibaya. Kitu pekee ambacho watu huwa wanakipata kwenye njia za mkato ni mikato, yaani kupoteza zaidi.
Tatu ni usumbufu.
Kuna usumbufu wa kila aina kwenye mazingira yanayotuzunguka. Usumbufu huo unanasa umakini wetu, kuiba muda wetu na kutumia nguvu zetu kwa namna isiyo sahihi.
Watu wengi hudhani usumbufu ni mpaka kiwe kitu kibaya.
Lakini usumbufu ni chochote ambacho hakina mchango kwenye malengo unayotaka kuyafikia.
Ni lazima uachane na yote yasiyo muhimu ili kuweka kipaumbele kwa yale muhimu tu.
Wajibu wako mkubwa kwenye hii safari ya mafanikio ni kutumia vizuri mwili na mazingira yako badala ya kukubali viwe kikwazo kwako.
#NidhamuUadilifuKujituma
#AfyaUtajiriHekima
#KaziUpendoHuduma
#UpekeeUdadisiUbunifu
#UshirikianoUtegemeanoUwajibikaji
#BilioneaMafunzoni
#NajengaBiashara
#HakunaKingineMuhimu
#LazimaNitoboe
#NawekaKaziNifanikiwe
Navuka uvivu wa mwili kwa kusukuma mwili wangu kufanya yale yanayotakiwa kufanya .
LikeLike
Vizuri
LikeLike
Mwili na mazingira ni vikwazo vikubwa kwa mtu kufanikiwa, vishinde vikwazo hivi.
Asante sana Kocha Dr Makirita Amani
LikeLike
Hakika
LikeLike
Asante kocha.
LikeLike
Karibu
LikeLike
Kutumia vizuri mwili na mazingira yangu badala ya kukubali viwe vikwazo.
LikeLike
Ndiyo.
LikeLike
Asante Kocha nitaweza kuvuka vikwazo vya mwili na mazingira ili kufikia mafanikio makubwa
LikeLike
Kila la kheri.
LikeLike
Wajibu wako mkubwa kwenye hii safari ya mafanikio ni kutumia vizuri mwili na mazingira yako badala ya kukubali video vikwazo kwako
LikeLike
Hakika
LikeLike
Nakwenda kuachana na yale yote ambayo sio muhimu katika malengo yangu na kufanya yale ya muhimu tu.
LikeLike
Kila la kheri.
LikeLike
Nitajitahidi kutumia vizuri mwili na mazingira yangu katika kuyafikia mafanikio makubwa katika maisha yangu badala ya kuvikubali viwe vikwazo katika safari yangu ya mafanikio. Asante sana kocha
LikeLike
Karibu
LikeLike
Ni kweli kocha mwili na mazingira vinatuathiri Sana.
LikeLike
Tuvishinde.
LikeLike
Asante sana
LikeLike
Karibu
LikeLike
Asante Kocha.
Ili kupata mafanikiio makubwa, Nitapambana kikamilifu kukabiliana na vikwazo hivi viwili; mwili na mazingira.
LikeLike
Kila la kheri
LikeLike
Kweli kabisa kabisa mwili na mazingira vinachangia sana maendeleo yetu
Asante
LikeLike
Hakika
LikeLike
Asante Kocha. 🙏🏽
LikeLike
Karibu
LikeLike
Nitatumia vizuri mwili na mazingira kuweza kufanya makubwa
LikeLike
Vizuri
LikeLike
Asante kocha,Nitajitahidi kutumia mwili na nguvu ili nifanikiwe kwenye hii safari sio viwe kikwazo cha kutofanikiwa.
LikeLike
Kila la kheri
LikeLike
Umenena vyema sana.Mwili ukiongozwa na tamaa unakua kikwazo kufanikiwa .Mwili haupendi kuumia bali kusikia raha,hakuna raha kwenye mafanikio kuna namna lazima usijisikie vizuri kwa muda ili ufanikiwe.
LikeLike
Kabisa.
LikeLike
Mchakato wa BM no kuvuka vyote Vikwazo vya Mwili na Mazingira, dawa Ni kukaa kwenye hii Boti ya nifike salama kwenye mafanikio makubwa
LikeLike
Vizuri
LikeLike
Mafanikio ni kutumia mwili na mazingira yako vizuri.
LikeLike
Hakika
LikeLike
Mabadiliko yanataka mwili uwe vizuri na kujua namna mazingira yanazuia kufanikiwa jwa mtu
LikeLike
Kabisa.
LikeLike
Mwili na mazingira
LikeLike
Ndiyo.
LikeLike
Asante sana kocha, mafanikio yangu ni kutumia vzr mwili na mazingira vzr.
LikeLike
Hakika
LikeLike