3095; Ongeza shinikizo.
Rafiki yangu mpendwa,
Vitu vyote imara kwenye maisha huwa vinatengenezwa kwa shinikizo kubwa.
Madini ya almasi, ambayo ndiyo magumu zaidi na yenye thamani kubwa, ni mkaa ambao umepita kwenye shinikizo kubwa na kwa muda mrefu.
Hivyo pia ndivyo ilivyo kwa watu, watu wanaofanikiwa sana, ambao pia ndiyo huwa watu imara zaidi, huwa wanapitia shinikizo kubwa kwenye maisha yao.
Dan Pena, ambaye ni Kocha wa ufanisi mkubwa, huwa anasema kizazi cha sasa hakiwezi kupata mafanikio kwa sababu ni laini sana na kikipitia shinikizo kinalegea badala ya kuwa imara.
Watu wengi huwa hawapendi kukutana na ugumu au changamoto kwenye maisha yao.
Hivyo huwa wanakazana kutafuta njia rahisi na kukwepa njia ambazo ni ngumu.
Cha kushangaza, kwenye kukwepa ugumu, kunawaacha wakiwa laini na wasioweza kukabiliana na chochote.
Sehemu ya mafanikio makubwa ni uimara wa kukabiliana na wajibu ambao unaambatana na mafanikio hayo.
Wengi kwa kukosa uimara wa kutosha, huwa wanashindwa kuyahimili hata mafanikio madogo wanayopata, hivyo wanayapoteza.
Shinikizo ndiyo nishati inayokusukuma upate mafanikio makubwa.
Shinikizo linakupa njaa na hasira ya kukusukuma kufanya vitu vipya na vikubwa zaidi.
Bila ya shinikizo, watu huwa wanarudi kwenye mazoea na uzembe ambao wamekuwa wanafanya mara nyingi.
Unapaswa kuchukua hatua za hatari zaidi.
Chochote unachohofia kufanya, hicho ndiyo unapaswa kuanza kukifanya mara moja.
Hofu unayokuwa nayo juu ya kitu fulani ni kiashiria kwamba kitu hicho ni kipya na kikubwa kwako.
Ukiacha kufanya kwa sababu ya hofu, unakuwa umekwepa shinikizo na hivyo kujinyima fursa ya ukuaji.
Bila ya kuchukua hatua kubwa na za hatari.
Bila ya kufanya yale unayohofia kufanya.
Bila ya kupita kwenye shinikizo kubwa.
Huwezi kupata mafanikio makubwa kwenye maisha yako.
Kila wakati wa maisha yako, unapaswa kuwa kwenye shinikizo ambalo unalifanyia kazi.
Adui mkubwa wa mafanikio makubwa ni kuwa kwenye utulivu na kuridhika kwa muda mrefu.
Usikubali kuwa kwenye hali hiyo ya utulivu na kuridhika hata kwa muda mfupi.
Kila wakati tengeneza hali zinazokupa shinikizo ili likusukume kufanikiwa.
Kila unapojiona ukiea kwenye hali ya utulivu na kuridhika, chukua hatua zinazokuweka kwenye hatari na hivyo kusukumwa kuchukua hatua za tofauti.
Kuna hatua nyingi za hatari unazoweza kuchukua ili kujiweka kwenye shinikizo ambalo litakusukuma kufanikiwa.
Unaweza kuchukua mkopo ambao ni mkubwa, ambao utakusukuma ufanye zaidi ili uweze kuuza zaidi na kulipa deni.
Pia unaweza kuwaahidi watu vitu vikubwa na ambavyo havijazoeleka.
Ahadi hiyo inaambatana na adhabu kubwa kama utashindwa kuitekeleza. Hilo litakupa shinikizo kubwa la kuhakikisha unatekeleza.
Kwa kifupi, pale unapojikuta una raha, utulivu na kuridhika, usijisifie kwamba umeshafanikiwa, bali shtuka kwa sababu upo kwenye njia ya upotevu.
Kila wakati unapaswa kuwa chini ya shinikizo fulani.
Kila wakati unapaswa kuwa kwenye hali ya kujisukuma zaidi.
Hiyo ndiyo inayokufanya uwe imara zaidi na ujenge mafanikio makubwa.
#NidhamuUadilifuKujituma
#AfyaUtajiriHekima
#KaziUpendoHuduma
#UpekeeUdadisiUbunifu
#UshirikianoUtegemeanoUwajibikaji
#BilioneaMafunzoni
#NajengaBiashara
#HakunaKingineMuhimu
#LazimaNitoboe
#NawekaKaziNifanikiwe
Kila unapojiona ukiwa kwenye hali ya utulibu na kuridhika, chukua hatua zinazokuweka kwenye hatari na hivyo kusukumwa kuchukua hatua za tofauti.
LikeLike
Kabisa.
LikeLike
Kila unapojiona ukiwa kwenye hali ya utulivu na kuridhika, chukua hatua zinazokuweka kwenye hatari na hivyo kusukumwa kuchukua hatua za tofauti.
LikeLike
Asante Kocha,
Nitakuwa kwenye shinikizo daima, hali ya kunisukuma kuchukua hatua kufanya makubwa zaidi.
LikeLike
Vizuri
LikeLike
Nk kweli ukikaa bila kudaiwa utalala na kubweteka lakini ukiwa unadaiwa hata usinguzi hautakuja kabisa
LikeLike
Kabisa.
LikeLike
Shinikizo ndiyo njia nzuri ya kuyaelekea mafanikio makubwa.
LikeLike
Hakika.
LikeLike
Comfort zone is not a success procedure. Shinikizo linatuweka kwenye ukuaji na hamasa ya kufanikiwa zaidi kuliko Hali tulivu. Sintakaa kwenye utulivu na Mazoea, niweka shinikizo kwenye maisha yangu ili kupiga hatua kubwa muda wote wa maisha yangu
LikeLike
Vizuri
LikeLike
Kila wakati napaswa kuwa chini shinikizo na kila wakati napaswa kuwa katika hali ya kujisukuma zaidi.
Asante kocha.
LikeLike
Vizuri
LikeLike
Nikweli kocha ukikaa umetulia na pia umeridhika na mafanikio madogo ambayo unayo juwa upo kwenye hatari kwasababu gharama zako zao haziwezi kutulia huwa zinaongezeka mara zote Kwa hiyo inatubidi tuendelee kujisukuma sana
LikeLike
Hakika
LikeLike
Nikweli kocha mutu akikaa umetulia na pia umeridhika na mafanikio madogo ambayo anayo juwa upo kwenye hatari kwasababu gharama zako zao haziwezi kutulia huwa zinaongezeka mara zote Kwa hiyo inatubidi tuendelee kujisukuma sana Asante sana kocha
LikeLike
Asante sana kocha,sio kufurahia tu,bali kila mara natakiwa kuwa juu ya shinikizo binafs ktk kufikia lengo langu la mauzo ili kuweza kujisukuma zaidi.
LikeLike
Vizuri.
LikeLike
Adui mkubwa wa mafanikio makubwa ni kuwa kwenye utulivu.
Usikubali kuwa kwenye utulivu hata kwa muda mfupi, chukua hatua za Hatari zaidi.
LikeLike
Hakika
LikeLike
Hali ya utulivu na kuridhika kunaua biashara na hatimaye kukosa mafanikio. Asante kocha kwa somo
LikeLike
Karibu
LikeLike
Mtapambana mara zote kuwa na shinikizo ili kuchukua hatua kubwa kwenye maisha kwa kujifunza zaidi
LikeLike
Vizuri
LikeLike
Asante kocha,Kila mara inabidi niwe na shinikizo fulani ,hii ndo inanifanya niwe imara zaidi kwenye mafanikio.
LikeLike
Vizuri
LikeLike
Ahsante sana kocha, nitajipa shinikizo zaidi kila ninapojiona nimeridhika ili kupiga hatua zaidi kwakutoa ahadi za malengo makubwa zaidi
LikeLike
Vizuri
LikeLike
Kwa kifupi, pale unapojikuta una raha, utulivu na kuridhika, usijisifie kwamba umeshafanikiwa, bali shtuka kwa sababu upo kwenye njia ya upotevu.
Kila wakati unapaswa kuwa chini ya shinikizo fulani.
Kila wakati unapaswa kuwa kwenye hali ya kujisukuma zaidi.
Hiyo ndiyo inayokufanya uwe imara zaidi na ujenge mafanikio makubwa.
Asante sana
LikeLike
Hakika
LikeLike
Kawaida ni adui wa mafanikio.Kila mara nitajisukuma zaidi kwa malengo makubwa zaidi.
LikeLike
Vizuri
LikeLike
Ni kweli kabisa. Hata mimea inapokuwa kitaluni,kabla ya kupelekwa kupandwa shambani huinakuwa subjected kwenye mazingira magumu (hardenning off)kama bile kunyimwa maji,kuondolewa kivuli. Lengo ni kuiandaa kwa ajili ya kufanya vizuri shambani. Mimea isipopitishwa katika hali hii h
uwa haifanyi vizuri shambani.
LikeLike
Kabisa.
Na mimea inayoota eneo lenye maji mengi, mwanga wa kutosha na hakuna misuko suko kama upepo, huwa inakuwa dhaifu na hata mazao yake kama mbao haziwi imara.
Shinikizo ni muhimu kwenye kuimarisha kila kitu.
LikeLike
Bila ya kuchukua hatua kubwa na za hatari.
Bila ya kufanya yale unayohofia kufanya.
Bila ya kupita kwenye shinikizo kubwa.
Huwezi kupata mafanikio makubwa kwenye maisha yako.
Asante sana
LikeLike
Hakika
LikeLike
Unapaswa kuchukua hatua za hatari zaidi.
LikeLike
Kabisa
LikeLike
Kila wakati wa maisha yangu, napaswa kuwa kwenye shinikizo ambalo nalifanyia kazi.Kamwe sitakiwi niwe kwenye utulivu.
LikeLike
Kabisa
LikeLike
Asante sana kocha,nipo kwenye shinikizo kubwa sana na ujumbe huu unanijulisha kwamba njia hiyo ni sahihi. Asante na siku njema
LikeLike
Endelea kuwa imara.
LikeLike
Kila mara nitajiweka kwenye shinikizo kubwa ili kufanikiwa…
LikeLike
Vizuri
LikeLike
Bila ya kupitia kwenye shinikizo kubwa kamwe hutaweza kupata mafanikio makubwa kwa sababu
Shinikizo ndio nishati inayokusukuma upate mafanikio
Makubwa.
Asante kocho kwa ( kitendea kazi)
LikeLike
Vizuri
LikeLike
Asante Kocha, kila wakati natakuwa kwenye hali ya shinikizo yaani nitajisukuma kila siku.
LikeLike
Vizuri
LikeLike
Sitaweza kupata mafanikio makubwa kwenye maisha yangu bila ya kuchukuwa hatua kubwa na za hatari, kufanya yale ninayohofia kufanya au bila ya kupitia kwenye shinikizo kubwa.
LikeLike
Hakika
LikeLike
Usikubali kukaa kwenye hali hiyo ya utulivu kwa muda mrefu
LikeLike
Kweli
LikeLike
“Madini ya almasi, ambayo ndiyo magumu zaidi na yenye thamani kubwa, ni mkaa ambao umepita kwenye shinikizo kubwa na kwa muda mrefu.”
Kama hivi ndivyo basi hakuna chenye thamani kama msongo/shinikizo kwenye uhai na ustawi.
Asante
LikeLike
Hakika, shinikizo ndiyo linaimarisha kila kitu.
LikeLike
Shinikizo linakupa njaa na hasira ya kukusukuma kufanya vitu vipya na vikubwa zaidi.
LikeLike
Ndiyo
LikeLike