3098; Tatizo la uongo.
Rafiki yangu mpendwa,
Chanzo kikubwa cha msongo kwenye maisha ya wengi ni uongo.
Pale maisha ya mtu yanapokuwa tofauti na uhalisia wake, msongo mkubwa unajengeka ndani yake.
Chanzo cha msongo huo mkubwa huwa ni hali ya kuigiza kitu ambacho hakipo.
Watu huwa hawalioni tatizo la uongo kwa haraka.
Awali wanaanza na uongo kidogo, ili kuwashawishi watu kwa namna fulani.
Sasa changamoto inakuwa ili kutunza uongo mdogo wa awali, inabidi watumie uongo mkubwa zaidi ya huo wa awali.
Ni katika kutumia uongo mkubwa kufunika uongo wa nyuma ndiyo mtu anajikuta amezama kwenye shimo kubwa la uongo ambao inakuwa vigumu kuendelea kuuficha.
Hitaji la kuendelea kuficha uongo ambao unaendelea kukua ndiyo chanzo kikubwa cha msongo kwenye maisha ya watu.
Wanakuwa walianza na uongo kidogo, tena ambao hawakumaanisha sana, lakini wanakuja kujikuta kwenye shimo kubwa ambalo ni vigumu kutoka.
Kinachowafanya watu wadanganye ni kutaka kuwaridhisha wengine.
Kwa kuwa ukweli ni mchungu na haubembelezi, wengi huona ni rahisi kudanganya kuliko kueleza ukweli.
Wanachokuwa hawajui ni kwamba ukweli huwa unakuwa mchungu, lakini hauna mzigo wa kuendelea kubeba.
Uongo huwa unakuwa rahisi, lakini ugumu wake ni uzito wa kuendelea kuubeba kwa muda mrefu.
Kupunguza msongo kwenye maisha yako, ili pia uweze kupeleka umakini wako wote kwenye safari yako ya mafanikio, mara zote kuwa mkweli.
Kuwa halisi kwako na usidanganye wala kuishi maisha ya kuigiza ili kuwaridhisha wengine.
Kuwa mkweli mara zote kunaweza kuwaudhi baadhi ya watu.
Na hilo ni sahihi kabisa, kwa sababu kama inabidi udanganye ili kuwaridhisha watu, bado utakuja kuwaudhi tu, tena kwa ukubwa zaidi.
Kama unatumia uongo ili usiwapoteze watu, bado utakuja kuwapoteza tu, tena kwa maumivu makubwa zaidi.
Kama inabidi usiwe halisi kwako ndiyo uweze kuwabakisha watu fulani kwenye maisha yako, bado tu utawapoteza.
Kwa sababu uongo huwa hauna maisha marefu.
Ni bora kuwa mkweli na ukawapoteza watu mapema, ili ufungue njia sahihi kwako.
Kitu ambacho watu huwa wanakihofia kwenye kuwa wakweli ni kukosa baadhi ya fursa.
Lakini ukweli ni kwa kila fursa unayoipata kwa kutumia uongo, kuna nyingine nyingi bora zaidi unazokuwa umezikosa.
Ni vile wengi huwa hawana uwezo wa kuona hilo, ila ukweli ni uongo una gharama kubwa kuliko ukweli.
Ukiwa mkweli mara zote, maisha yatakupeleka kwenye uelekeo sahihi, ambapo utakutana na fursa ambazo ni bora kuliko zile unazokuwa umezipoteza.
Sema ukweli kama ulivyo,
Ishi kwa uhalisia wako,
Ambatana na wale ambao wanaweza kuhimili ukweli,
Na weka juhudi kubwa sana kwenye kila unachotanya.
Kwa kuzingatia hayo, utaweza kujenga mafanikio unayoyataka.
Kila unapokuwa na msongo kwenye maisha yako, anza kwa kujiuliza ni wapi hujawa mkweli kwenye maisha yako. Angalia ni wapi hujauishi uhalisia wako kama ulivyo.
Ukiyajua hayo na kuyatatua, utaweza kupunguza sehemu kubwa ya msongo kwenye maisha yako.
#NidhamuUadilifuKujituma
#AfyaUtajiriHekima
#KaziUpendoHuduma
#UpekeeUdadisiUbunifu
#UshirikianoUtegemeanoUwajibikaji
#BilioneaMafunzoni
#NajengaBiashara
#HakunaKingineMuhimu
#LazimaNitoboe
#NawekaKaziNifanikiwe
Uongo huwa unakuwa rahisi, lakini ugumu wake ni uzito wa kuendelea kuubeba kwa muda mrefu.
LikeLike
Kabisa
LikeLike
Kupunguza msongo kwenye maisha, ili pia uweze kupeleka umakini wako wote kwenye safari ya mafanikio, mara zote kuwa mkweli.
LikeLike
Hakika
LikeLike
Njia bora ni kupunguza msongo wa mawazo ili kuwekeza nguvu kwenye mambo machache
LikeLike
Hakika
LikeLike
Kusema ukweli daima bila kuona utawapoteza wangapi kwenye kusema ukweli huo badala ya kusema uongo na kuja kuumbuka baadae
LikeLike
Kama ni wa kupotea, watapotea tu, hata udanganyeje.
LikeLike
Unaweza kufanikiwa kwa muda mfupi kusema uongo ili kupata kile unachotaka, Lakini pale ukweli utakapojulikana utakuwa umepoteza sifa ya uaminifu kwa wale waliokusaidia.
LikeLike
Kabisa
LikeLike
Kwa kiasi kikubwa naona ukweli ukiendana na kusema hapana.Ni kupitia ukweli tunajiweka huru.
LikeLike
Kabisa, maana ndiyo nyingi huwa ni za uongo.
LikeLike
Ukweli unakuweka huru na kuondoa msongo
Asante sana
LikeLike
Karibu
LikeLike
Nitasema ukweli mara zote na kuishi katika ukweli huo ili kujenga mafanikio makubwa.
LikeLike
Kila la kheri.
LikeLike
Tumia ukweli uwe huru na uelekee kwenye njia sahihi kuliko Uongo ambao unanjia fupi. Mienajua madhara ya Uongo na sipendi kuutumia labda pale ninapokuwa nahitaji kuokoa maisha ya mtu.
LikeLike
Vizuri sana.
LikeLike
Ili maisha yanipeleke kwenye uelekeo sahihi,napaswa kuwa mkweli mara zote.
LikeLike
Kabisa
LikeLike
Kuwa mkweli kwako mwenyewe itakusaidia kuishi maisha ya furaha.
Asante sana
LikeLike
Kabisa
LikeLike
Acha uongo kuwa halisi.
LikeLike
Ndiyo.
LikeLike
Nikweli kabisa
LikeLike
Ndiyo
LikeLike
Kuwa mkweli kwenye mambo machache unayofanya ili kuondoa msongo
LikeLike
Ndiyo.
LikeLike