3093; Ugumu usio na ulazima.
Rafiki yangu mpendwa,
Maisha na mafanikio huwa ni rahisi,
Lakini watu wamekuwa wanayafanya kuwa magumu bila ya ulazima wowote.
Watu huwa wanatengeneza ugumu huo kwa kuhangaika kutafuta njia za mkato na ambazo hazihusishi kufanya kazi.
Ni jambo la kushangaza, lakini ndivyo ukweli ulivyo.
Watu wanayafanya maisha kuwa magumu pale wanapokuwa wanatafuta njia za mkato ili kukwepa kuweka kazi.
Kwa kukwepa kazi, watu wanayafanya maisha yao kuwa magumu zaidi.
Lakini kwa kukubali kuweka kazi, kwenye mambo ya msingi kwa kurudia rudia bila kuchoka, maisha yanakuwa rahisi.
Tuangalie mfano wa eneo la fedha. Ili kujiweka vizuri kwenye eneo la fedha, unahitaji kufanya mambo mawili tu rahisi; kuongeza kipato na kudhibiti matumizi.
Hayo ni rahisi kabisa ambayo kila mtu anaweza kuelewa na kufanya.
Lakini sasa, angalia vitu watu wanafanya kwenye eneo la fedha.
Mara kucheza sijui michezo gani, mara kuhangaika na aina za uwekezaji ambazo mtu mwenyewe hawezi kuelezea.
Yote hayo yanafanya zoezi zima kuwa gumu na hata kupelekea watu kupoteza fedha zaidi.
Kadhalika kwenye eneo la afya, unahitaji kufanya mambo rahisi tu ili kujenga afya bora; kula kwa usahihi na kufanya mazoezi.
Lakini unapoangalia mambo ambayo watu wanahangaika nayo kwenye eneo la afya, utashangaa kwa nini wanafanya mambo kuwa magumu zaidi ya yanavyopaswa kuwa.
Kinachofanya watu watafute ugumu kwenye maeneo mengi ya maisha yao ni kupenda vitu vipya kila wakati.
Urahisi wa maisha na mafanikio upo kwenye kufanya vitu vya msingi, kwa kurudia rudia kwa muda mrefu bila kuacha.
Wengi huwa hawana uvumilivu wa kurudia rudia yale ya msingi kwa muda mrefu. Huwa wanachoka haraka na kujikuta wamekimbilia kwenye mambo yanayoonekana ni mapya na ya kusisimua.
Huko ndiko wanafanya mambo kuwa magumu na kujichelewesha kupata matokeo waliyopaswa kuyapata.
Kwenye kila eneo la maisha yako, mafanikio hayatokani na kufanya mambo mapya na magumu, bali yanatokana na kufanya mambo ya msingi kwa msimamo bila kuacha.
Urahisi wa safari ya mafanikio upo kwenye kukubali kuweka kazi kwa muda mrefu bila kuchoka wala kukata tamaa.
Safari ya mafanikio huwa ngumu sana pale mtu anapoanza kutafuta njia za mkato na ambazo hazihusishi kufanya kazi.
Kwa kukwepa kazi na kutaka kurahisisha safari, wanaishia kufanya mambo kuwa magumu na marefu zaidi.
Kwenye kila eneo la maisha yako, jiulize mambo yapi ndiyo ya msingi kabisa kisha chagua kuweka kazi kwenye maeneo hayo kwa muda mrefu bila kuacha.
Mambo ya msingi bado yanafanya kazi na ni sahihi kwenye safari ya maisha na mafanikio.
Tukomae na hayo na kuacha kupoteza muda na nguvu kwenye njia za mkato.
#NidhamuUadilifuKujituma
#AfyaUtajiriHekima
#KaziUpendoHuduma
#UpekeeUdadisiUbunifu
#UshirikianoUtegemeanoUwajibikaji
#BilioneaMafunzoni
#NajengaBiashara
#HakunaKingineMuhimu
#LazimaNitoboe
#NawekaKaziNifanikiwe
Urahisi wa safari ya mafanikio upo kwenye kukubali kuweka kazi kwa muda mrefu bila kuchoka wala kukata tamaa.
LikeLike
Hakika.
LikeLike
Nitafanya mambo ya msingi tu kwakujirudiarudia ili kuvutia mafanikio zaidi
LikeLike
Vizuri.
LikeLike
Asante Kocha kwenye hili la afya ni muhimu sana kuzingatia chakula na mazoezi.
LikeLike
Karibu
LikeLike
Tufanye mambo kwa urahisi
Tule tufanyemazoezi
Tuongeze mauzo tuzibiti matumizi mambo marahisi sana tu tukiyafuata na kuachana na starehe au kupenda uaraka na vitu vizurivizuri
LikeLike
Kabisa.
LikeLike
Asante kcha
Mafanikio hayatokani na kufanya mambo mapya na magumu,bali yanatokana na kufanya mambo ya msingi kwa msimamo bila kuacha.
LikeLike
Mambo ya msingi ndiyo yenye kila tunachohitaji.
LikeLike
Mambo gani ni ya msingi sana kwangu? Baada ya kujua nakaa hapo kwa msimamo. Asante Kocha.
LikeLike
Hakika
LikeLike
Kwenye kila eneo la maisha yako, mafanikio hayatokani na kufanya mambo mapya na magumu, bali yanatokana na kufanya mambo ya msingi kwa msimamo bila kuacha.
Asante sana
LikeLike
Kweli.
LikeLike
Asante kwenye eneo la fedha, mambo ya msingi kufanya kwa kujirudia kwa msimamo ni kuongeza kipato, kudhibiti matumizi, kudhibiti madeni, kufanya uwekezaji, kuweka akiba. Mengine ni magumu sana na hatari
LikeLike
Kabisa.
LikeLike
Watu wanayafanya maisha kuwa magumu pale wanapokuwa wanatafuta njia za mkato ili kukwepa kuweka kazi.
LikeLike
Kabisa
LikeLike
Asante Kocha,
Utajiri namba moja ni afya, tuzingatie lishe bora na mazoezi ya mwili.
LikeLike
Hakika
LikeLike
Nitajitahidi kuyarahisisha maisha yangu kwa kufanya yaliyo ya msingi tu. Punguza matumizi, ongeza kipato, Kula kwa afya na kufanya mazoezi
LikeLike
Vizuri
LikeLike
ASANTE sana
LikeLike
Karibu
LikeLike
Ili ufanikiwe ongeza kipato na punguza matumizi.
LikeLike
Rahisi na ya uhakika.
LikeLike
Urahisi wa maisha na mafanikio upo kwenye:
1. Kufanya vitu vya msingi
2. Kufanya vitu kwa kurudia rudia
3. Kufanya vitu kwa muda mrefu
4. Kufanya vitu bila kuacha.
Na hakuna njia ya mkato na ambayo haihusishi kufanya kazi.
LikeLike
Njia za mkato zinakuacha na mikato mingi.
LikeLike
Katika Maisha chagua Mambo ya msingi Kisha yafanyie kazi kwa nidhamu Kali na kwa kurudia rudia kwa muda
Mlefu na kwa msimamo lazima utafanikiwa.
Asante kocha
LikeLike
Karibu
LikeLike
Asante kocha mimi nimechagua kwa kila eneo ambalo nalifanyia kazi nifanye tu mambo ya msingi ili niyavitie mafanikio
LikeLike
Vizuri.
LikeLike
Asante kocha,nitapambania mambo ya msingi kuliko kutafuta urahisi na kutofanikiwa.
LikeLike
Kila la kheri.
LikeLike
Mambo ya .msingi ni sahihi na ndio maana maisha ya mafanikio yanafanyika
LikeLike
Kabisa.
LikeLike
Safari ya mafanikio huwa ngumu sana pale mtu anapoanza kutafuta njia za mkato na ambazo hazihusishi kufanya kazi.Asante Kocha.
LikeLike
Kabisa.
LikeLike
Asante sana kocha, kwenye safari ya mafanikio kuachana na njia za mkato, muhimu sana kongeza kipato na Kudhibiti matumizi
LikeLike
Hakika
LikeLike
Nitafanya mambo ya msingi kwa msimamo bila kuacha. Asante sana kocha
LikeLike
Vizuri.
LikeLike