3118; Watu wengi wanataka ufanikiwe, mpaka utakapofanikiwa.
Rafiki yangu mpendwa,
Unapokuwa na malengo ya mafanikio makubwa, huwa unapata uungwaji mkono na watu walio wengi kwenye maisha yako.
Unaposhirikisha malengo na mipango mikubwa unayokuwa nayo, wengi wanafurahia kwa sababu unakuwa unawafanya wakumbuke malengo makubwa ambayo walikuwa nayo pia.
Watakutia sana moyo kwamba upambane na majibu mazuri yatakuja.
Unapambana kweli na unafanikiwa kwenye yale uliyopanga kufikia.
Ulitegemea wale waliokuwa wanakusifia wawe ndiyo wa kwanza kwanza kufurahia mafanikio yako.
Lakini kinachotokea kinakuwa ni kinyume kabisa na matarajio yako.
Watu walioonekana kukuunga mkono wakati unaanza, wanageuka na kuwa maadui wako wakubwa baada ya kufanikiwa.
Kuna sababu mbili zinazopelekea mafanikio yako kuwa chanzo cha wale waliokuwa wanakuunga mkono mwanzoni kubadilika na kuwa maadui wako.
Moja ni mafanikio yako yanaonyesha uzembe wao.
Kwa wewe kufanikiwa, kunawafanya wengine waonekane ni wazembe.
Hasa pale unapokuwa umeanzia chini kabisa na kufanikiwa, unawafanya wengine waonekane ni wazembe, wameshindwaje na wao kufanikiwa?
Kwa sababu hakuna anayependa kuonekana ni mzembe, inapelekea uchukiwe na wale wasiofanikiwa.
Mbili ni kukosa udhibiti kwako.
Watu wengi huwa wanapenda kuwa na udhibiti kwa watu wengine, kuwapangia nini cha kufanya, kwa namna gani na wakati gani.
Kadiri unavyofanikiwa ndivyo unavyozidi kuwapuuza watu na kuhangaika zaidi na mambo yako.
Hilo linafanya watu waone una kiburi na dharau, kwa sababu hawana tena udhibiti kwako.
Unachopaswa kufanya ni kuwapuuza wote wenye chuki na wewe.
Unapaswa kuendelea kuyapambania mafanikio makubwa zaidi unayoyataka.
Wale walioshindwa hawapaswi kuwa kikwazo kwako, badala yake wafanye kuwa kichocheo kwako kufanikiwa zaidi.
Wanaokuchukia kwa sababu ya mafanikio yako usiwachukie, bali waonee huruma.
Waonee huruma jinsi maisha yao yalivyo magumu kwa kuendeshwa na chuki.
Fikiria mtu anayeamka asubuhi na matumizi bora ya muda wa siku yake nzima ni kuwa na chuki kwa wengine.
Kwa hakika anakuwa na maisha magumu mno, huku akiwa hana anachovuna.
Wewe endelea kuweka umakini wako wote kwenye kujenga mafanikio makubwa zaidi kwako.
Uzembe uliowazuia wengine kufanikiwa haupaswi hata kupata nafasi kwako.
Mara zote baki ukiwa na udhibiti mkubwa sana kwako binafsi ili uwe huru kufanya kile unachotaka kufanya.
Hulazimiki kufanya yale wengine wanakutaka ufanye ili tu kuwaridhisha.
Nini maana ya wewe kujitesa na kupambana kufanikiwa kama utawaruhusu wakudhibiti vile wanavyotaka wao wenyewe?
Kwenye maisha yako, huwajibiki kukaa chini ya udhibiti wa kundi kubwa la ambao hawajafanikiwa.
Huhitaji hata kuwapa nafasi ya kukusumbua.
Unapaswa kuwapuuza kabisa.
Na hata wakikuambia mafanikio yamekupa kiburi na bila kuwasikiliza wao utaanguka, wacheke kabisa.
Maana kama ushauri wao ungekuwa unafanya kazi vizuri, kwa nini hawajautumia wao wenyewe kupata mafanikio makubwa?
Watu huwa wanapenda kujipa umaarufu na umuhimu wasiokuwa nao.
Wewe ni kuwapuuza tu na kuendelea na safari yako ya mafanikio makubwa.
#NidhamuUadilifuKujituma
#AfyaUtajiriHekima
#KaziUpendoHuduma
#UpekeeUdadisiUbunifu
#UshirikianoUtegemeanoUwajibikaji
#BilioneaMafunzoni
#NajengaBiashara
#HakunaKingineMuhimu
#LazimaNitoboe
#NawekaKaziNifanikiwe
ahsante kocha.
anayekuchukia akuanza kukuchukia wewe, alianza kujichukia yeye kwa kushindwa kutimiza mipango yake kisha kuja kukuchukia na wewe. (uwezi kutoa kitu ambacho huna uyo ana chuki ndani yake)
Ahsante
LikeLike
Huo ndiyo ukweli.
LikeLike
Watu huwa wanapenda kujipa umaarufu na umuhimu wasiokuwa nao, wewe ni kuwapuuza tu na kuendelea na safari yako ya mafanikio makubwa.
LikeLike
Hiyo ndiyo dawa.
LikeLike
Na hata wakikuambia mafanikio yamekupa kiburi na bila kuwasikiliza wao utaanguka, wacheke kabisa.
Maana kama ushauri wao ungekuwa unafanya kazi vizuri, kwa nini hawajautumia wao wenyewe kupata mafanikio makubwa?
Asante sana Kocha Dr Makirita Amani
LikeLike
Kabisa yani, tusikubali kutishwa kijinga, safari ya mafanikio yenyewe ni ya kutisha.
LikeLike
Ni kuwaonea huruma wapuuze na wewe kusonga mbele maana hakuna mahali watakusaidia chochote bali ni kuangalia kama utaanguka hiyo ni sawa na fisi anayesubiri mkono wa mtu udondoke aokotee atasubiri sana
LikeLike
Lazima tuwasubirishe sana.
LikeLike
Huu ni ukweli mchungu yaani mtu akifanikiwa mafariki na watu wako wa karibu ndiyo wa kwanza kukuchukia kwasababu mafanikio yanakua tishio kwao na wanageuka kuwa maadui kwasababu wengine watawaona kama wazembe kwa kuwauliza inawezekanaje huyo afanikiwe kuwashinda wakati munafanya kazi moja ? Kwa hiyo wajibu wangu nikuwapuuza nakuendelea na mambo yangu Asante kocha
LikeLike
Tuwapuuze tu, maana tayari maisha yanawaadabisha vya kutosha.
LikeLike
Wa puuze wavivu na endelea Kwa viwango vikubwa
Asante
LikeLike
Kabisa.
LikeLike
Naweka Nguvu na umakini wangu katika kujenga mafanikio makubwa zaidi.
LikeLike
Kila la kheri.
LikeLike
Asante Kocha,
Nitampuuza kila anayenichukia kwa sababu ya mafanikio yangu. Nitakuwa makini zaidi.
LikeLike
Kila la kheri.
LikeLike
Mafanikio yako yanaonyesha usembe wao ndio maana wanakuchukia.
LikeLike
Kabisa
LikeLike
Sitoruhusu Mtu yeyote ambae hajafanya makubwa kwenye Maisha yake avuruge maisha yangu
LikeLike
Vizuri sana.
LikeLike
asante sana
LikeLike
Karibu
LikeLike
Kumbe mafanikio yangu yanaonyesha uzembe wao, najitahidi Ili niweze nifanikiwe na nifikie mafanikio makubwa ya ubilionea kabisa. Asante Kocha.
LikeLike
Ndiyo
LikeLike
Kwenye safari ya mafanikio,nitapuuza kila yeyote atakayetaka kuvuluga maisha yangu hasa safari ya mafanikio.
LikeLike
Kila la kheri
LikeLike