3132; Viwango vimeshushwa sana.
Rafiki yangu mpendwa,
Watu wengi huwa wana tabia ya kulalamikia mfumo wa elimu kwamba viwango vya ufaulu vimeshushwa sana.
Kwa ufaulu mkubwa ambao watoto wa siku hizi wanakuwa nao, mtu yeyote aliyesoma zamani anaona kama angesoma zama hizi, basi na yeye angepata ufaulu mkubwa sana.
Na hapo mtu hajaweka urahisi wa kujifunza uliopo kwenye zama hizi ukilinganisha na zamani.
Mambo hayo ambayo wengi wamekuwa wanayaona kwenye mfumo wa elimu ni ya kweli kabisa.
Lakini unajua nini kingine cha kweli?
Ni viwango ambavyo vipo kwenye kila eneo la maisha.
Viwango vilivyopo kwenye kila eneo la maisha vimeshushwa sana kiasi kwamba yeyote anayeshindwa kwenye eneo lolote ni uzembe wake tu ndiyo unakuwa umechangia.
Tuangalie eneo la biashara, unafikiri mtu aliyeishi miaka 50 iliyopita atayaonaje mazingira ya mtu kuanzisha biashara kwa sasa?
Hebu fikiria ni mahitaji kiasi gani ambayo mtu alipaswa kuwa nayo miaka 50 iliyopita ili kuweza kuanza biashara.
Kwa hakika mahitaji ni mengi sana, kuanzia eneo la uhakika, mtaji mkubwa, watu na kadhalika.
Lakini angalia leo hii, mtu yeyote anaweza kuanzisha biashara yoyote anayoitaka bila ya kuwa na hayo matakwa yaliyohitajika kipindi hicho.
Leo hii mtu anaweza kuanzisha biashara bila ya kuwa na eneo, wala mtaji, wala watu.
Yaani mtu hahitaji hata kuwa na wazo bora na la tofauti.
Viwango vya kuanzisha biashara vimeshushwa mno kiasi kwamba mtu yeyote kutokuwa na biashara zama hizi ni uzembe wake tu.
Kadhalila ni viwango vya mafanikio kwenye eneo lolote lile la maisha.
Miaka mingi ya nyuma, mafanikio ya mtu kwenye maisha yalitegemea sana amezaliwa kwenye familia ya aina gani.
Na hapo ni awe na bahati asiwe amezaliwa kwenye familia ya watumwa, maana aliendelea kuwa mtumwa maisha yake yote.
Mtu aliyezaliwa kwenye familia ya kifalme, alikuwa na uhakika wa mafanikio.
Na aliyezaliwa kwenye familia ya kimasikini, hakuwa na namna ya kutoka kwenye huo umasikini.
Lakini hebu angalia leo hii, mtu yeyote anayetaka kufanikiwa, anaweza kufanya hivyo bila ya kuzuiwa na chochote.
Na hata mafanikio yenyewe ya kumpa mtu utofauti, siyo makubwa sana.
Kwa kuwa wengi kwenye jamii hawapambani kupata mafanikio makubwa, mafanikio yoyote madogo mtu anaweza kuyapata, yatamfanya aonekane wa tofauti kabisa.
Hapo hatujaangalia eneo la kujifunza.
Tukirudi nyuma miaka michache tu, kabla ya kuja kwa mapinduzi ya mtandao wa intaneti na simu janja, kujifunza kitu chochote lilikuwa zoezi moja gumu sana.
Kusoma vitabu ilikuwa mpaka uende maktaba na hapo ni ubahatike kupata kitabu ulichotaka.
Kujifunza taaluma au ujuzi wowote ilikutaka ujiandikishe kwenye vyuo na kusoma kwa miaka mingi.
Lakini leo hii, kwa kuwa tu na simu janja unaweza kujifunza kitu chochote kwa muda wowote ukiwa popote.
Unaweza kupata na kusoma kitabu chochote unachotaka.
Na pia unaweza kujifunza taaluma au ujuzi wowote unaoutaka ndani ya muda mfupi sana.
Viwango vya kujifunza vimeshushwa sana, inashangaza kwa nini wengi hawajifunzi.
Rafiki, tunaweza kuendelea na hilo kwenye kila eneo la maisha na kuona jinsi ambavyo viwango vya kufanikia kwenye kila eneo vimeshushwa sana.
Hivyo basi, kama hujafanikiwa kwenye eneo lolote lile la maisha yako, kuna sababu moja tu ambayo ni uzembe wako binafsi.
Kama umeshindwa kujitofautisha na kundi kubwa la watu ambao hawana mafanikio makubwa, jua umejitakia wewe mwenyewe.
Kwa jinsi viwango vya mafanikio vimeshushwa sana kwenye kila eneo, ni kujidharau kwa hali ya juu sana kama tutashindwa kuyapata mafanikio makubwa tunayoyataka.
Huhitaji hata nguvu kubwa sana kufanikiwa, unachohitaji ni usiwe tu mzembe, uache kufuata mkumbo na kushika njia yako.
Mtu aliyekuwa na kiu kubwa ya mafanikio, ila akafa miaka 50 iliyopita bila ya kufanikiwa, akifufuka leo atakufa tena akiwa na sonona.
Kwa sababu atashangaa sana jinsi mafanikio yamekuwa rahisi, halafu watu wengi bado hawajafanikiwa.
Atashindwa kabisa kuelewa iweje watu wanateseka wakati mambo yamerahisishwa sana?
Tusiwe sehemu ya wale watakaomwangusha mtu wa aina hiyo.
Badala yake tuwe sehemu ya kumfanys ajivunie, kwa kuona tumeweza kutumia vizuri fursa nyingi zinazopatikana kujijengea mafanikio makubwa.
Viwango vimeshushwa sana,
Ushindani umekuwa mwepesi mno,
Lakini pia nguvu ya kuturudisha nyuma nayo imekuwa kubwa.
Tusikubali kumezwa na nayo mazoea, badala yake tutumie vizuri fursa zinazotuzunguka kufanya makubwa.
Tuishi kwenye zama tulizopo sasa, tukiwa na njaa ya mafanikio waliyokuwa nayo watu wa zama zilizopita.
Kwa namna hiyo tutaweza kufanya makubwa sana.
#NidhamuUadilifuKujituma
#AfyaUtajiriHekima
#KaziUpendoHuduma
#UpekeeUdadisiUbunifu
#UshirikianoUtegemeanoUwajibikaji
#BilioneaMafunzoni
#NajengaBiashara
#HakunaKingineMuhimu
#LazimaNitoboe
#NawekaKaziNifanikiwe
Viwango vimeshushwa sana,
Ushindani umekuwa mwepesi mno,
Lakini pia nguvu ya kuturudisha nyuma nayo imekuwa kubwa.
Tutumie fursa hii ya viwango kushushwa kufanya makubwa.
Asante sana Kocha Dr Makirita Amani
LikeLike
Kabisa.
LikeLike
Sitakubali kumezwa na mazoe bali natumia vizuri fursa zilizonizunguka ili niweze kufanya makubwa kwenye maisha yangu, kwani zama hizi viwango vimeshushwa sana kwenye kila kitu sipaswi kuwa na sababu hata moja kwanini nisifanikiwe.
LikeLike
Vizuri.
LikeLike
Kwa kweli ni uzembe mkubwa kushindwa kufanikiwa katika zama hizi ambazo viwango vimeshushwa sana.
LikeLike
Ndiyo
LikeLike
Nisiishi kwa mazoea,viwango vimeshushwa sana.Nitumie vyema fursa zilizopo kupata mafanikio makubwa ninayoyahitaji.
LikeLike
Ndiyo
LikeLike
Ni kweli kabisa viwango vimeshuka ila pia viwango vimeongezeka
LikeLike
Ufafanuzi zaidi tafadhali, maana maelezo yako yanakinzana.
LikeLike
Kweli viwango vimeshushwa kama ninaweza kununua vipande kwenye simu wakati miaka 30 nyuma wazee wetu ilikuwa lazima waende kwenye ofisi husika kweli tunapaswa kupambana kufikia mafanikio kwa haraka.
LikeLike
Na hapo bado hajasafiri kwa siku kadhaa ndiyo aweze kufanikisha hilo.
Tusichukulie poa, tutumie vizuri hizi fursa za sasa ambazo watu wa nyuma hawakuwa nazo.
LikeLike
Ni kweli umaskini ni uzembe wa mtu maana uwezo wa kufanikiwa ni wa kila mtu akiacha uvivu na uzembe
LikeLike
Ndiyo.
LikeLike
Ni kweli kabisa kocha kuwa wengi tunaona viwango vya elimu vimeshushwa na kuwaona wale walioko shuleni ni wazembe sana kwa kufeli. Kumbe tusilojua ni kuwa viwango vimeshushwa katika maeneo mengi ya maisha yetu. Nakushukuru sana kwa angalizo hili nitajitahidi kujitoa kwenye uzembe nilionao.
LikeLike
Ndiyo, viwango vimeshushwa kila mahali, tusiwe tu wazembe.
LikeLike
Asante kocha nguvu yakuturudisha nyuma nayo imekua
Kubwa kwa hiyo nitauepuka uzembe kama ukoma
LikeLike
Ndiyo
LikeLike
Viwango vimeshushwa sana,mafanikio makubwa Kwa zama hizi yanawezekana Kwa mtu yoyote tuache uzembe ,uvivu na ujinga tuweke kazi kubwa tupate mafanikio
Asante.
LikeLike
Ndiyo
LikeLike
Hakika ni uzembe wa Hali ya juu kutopata mafanikio makubwa kwenye zama hizi,Nitapambana kwa Kila namna nisife nikiwa maskini
LikeLike
Kila la kheri.
LikeLike
Ahsante dana kocha, Kwa jinsi viwango vya mafanikio vimeshushwa sana kwenye kila eneo, ni kujidharau kwa hali ya juu sana kama tutashindwa kuyapata mafanikio makubwa tunayoyataka. Nitapambana hadi mafanikio yawe mikononi mwangu
LikeLike
Kila la kheri
LikeLike
Napambana kutokuwa mzembe
LikeLike
Vizuri
LikeLike
Viwango vimeshushwa sana kufanikiwa kupo rahisi sana
LikeLike
Ndiyo
LikeLike
Viwango vya ufaulu kwa wanafunzi vimeshushwa,
Kwa kifupi karibu ktk kila nyanja za Maisha yetu viwango vimeshushwa.
Hivyo Kama hujafanikiwa ktk eneo lolote la Maisha yako
Kuna sababu moja mbili tu ambazo uvivu ,usembe,
Asante Sana kocha .
LikeLike
Hakika
LikeLike
Asante kocha kwa kutukumbusha hili, nitatumia vizuri fursa zinazonizunguka kufanya makubwa
LikeLike
Vizuri
LikeLike
Asante kocha, nitatumia vizuri fursa zinazonizunguka kufanya makubwa
LikeLike
Ni kweli kabisa! Viwango vya mafanikio vimeshushwa sana!
Ni uzembe tu kutokufanikiwa.
LikeLike
Ndiyo
LikeLike
Viwango vimeshushwa sana na ushindani umekuwa mwepesi mno.
LikeLike
Ndiyo
LikeLike
Asante Kocha, kwa sasa uzembe ndiyo adui wa kufikia mafaniko yetu, kwani viwango vimeshushwa sana kila eneo ambalo mtu anataka kufanikiwa nalo.
LikeLike
Hakika
LikeLike
Viwango vimeshushwa sana kocha.
Nitolee mfano nilipoanza Kazi ya ujenzi, Kila kitu kilikuwa ni kigumu, kwanza kumpata mteja ilikuwa ni Kazi sana. Ili umpate mteja ilikuwa ni lazima ujulikane kwenye kundi kubwa la watu.
Mawasiliano yalikuwa ni lazima uonane na mteja USO Kwa USO.
Nakumbuka nilikuwa natoka nyumbani Hadi site unakuta maji hakuna unarudi nyumbani na hapo uache ujumbe Kwa mdomo kuwa maji yachotwe Ili kesho iendelee na Kazi. Ukirudi kesho yake maji hakuna nabado utarudia Tena na Tena Hadi ufanye Kazi hiyo.
Leo Kila kitu rahisi fundi ukiwa nyumbani unapata Kazi, upapokea pesa , unafanya Kazi za ujenzi ukiwa nyumbani Kwa kuwasilisna Kwa mtandao na mambo yakawa yameisha..
Ni kweli kabisa kutokufanikiwa Kwa kipindi hiki kinachochangia ni uzembe tu.
LikeLike
Asante sana Mcharo, umetoa mfano wenye nguvu kubwa mno, ambao ndiyo uhalisia kabisa. Tujikumbushe sana haya, ili tunaposhindwa kupata mafanikio, tujue ni uzembe wetu wenyewe.
LikeLike
Nimeipenda na kurudi kusoma tena na tena
LikeLike
Vizuri, chukua hatua.
LikeLike
NIKWELI KUTOFANIKIWA KWENYE ZAMA HIZI SABABU KUBWA NI UZEMBE
LikeLike
Ndiyo
LikeLike
Sitaki kuwa mzembe lazima niweke kazi kulingana na Viwango nilivyojiwekea
LikeLike
Kila la kheri.
LikeLike