3100; Wanakutangaza vizuri.
Rafiki yangu mpendwa,
Maisha huwa yanachanganya sana.
Unapokuwa chini na hujafanikiwa, watu wako wa karibu wataonyesha kukupenda na kukuonea huruma.
Kwa sababu nao wanakuwa hawajafanikiwa, wanakuwa wanafarijika sana kuwa karibu na wewe.
Lakini mambo yanabadilika sana pale unapoamua kushika hatamu ya maisha yako na kufanikiwa.
Unapochagua kuweka juhudi kubwa ili kuyabadili maisha yako na kufanikiwa na ukaanza kupata matokeo ya tofauti, utaanza kutengeneza maadui.
Wale waliokuwa wa karibu kwako ndiyo wanaokuwa na chuki kubwa kwako kwa sababu ya mabadiliko yanayokuwa yanaendelea kwenye maisha yako.
Kibinadamu hilo jambo linaumiza sana.
Watu wako wa karibu ambao ulitegemea wayafurahie mafanikio yako, wanakuwa wa kwanza kuyachukia na kujenga uadui na wewe.
Na kikubwa kinachowafanya watu wako wa karibu wakuchukie pale unapofanikiwa kuliko wao ni kwa sababu mafanikio yako yanaonyesha uzembe wao.
Watu hao wana sababu nzuri kwa nini hawajafanikiwa. Wewe kufanikiwa kunaharibu sababu zao, kitu ambacho hawawezi kukipenda.
Kibinadamu, hiyo hali inaumiza na unaweza kutamani hata uachane na mafanikio ili ukubalike na kupendwa na hao watu wako wa karibu.
Lakini kamwe usije ukafanya hivyo, kwa sababu kwenye hiyo safari yako ya mafanikio unahitaji sana watu wenye chuki na wewe.
Kuwa na watu wenye chuki na wewe kuna faida nyingi, lakini kubwa mbili ni;
Moja ni kiashiria kwamba upo kwenye njia sahihi. Inatakiwa ikupe wasiwasi mkubwa kama kila mtu anakubaliana na wewe na kufurahia kila unachofanya. Hali ikiwa hivyo ni kiashiria hakuna makubwa na ya tofauti unayofanya.
Mbili ni wenye chuki na wewe huwa wanakutangaza vizuri sana kuliko hata wale wanaokupenda. Wale wanaokuchukia watahakikisha wanakusanya watu wengine wengi ambao wanakuchukia pia. Hivyo wataweka juhudi kubwa sana kusema mambo yako mabaya, yawe ya kweli au ya uongo, ili uchukiwe na wengi zaidi.
Ni kupitia kutaka kwao kukuchonganisha na walio wengi ndiyo wanazidi kukutangaza zaidi.
Wale wanaokuchukia wanakutangaza kwa juhudi na msimamo mkubwa kuliko hata wale wanaokupenda.
Wanaokupenda mara nyingi wataonyesha kukukubali wao wenyewe na hawatahangaika sana na wengine ambao hawakupendi.
Lakini wasiokupenda huwa wanataka kuona wengine wengi nao pia hawakupendi.
Ni hitaji hilo ndiyo linawafanya wawe watangazaji wako wazuri. Wanawafikia wengi zaidi kuwaonyesha ubaya wako.
Kadiri wengi wanavyosikia kuhusu wewe, hata kama ni kwa ubaya, ndivyo pia unavyozidi kuwafikia wengi sahihi.
Kuna ambao watakujua kwa mabaya, lakini wanapokufuatilia wanagundua wewe siyo mbaya kama unavyosemwa. Na hao watakuwa na manufaa makubwa kwako.
Kwa maana hiyo basi, unapaswa kuwapenda sana wale wanaokuchukia, kwa sababu wana mchango mzuri sana kwenye mafanikio yako.
Na kwa sababu wenye chuki na wewe wanakutangaza sana, wape shoo nzuri, wape vitu ambavyo vitachochea chuki kubwa kwao ili wasiweze kutulia kabisa. Chochea chuki zao kiasi cha kuwafanya waache majukumu yao ya msingi na wazidi kukutangaza kwa wengi zaidi.
Kwenye maisha, ni bora watu wakuchukie, kuliko wakudharau, kukupotezea au kutokukujua kabisa. Ni bora ujulikane hata kwa ubaya ambao siyo wa kweli, kuliko kutokujulikana kabisa.
Kwa hiyo basi, kama kuna watu wamejitolea kukutangaza bure kupitia chuki zao, watumie vizuri ili uweze kuwafikia wengi zaidi.
Lengo lako kwenye maisha halipaswi kuwa kutokuchukiwa au kupendwa na kila mtu.
Bali lengo lako kwenye maisha linapaswa kuwa ni kufanikiwa. Na unapofanikiwa, lazima utatengeneza watu wanaokuchukia, siyo kwa sababu zako, bali kwa sababu zao wenyewe.
Jua hao wanaokuchukia ni watu wanaokutangaza kwa nguvu hivyo watumie vizuri kuwafikia wengi unaowalenga.
Badala ya kuacha safari ya mafanikio ili usichukiwe na wengi, ichochee zaidi safari hiyo ili wale wenye chuki wakutangaze kwa wengi zaidi.
Na kupitia chuki zao kali, ndivyo pia wanavyokuweka kwenye nafasi ya kuwafikia wengi ambao watakupenda na kukukubali sana.
Kwa vyovyote vile, kuwa na watu wanaokuchukia ni ushindi mkubwa kwenye maisha yako, utumie vizuri ushindi huo.
#NidhamuUadilifuKujituma
#AfyaUtajiriHekima
#KaziUpendoHuduma
#UpekeeUdadisiUbunifu
#UshirikianoUtegemeanoUwajibikaji
#BilioneaMafunzoni
#NajengaBiashara
#HakunaKingineMuhimu
#LazimaNitoboe
#NawekaKaziNifanikiwe
Kuwa na watu wanaonichukia kwenye maisha yangu ni ushindi mkubwa kwenye maisha yangu
LikeLike
Ndiyo
LikeLike
Kuwa na watu wanaokuchukia ni ushindi mkubwa kwenye maisha yako, sina budi kuutumia vizuri ushindi huo.
LikeLike
Hakika
LikeLike
Kuwa na watu wanaokuchukia ni is ishara kuwa kuna kitu unafanya na ni mafanikio.Nitapambana kufikia mafanikio ninayoyahitaji na kuwaacha wenye chuki na mimi waendelee kunitangaza kwa wengine wengi.
LikeLike
Vizuri
LikeLike
Kuwa na watu wanao kuchukia ni ishara tosha ya mafanikio
LikeLike
Kabisa
LikeLike
Asante Kocha kwa ujumbe nilikuwa nawaza ni kwa nini watu hujitokeza kuchukia wengine hata kama hakuna chochote unachofanya dhidi yao. Asante
LikeLike
Ndiyo asili ya binadamu ilivyo.
LikeLike
Asante sana kocha, sitaacha kufanya kitu kwa sababu nachukiwa nitaendelea kupiga hatua tu.
LikeLike
Vizuri
LikeLike
Nitawatumia wanaonichukia kama sababu ya kupiga hatua zaidi katika biashara yangu. Asante kocha
LikeLike
Vizuri
LikeLike
Kwenye maisha, ni bora watu wakuchukie, kuliko wakudharau, kukupotezea au kutokukujua kabisa. Ni bora ujulikane hata kwa ubaya ambao siyo wa kweli, kuliko kutokujulikana kabisa.
Kwa hiyo basi, kama kuna watu wamejitolea kukutangaza bure kupitia chuki zao, watumie vizuri ili uweze kuwafikia wengi zaidi.
LikeLike
Tumia kila silaha kupata ushindi.
LikeLike
Kwenye maisha, ni bora watu wakuchukie, kuliko wakudharau, kukupotezea au kutokukujua kabisa. Ni bora ujulikane hata kwa ubaya ambao siyo wa kweli, kuliko kutokujulikana kabisa.
Asante sana
LikeLike
Vizuri
LikeLike
Heri kuonewa wivu kuliko kuonewa huruma
LikeLike
Ndiyo
LikeLike
Asant sana
LikeLike
Karibu
LikeLike
Asante kocha,Badala ya kuacha safari ya mafanikio ili nisichukiwe na wengi inabidi niichochee zaidi safari ili kusudi wanitangaze zaidi.
LikeLike
Ongeza kasi zaidi.
LikeLike
Lengo langu kwenye maisha ni kufanikiwa na sio kuchukiwa au kupendwa na kila mtu.
Habari njema ni kwamba watu wanaonichukia ndio wanaonitangaza kwa nguvu hivyo nitawatumia vizuri ili kuwafikia wengi ninaowalenga.
LikeLike
Kabisa.
LikeLike
Asante sana Kocha,
Watu wakikuchukia kwa sababu zao wenyewe, Shukuru, wanakutakia safari njema ya maisha yako ya mafanikio.
LikeLike
Kabisa
LikeLike
Wanaokuchukia ndio wanaokutangaza kuliko wanaokupenda.
LikeLike
Kweli.
LikeLike
Kwenye maisha, ni bora watu wakuchukie, kuliko wakudharau, kukupotezea au kutokukujua kabisa. Ni bora ujulikane hata kwa ubaya ambao siyo wa kweli, kuliko kutokujulikana kabisa.
Kwa hiyo basi, kama kuna watu wamejitolea kukutangaza bure kupitia chuki zao, watumie vizuri ili uweze kuwafikia wengi zaidi.
Asante sana Kocha Dr Makirita Amani
LikeLike
Kabisa.
LikeLike
Ni bora uchukiwe na na watu kuliko kupendwa
LikeLike
Kamilisha sentensi hii vizuri.
LikeLike
Kuchukiwa ni kiashilia kwamba uko kwenye njia sahihi
Shuklani kocha.
LikeLike
Karibu
LikeLike
Kama ukiona Kila mtu anakusifu na kukupenda ujue Bado hujafanya kitu kilichowastua watu.
LikeLike
Hakika
LikeLike
Kikubwa ni focus ili kufikia ushindi kila mtu atakuchukia kwa sababu zake mwenyewe
LikeLike
Hakika
LikeLike
Sitawachukia maadui zangu ili wanisaidie kunitangaza zaidi.
LikeLike
Vizuri
LikeLike
kuwa na watu wanaokuchukia ni ushindi mkubwa kwenye maisha yako,
LikeLike
Kabisa.
Ni dalili kuna makubwa unafanya.
LikeLike