3089; Pumua, kula, fanya kazi.
Rafiki yangu mpendwa,
Kuna mambo mengi sana ambayo tumekuwa tunahangaika nayo kwenye maisha yetu.
Na kwa kuwa muda wetu ni wenye ukomo na mambo ya kufanya kuwa mengi, huwa ni rahisi kuahirisha baadhi ya mambo.
Kuna mengi sana ambayo huwa tunayaahirisha, kwa sababu ya muda.
Lakini kuna ambayo huwa hatuwezi kuyaahirisha, hata iweje.
Hiyo ni kwa sababu hayo ndiyo yameshikilia uhai wetu.
Haijalishi tumetingwa kiasi gani, huwa hatuwezi kuahirisha kupumua.
Kupumua ndipo uhai wetu ulipo hivyo tutafanya wakati wote.
Kadhalika kwenye kula chakula, hatuwezi kuahirisha hilo kwa muds mrefu. Tunaweza kutingwa sana na kuchelewa kula, lakini hatutaacha kabisa.
Cha kushangaza sasa, inapokuja kwenye kufanya kazi, kutekeleza majukumu yanayotupa yale tunayotaka, huwa tunatafuta kila sababu ya kuahirisha na tukiipata tunaitumia vizuri sana.
Kadiri majukumu ya kutekeleza yanavyokuwa magumu, ndivyo nafasi ya kuahirisha inavyokuwa kubwa.
Hiyo ni kwa sababu hatupendi kujisumbua na kujitesa.
Lakini ambacho tunasahau ni umuhimu mkubwa wa kazi kwetu na maisha yetu kwa ujumla.
Kazi ndiyo inatupa mafanikio yoyote tunayoyataka kwenye maisha yetu. Hakuna mafanikio yanayopatikana bila ya kazi.
Na zaidi, kazi ndiyo inafanya maisha yetu kuwa na maana kwetu wenyewe na hata kufanya tuheshimiwe na wengine. Watu watakukubali na kukuheshimu kwa mchango unaokuwa nao kwao na kwa watu wengine, kupitia kazi unayofanya.
Kufanya kazi ni moja ya vipaumbele muhimu sana kwenye maisha yako.
Hivyo ni wajibu wako kuhakikisha kila siku unafanya kitu kwenye kazi yako bila ya kujali nini kinaendelea kwenye maisha yako.
Kama unapumua na kama umeweza kula, basi hakikisha pia unatekeleza majukumu yako kwenye siku hiyo.
Vipaumbele vikubwa kwenye maisha yako na muda wako wote vinapaswa kuwa hivyo vitatu; kupumua, kula na kufanya kazi.
Yaani hivyo ni vipaumbele ambavyo havina mjadala, ambavyo utavifanya inyeshe mvua au liwake jua.
Weka kipaumbele kikubwa kwenye kazi kama unavyoweka kwenye kupumua na kula na utaweza kufanya makubwa sana kwenye maisha yako.
Mengine yanaweza kusubiri, lakini siyo kupumua, kula na kufanya kazi.
Hayo ni muhimu kwa afya yako na maisha yako kwa ujumla.
Ni mambo ambayo ukiyajali yanajenga maisha yako na ukiyapuuza unayaharibu maisha yako.
Ukweli ni kwamba watu wengi huwa hawaipendi kazi na wanatumia muda wao mwingi kwenye kutafuta njia za mkato za kufanikiwa.
Lakini pia ni watu wengi ambao huwa hawapati mafanikio makubwa.
Kwa hiyo inajidhihirisha wazi hapo kwamba kinachopendwa na wengi, huwa hakina thamani wala manufaa makubwa.
Kama ambavyo usipopumua na kula hujisikii vizuri, ndivyo pia unavyopaswa kutokujisikia vizuri usipofanya kazi.
Kwa kufanya hivyo utajiepusha na matatizo mengi yanayotokana na kutokupenda kazi.
Tunajua kuhusu watu wanaokufa kwa kushindwa kupumua, mfano wanaopata magonjwa ya mfumo wa upumuaji.
Tunajua kuhusu watu wanaokufa kwa kukosa chakula, mfano wanaokuwa kwenye magonjwa au majanga mbalimbali.
Lakini ambacho wengi hawajui ni watu wanaokufa kwa kutokufanya kazi.
Hilo lipo sana ila halipo wazi kwa wengi.
Ukiangalia watu wengi wanaofanya kazi, huwa na afya nzuri na imara, lakini wanapostaafu kazi, afya zao zinazorota na kufa ndani ya muda mfupi.
Hiyo ni kwa sababu wanapostaafu kazi, miili yao inaona haina tena matumizi na hivyo kuwa dhaifu, kitu kinachofanya kufa iwe rahisi kwao.
Hivyo basi, kama unataka kuwa na maisha marefu, fanya kazi maisha yako yote. Epuka sana kitu kinachoitwa kustaafu.
Moja ya sababu za wewe kujenga biashara kubwa zinaweza kuwa ni ujenge uhuru wa kifedha ili usihitajike tena kufanya kazi.
Ni lengo zuri hilo, lakini kamwe usije ukafika hatua ya kuacha kufanya kazi.
Hata pale unapokuwa umefikia uhuru wa kifedha, kwamba unaweza kuendesha maisha yako hata kama hufanyi kazi, ni muhimu sana uendelee kufanya kazi kila siku.
Unapokuwa na uhuru wa kifedha na usifanye kazi, fedha huzo ulizopambana kuzipata zitakuua mapema sana.
Lakini unapokuwa na uhuru wa kifedha na ukaendelea kuchapa kazi kwa juhudi kubwa, fedha hizo zitakufanya uishi kwa miaka mingi zaidi.
Masikini wengi huona wanafanya kazi ili waishi, hivyo wanapoweza kuishi bila ya kazi wanaacha kujituma mara moja, na huo ndiyo unakuwa mwisho wao.
Matajiri wanajua wanaishi ili wafanye kazi na kadiri wanavyotajirika ndivyo wanavyofanya kazi zaidi, kitu kinachowafanya wakue zaidi kimafanikio.
Ipende kazi,
Ipe kazi kipaumbele,
Epuka kabisa kustaafu,
Ishi ili ufanye kazi na siyo kufanya kazi ili uishi.
Ubinadamu ni kazi unayofanya, hivyo fanya kazi ili kutimiza ubinadamu wako.
#NidhamuUadilifuKujituma
#AfyaUtajiriHekima
#KaziUpendoHuduma
#UpekeeUdadisiUbunifu
#UshirikianoUtegemeanoUwajibikaji
#BilioneaMafunzoni
#NajengaBiashara
#HakunaKingineMuhimu
#LazimaNitoboe
#NawekaKaziNifanikiwe
Masikini wengi huona wanafanya kazi ili waishi, hivyo wanapoweza kuishi bila ya kazi wanaacha kujituma mara moja, na huo ndiyo unakuwa mwisho wao.
Matajiri wanajua wanaishi ili wafanye kazi na kadiri wanavyotajirika ndivyo wanavyofanya kazi zaidi, kitu kinachowafanya wakue zaidi kimafanikio.
Asante sana Kocha Dr Makirita Amani
LikeLike
Ndivyo ilivyo
LikeLike
Kupumua,kula,kufanya kazi ndio vipaumbele
Tunaishi ili kufanya kazi na si kufanya kazi ili kuishi.
Asante sana kocha.
LikeLike
Karibu
LikeLike
Naishi ili nifanye kazi.
LikeLike
Hivi ndivyo vipaombele vya kunifanya niweze kuendelea kuishi
-kupumua
-kula
-kufanya kazi
Ubinadamu ni kazi ninayoifanya,napaswa nifanye kazi ili nitimize ubinadamu wangu
Asante kocha
LikeLike
Hakika
LikeLike
Safi sana.
LikeLike
Unafanya kazi bila kustaafu na mwisho unakua na fedha ambayo inakuwezesha wewe kuishi miaka mingi kumbe ukistaafu mna mwili pia unakosa kazi tujiwekee lengo kubwa
LikeLike
Kabisa
LikeLike
Naishi Ili nifanye kazi.
LikeLike
Safi.
LikeLike
Kazi ya utabibu wa binadamu nitaifanya milele hata nitakapofikia uhuru wa kifedha kwa namba ya utajiri wa bilionea nitaendelea kuifanya.
Angalia fedha ulizopambana kuzitafuta zisije zikakuua ukishazipata kwa kuacha kuendelea na mchakato wa kufanya kazi.Tunaishi ili kufanya kazi.
LikeLike
Kila la kheri.
LikeLike
Nitafanyabkazi siku zote sitastaafu
LikeLike
Safi.
LikeLike
Kuna watu wanakufa kwa kukosa chakula. wengine wanakufa kwa kukosa pumzi na wengine wanakufa kwa kutokufanya kazi.
ASANTE SANA KOCHA
LikeLike
Imekaa hivyo
LikeLike
Pumua, kula, fanya kazi, dhana nzuri sana hii, tukiweza kuiishi mafanikio siyo kitu cha kutafuta kati yetu. Asante sana kocha.
LikeLike
Kabisa.
LikeLike
Asante Kocha,
Sitastaafu kufanya kazi.
LikeLike
Kila la kheri
LikeLike
Nimesoma Kocha na ni kweli unayosema bila kazi ni tabu kuishi na kwamba wanaostaafu wanakufa mapema kwa vile huwa hawafanyi kitu tena baada ya kustaafu. Tunatakiwa tuendelee kujituna na kufanya kazi hadi mwisho.
Asante sana Kocha.
LikeLike
Kabisa.
LikeLike
Kazi ndio kipaombele cha kwanza. Kwenye kazi hakuna mustafu, hivyo fanya kazi kwenye maisha yako yote.
LikeLike
Hakika
LikeLike
Kama unapumua na kama umeweza kula, basi hakikisha pia unatekeleza majukumu yako kwenye siku hiyo.
Asante sana
LikeLike
Ndiyo hivyo
LikeLike
Pumua,kula, kufanya Kazi+UVUMILIVU hayo ndiyo vipaumbele vyangu.asante sana kocha
LikeLike
Kila la kheri
LikeLike
Kaz Kaz Kaz
LikeLike
Kazi
LikeLike
Nitafanya kazi maisha yangu yote
LikeLike
Kila la kheri.
LikeLike
Asante kocha,Nitafanya kazi na kuipa kipaombele kazi.hakuna kustaafu kwenye kazi.
LikeLike
Vizuri
LikeLike
Ipende kazi
LikeLike
Hakika
LikeLike
Hakuna mafanikio bila kufanya kazi.
Hivyo ninawajibika kila siku ninafanya kazi.
Asante kocha
LikeLike
Vizuri
LikeLike
Kupumua kula kazi Kila siku .
Asante kocha hakuna mtu kustaafu hapa.
LikeLike
Safi sana.
LikeLike