3106; Kitu cha kwanza kufanya kila unapoamka asubuhi.
Rafiki yangu mpendwa,
Kwenye zama tunazoishi sasa, zama za teknolojia ambapo simu zetu janja (smartphones) zimeshika sehemu kubwa ya maisha yetu, huwa ndiyo kitu ambacho tunakigusa mara nyingi zaidi.
Huwa natania kwamba mtu anaweza kuamka asubuhi, kabla hata hajajua kama anaweza kutembea au la, tayari anakuwa ameshashika simu yake.
Na simu hizo watu wanazishika mara nyingi kuliko hata baadhi ya viungo vya miili yao.
Kwa kuwa simu hizo zina mambo mengi, mtu unaposhika ni rahisi kwenda kwenye mambo yasiyokuwa na tija kwako.
Ni rahisi kujikuta umeshaenda kwenye mitandao ya kijamii au kufuatilia habari mbalimbali.
Sasa hakuna njia mbaya ya kuianza siku yako kama kwa kufuatilia mambo ya wengine, kama mitandao ya kijamii au habari.
Hivyo basi, hata kama kila unapoamka utaishika simu yako mapema, kuna kitu nashauri kiwe cha kwanza kukifanya kwenye hiyo simu yako, ambacho kitakupa msukumo wa tofauti siku nzima.
Kitu hicho ni kuzihesabu fedha zako zote ulizonazo.
Utafanyaje hilo kwa kutumia simu nitakuambia, lakini kwanza tuanze na umuhimu wa kufanya zoezi hilo.
Wakati naanza kujifunza mambo haya ya maendeleo binafsi, nilimsoma mwandishi mmoja aliyeshauri mtu utembee na kiasi fulani cha fedha na uwe unakihesabu mara kwa mara.
Tunajua nguvu ya fikra zetu, kwamba huwa tunakuwa kile tunachofikiri kwa muda mrefu.
Hivyo kwa mtu kuhesabu fedha mara kwa mara, unakuwa unafikiri fedha kwa muda mrefu na hivyo kufanya fikra zako kukaa na mawazo hayo ya fedha, kitu chenye nguvu ya kukufanya uone fursa nyingi zaidi za kuzipata kwa wingi.
Inaweza isiwe rahisi kwako kuwa na kiasi fulani cha fedha unachohesabu kila mara.
Lakini hizi simu zetu janja, zina njia rahisi ya kuhesabu fedha zetu kila mara kwa urahisi.
Unafanya hivyo kwa kutumia aplikesheni mbalimbali za maeneo yote ambayo fedha zako zipo.
Hivyo anza kwa kuweka aplikesheni hizo kwenye simu yako kama bado hujafanya hivyo.
Kwa benki zote ambapo una akaunti, weka aplikesheni zake kwenye simu yako.
Kwa mitandao yote ya simu unayotumia huduma zake za kifedha, weka aplikesheni zake.
Halafu pia weka aplikesheni za uwekezaji wa masoko ya mitaji unayofanya. Kwa upande wetu ni UTT (vipande) na DSE (hisa na hatifungani).
Kwa kuwa na hizo aplikesheni ambapo akaunti zako zipo, ni rahisi kuangalia kiasi cha fedha kilichopo kwenye kila akaunti yako.
Hivyo basi, unapoamka asubuhi, cha kwanza kufanya unaingia kwenye hizo aplikesheni na kuangalia ni fedha kiasi gani unazo, kwenye kila akaunti na jumla.
Kwa kila akaunti, kuwa na lengo ni kiasi gani unataka kiwe huko.
Kisha kila siku angalia na kama ni pungufu, ianze siku yako kwa kujiuliza unaongezaje kiasi hicho na kufikia lengo?
Jiulize ni nini unatakiwa kwenda kuuza siku hiyo na kwa kiasi gani ili uweze kufikia lengo unalotaka?
Hapo utaianza siku kwa mtazamo tofauti kabisa.
Kama utakwama popote kwenye utekelezaji wa hilo, wasiliana na kule ambapo una akaunti zako na watakupa maelekezo sahihi ya kukamilisha hilo.
Kwa baadhi ya akaunti za benki, hasa za biashara unaweza ukashindwa kuona kwa aplikesheni, lakini ukaweza kuingia kwa mtandao na kuona, anza na hilo pia kila siku.
Usiianze siku yako kwa habari,
Usiianze siku yako kwa mitandao ya kijamii.
Usiianze siku yako kwa kufuatilia mambo ya wengine.
Bali anza siku yako kwa kuhesabu fedha zako zote (ukwasi) ulionao.
Na hapo ni kwa upande wa ukwasi zaidi, unaweza kuwa na uwekezaji mwingine uliofanya wa mali kama ardhi na majengo.
Huo siyo rahisi kuhesabu kila siku.
Unachotaka kuhesabu ni kile ambacho ni rahisi kugeuza kuwa fedha.
Kwenye ukurasa wa mbele wa simu yangu janja nina aplikesheni za Tigo pesa, Mpesa, NMB, CRDB na UTT. Nikishafungua mtandao kitu cha kwanza kufanya ni kuangalia salio kwenye akaunti zote hizo.
Na mara kwa mara kwa siku narudia kufanya hivyo, hata kama hakuna fedha mpya imeingia au nategemea iingie.
Lengo ni kuhakikisha kila wakati nafikiria malengo ya kifedha niliyonayo na pale nilipo kuyafikia.
Fanya zoezi hili kila unapoianza siku yako na mara kwa mara, lina nguvu kubwa ya kuweka fikra na mtazamo wako wa kifedha sawa.
#NidhamuUadilifuKujituma
#AfyaUtajiriHekima
#KaziUpendoHuduma
#UpekeeUdadisiUbunifu
#UshirikianoUtegemeanoUwajibikaji
#BilioneaMafunzoni
#NajengaBiashara
#HakunaKingineMuhimu
#LazimaNitoboe
#NawekaKaziNifanikiwe

Asante sana Kocha Dr Makirita Amani, application hizo tayari ninazo na mimeshaanza kufanyia kazi hilo.
LikeLike
Vizuri sana, muhimu kuzihesabu fedha zako kila siku.
LikeLike
Ni kweli kabisa mimi mwenyewe ninapoianza siku kwa kuangalia namba au kupiga hesabu fulani za fedha kuna nguvu fulani nakuwa nayo .
LikeLike
Kuna hasira kubwa unayotoka nayo pale unapoona namba za uhalisia ni tofauti sana na zile unazozitaka.
LikeLike
Hakika kujua pale nilipo kifedha na kule ninakopanga kwenda ni muhimu sana katika kuijenga vizuri saikolojia yangu ya fedha.
LikeLike
Ndiyo, inakupa msukumo mkubwa sana.
LikeLike
Ni kweli lazima uone ukwasi wako ukupe hasira ya kuongeza
LikeLike
Jua ukwasi wako kwenye kila dakika, itakusaidia sana kwenye kufanya maamuzi na kuchukua hatua sahihi.
LikeLike
Asante kocha kwa somo hili, ninaenda kulifanyia kazi
LikeLike
Kila la kheri.
LikeLike
Kuanzia sasa nitaianza Siku yangu kwa kuheabu fedha zangu.
LikeLike
Vizuri, tekeleza hilo kwa uhakika.
LikeLike
Asante Kocha.
Sitaianza siku yangu kwa habari, mitandao ya kijamii au kuwafuatilia watu wengine; Bali ukwasi. Nitaanza siku yangu kwa kuhesabu fedha zangu.
LikeLike
Safi sana, tekeleza kama ulivyoahidi.
LikeLike
Asante Sana kocha kwa ushauli huu Bora kabisa,
Ninafanyia kazi haraka iwezekanavyo.
LikeLike
Kila la kheri.
LikeLike
Asante sana kocha Kwa kunikumbusha hili.
Kuna kipindi nilikuwa na lengo langu na niliamua Kila siku nitaweka pesa kwenye mfuko huo.
Hivyo Kila nilipokuwa nikiongeza pesa zile nilikuwanazihesabu, kitendo kile kilinifanya nikamileshe lengo lile mapema na sikujua hata njia iliyonisukama kupata pesa Ile.
Ila Kwa SoMo la Leo nimegundua kumbe lilikuwa swala la kisaikolojia lilinisaidia kufikia kiasi kile mapema.
LikeLike
Vizuri sana, endelea na zoezi hilo kila siku ya maisha yako.
LikeLike
asante sana kocha.Uzuri hizo application zote ninazo tayati kwa simu yangu kitambo,ni mimi sasa kila siku kuangalia na kuweka lengo la kifedha kwa kila akaunti
LikeLike
Anza na hizo kila siku.
Na mara kwa mara angalia ukwasi wako.
Kwa sababu uzuri kufanya zoezi hilo ni bure kabisa.
LikeLike
Asante sana Kocha nafanyia kazi kuhakikisha ninazo application zote na niweke juhudi kwenye kuongeza kipato zaidi.
LikeLike
Kila la kheri.
LikeLike
Usiianze siku yako kwa habari,
Usiianze siku yako kwa mitandao ya kijamii.
Usiianze siku yako kwa kufuatilia mambo ya wengine.
Bali anza siku yako kwa kuhesabu fedha zako zote (ukwasi) ulionao.
Asante sama
LikeLike
Tuweke vipaumbele vyetu kwa usahihi.
LikeLike
Asante Kocha,nitaiangalia akaunti yangu ya biashara kila siku asubuhi
LikeLike
Kila la kheri.
LikeLike
Zoezi hili nimelikuwa nalifanya mara kwa mara lakini haikuwa kila siku na wala sikuwa na muda maalumu wa kufanya hivyo. Sasa naenda kuboresha kwa kuangalia fedha zangu kila ninapoamka.
Asante sana.
LikeLike
Safi sana, ukifanya hivyo unakuwa unaianza siku yako kwa msukumo mkubwa zaidi.
LikeLike
Asante kocha,Kila siku nitaakikisha naangalia fedha nilizonazo ili niweze kuona naweka nguvu wapi ili kufikia malengo.
LikeLike
Kila la kheri.
LikeLike
Nitaanza siku yangu kwa kuhesabu pesa zangu.
LikeLike
Safi sana.
LikeLike
Kitu cha kwanza kufanya ninapoamka asubuhi ni kuhesabu pesa zangu.
LikeLike
Vizuri sana.
LikeLike
Sijawahi kufanya hivyo, nitaanza kujitahidi kufanya hivyo ili inipe hasira na nguvu.
LikeLike
Vizuri, fanya kwa uhakika.
LikeLike
Usiianze siku yako kwa habari,
Usiianze siku yako kwa mitandao ya kijamii.
Usiianze siku yako kwa kufuatilia mambo ya wengine.
Bali anza siku yako kwa kuhesabu fedha zako zote (ukwasi) ulionao.
Na hapo ni kwa upande wa ukwasi zaidi, unaweza kuwa na uwekezaji mwingine uliofanya wa mali kama ardhi na majengo.
Huo siyo rahisi kuhesabu kila siku.
Unachotaka kuhesabu ni kile ambacho ni rahisi kugeuza kuwa fedha.
LikeLike
Tuzingatie sana hili.
LikeLike
Hili nalo nalo ni jambo. Ni kitu kidogo lakini kinaweza kuleta matokeo makubwa
LikeLike
Kabisa, inakufungua sana.
LikeLike