3102; Ni kuwa bora, siyo kufurahia tu.
Rafiki yangu mpendwa,
Hakuna kipindi ambapo maarifa ya mafanikio yamekuwa yanapatikana kwa wingi na urahisi.
Lakini pia ndiyo wakati ambao watu wanaopata mafanikio makubwa wanayoyataka wamekuwa wachache sana.
Ni jambo la kushangaza, iweje maarifa ya mafanikio kupatikana kwa wingi na urahisi, lakini wanaofanikiwa kuwa wachache?
Zipo sababu nyingi, lakini moja kubwa ni mtazamo wa mtu anayejifunza. Watu wengi huwa lengo lao la kujifunza ni kufurahia. Hivyo wanajifunza vile vitu wanavyovitaka tu. Wanapokutana na kitu ambacho kinawataka wabadilike kwa namna fulani, wanaachana nacho.
Watu wachache huwa lengo lao la kujifunza ni kuwa bora. Hawa wanajifunza yote wanayokutana nayo na kuwa tayari kubadilika pale inapohitajika kufanya hivyo.
Ni watu hao wachache ndiyo wanaopata mafanikio makubwa.
Jipime wewe mwenyewe unaingia kwenye kundi lipi kati ya hayo mawili.
Je unajifunza ili kufurahia au kuwa bora?
Ni kujifunza kuwa bora ndiko kwenye fursa ya wewe kupiga hatua zaidi.
Kwenye kujifunza ili kufurahia unaishia kujifunza yale tu ambayo tayari unayajua na kukubaliana nayo. Unakuwa hukutani na ukweli ambao unatikisa mtazamo mzima ulionao.
Kwenye kujifunza ili kuwa bora unajifunza mambo mapya ambayo yanakutaka kubadilika kwa kiasi kikubwa.
Kwa kila unachojifunza, jiulize matokeo ya mwisho yamekuwa nini, umefurahia tu au umekuwa bora?
Anzia hapo ili uweze kufanya makubwa zaidi kwenye maisha yako.
#NidhamuUadilifuKujituma
#AfyaUtajiriHekima
#KaziUpendoHuduma
#UpekeeUdadisiUbunifu
#UshirikianoUtegemeanoUwajibikaji
#BilioneaMafunzoni
#NajengaBiashara
#HakunaKingineMuhimu
#LazimaNitoboe
#NawekaKaziNifanikiwe
Kwenye kujifunza ili kuwa bora unajifunza mambo mapya ambayo yanakutaka kubadilika kwa kiasi kikubwa.
LikeLike
Ndiyo.
LikeLike
Ni kujifunza na kubadilishwa na mafunzo na kuwa bora zaidi ya ulivyokua mwanzo
LikeLike
Kupiga hatua.
LikeLike
Kujifunza lengo lake ni kuwa bora si kujifurahisha tu.
LikeLike
Hakika
LikeLike
Niwe bora na niache kufurah pekee
LikeLike
Ndiyo.
LikeLike
Nitajifunza kwa kuwa bora na siyo kufurahia tu. Asante sana kocha
LikeLike
Vizuri sana.
LikeLike
Asante Kocha,
Nitajifunza kuwa bora kwani ndiyo kuna fursa ya mimi kupiga hatua zaidi.
LikeLike
Kila la kheri.
LikeLike
Asante kocha,Ili nijifunze na kuwa bora lazima nijifunze mambo mapya ambayo nitakuwa kwa kasi na kufanikiwa.
LikeLike
Ndiyo.
LikeLike
Najifunza ili kuwa Bora. Naangalia Mambo gani yaliyo kwenye habari niliyosoma ambayo mwandishi alitaka niyajue Kisha nachukia hatua. Kama Kuna ya kufurahiana bilanm shka nitafurahia Ila muhimu Ni kujifunza.
LikeLike
Safi sana.
LikeLike
Watu wachache huwa lengo lao la kujifunza ni kuwa bora. Hawa wanajifunza yote wanayokutana nayo na kuwa tayari kubadilika pale inapohitajika kufanya hivyo.
Ni watu hao wachache ndiyo wanaopata mafanikio makubwa.
LikeLike
Hakika.
LikeLike
Kwenye kujifunza ili kuwa bora unajifunza mambo mapya ambayo yanakutaka kubadilika kwa kiasi kikubwa.
Asante sana
LikeLike
Ndiyo.
LikeLike
Nitajifunza ili kuwa bora kila siku.
LikeLike
Kila la kheri.
LikeLike
Jifunze kuwa bora na siyo kujifunza kufurahia.
LikeLike
Hakika
LikeLike
Nitahakikisha kwa kila nitakachokisoma ninakisoma kwa lengo la kuwa Bora pia nitakua tayari kwa mabadiliko nitakayopaswa kuyafanya.
Asante kocha
LikeLike
Vizuri.
LikeLike
Mwongozo wangu uwe kwa kila matokeo ya mwisho yanifanye kuwa bora na siyo kufurahia tu.
LikeLike
Ndiyo.
LikeLike
Je unajifunza ili kufurahia au kuwa bora?
LikeLike
Swali muhimu sana.
LikeLike