3134; Maswali mawili yatakayokuwezesha kuuza zaidi.
Rafiki yangu mpendwa,
Leo napenda nikupe taarifa ambazo zitakushtua kidogo.
Taarifa hizo zitakushtua kwa sababu ni tofauti kabisa na matarajio uliyonayo.
Kwenye biashara yako una wateja ambao tayari wananunua kwako mara kwa mara.
Lakini je unajua ni kwa kiasi gani wateja hao wanajua vitu vyote unavyoweza kuwauzia?
Unaweza kudhani wateja wako wanajua vitu vyote unavyouza, kwa sababu ulishawaambia.
Lakini huo siyo ukweli.
Wateja wanajua asilimia 20 tu ya vitu vyote ambavyo unauza.
Yaani kama unauza vitu 10, mteja wako anajua vitu viwili tu, vingine nane hajui kama unauza.
Unaweza kukataa hilo na kusema wateja wako wanajua vyote unavyouza kwa sababu umeshawaambia.
Lakini ukweli ni kwamba kwa sababu umewaambia wateja yote unayouza haimaanishi wanakumbuka.
Ni rahisi wewe kukumbuka vitu vyote unavyouza, kwa sababu ndiyo unavifikiria kwa muda mrefu.
Wateja wako wana mambo yao wanayoyafikiria kwa muda mrefu, ila biashara yako siyo moja kati ya hayo.
Kama bado inakuwa vigumu kwako kukubali hilo hebu jiulize ni mara ngapi umekutana na wateja wako wakiwa wananunua mahali pengine vitu ambavyo hata wewe unauza?
Na unapowauliza mbona hawanunui kwako wanakujibuje? Wengi watakuambia hawakujua kama pia unauza vitu hivyo.
Unaweza hata kuwaambia kwamba ulishawaambia, lakini bado haifasaidia.
Rafiki, sisi binadamu huwa tunaendesha maisha yetu kwa mazoea. Karibu nusu ya mambo tunayofanya kwenye siku yetu ni kwa mazoea, tunafanya kama ambavyo tumekuwa tunafanya.
Hivyo wateja wako pia tayari wanayo mazoea wanayoyatumia kwenye kufanya maamuzi ya manunuzi.
Tayari wameshazoea vitu gani wananunua kwako na vitu gani wananunua kwa wengine.
Kadhalika na wewe pia umekuwa unauza kwa mazoea.
Tayari unajua wateja wako wakija kwako wananunua vitu gani.
Unaweza kudhani ni vile tu wanavyonunua mara kwa mara ndiyo pekee wanavyohitaji.
Lakini kama ambavyo tayari tumeshaona, wateja wananunua zaidi, ila tu hawanunui kutoka kwetu.
Ili kuweza kuvuka hilo la wateja kututenga na sisi kuwatenga, tunatakiwa kuvunja hayo mazoea ambayo tayari yameshajengeka kati yetu na wateja.
Mazoea hayo yanavunjwa na maswali mawili ambayo unapaswa kuwauliza wateja wako wote mara kwa mara ili wajue vitu zaidi unavyouza na siyo vile tu walivyozoea wao.
Swali la kwanza ni; Hivi unajua …. ?
Hili ni swali ambalo unawauliza wateja wako kama wanajua kuhusu bidhaa au huduma nyingine unazouza, lakini hawajawahi kununua kwako.
Kwa mfano unaweza kumuuliza mteja; Hivi unajua pia tunauza … ambayo itakufaa sana kwa mahitaji/matumizi yako?
Hapo unachagua bidhaa au huduma ambazo unazo ila mteja hajawahi kununua kisha kumuuliza.
Unapaswa kuuliza swali hili mara kwa mara kwa wateja wako wote, hata kama ulishawaambia.
Kwa sababu kama hawajawahi kununua, jibu la kwanza ni kwamba hawajui kama unauza, hivyo vuka hilo kwa kuwaambia na kuwauliza mara kwa mara.
Swali la pili ni; Ni vitu gani vingine unavyonunua kwa wafanyabiashara wengine ila hupati huduma nzuri kama kwetu?
Swali hili linamtaka mtu akueleze vitu ambavyo tayari ananunua kwa wafanyabiashara wengine, ambavyo haridhishwi navyo.
Kwa majibu anayokupa, unaweza kuona kama ni vitu ambavyo tayari unauza na hivyo kuweza kumuuzia moja kwa moja.
Na kama ni vitu ambavyo huuzi, unaweza kumuunganisha mteja wako na wafanyabiashara ambao watawahudumia vizuri.
Yaulize maswali haya mara kwa mara kwa wateja wako wote kila wanapofanya manunuzi kwako au unapokutana au kuwasiliana nao.
Usidhani kwamba wanajua yote unayouza.
Na hata kama wanajua, usidhani wanakumbuka mara zote.
Kama hawajawahi kununua kwako au ni muda mrefu hawajanunua, jua kwamba hawajui au hawakumbuki.
Uliza maswali hayo ili kuwafahamisha na kuwakumbusha.
Kwa takwimu zinazotokana na kanuni ya wastani, kwa wateja watano unaowauliza maswali hayo, angalau mmoja atafanya manunuzi ya ziada kwako. Hiyo ni asilimia 20, namba ambayo ni kubwa kwenye mauzo.
Hivyo maswali hayo mawili yana nguvu kubwa ya kuongeza mauzo yako kwa uhakika.
Yaulize maswali hayo kwa wateja wako wote na mara kwa mara.
Hata kama ni kwa kurudia rudia kwa kila mteja, fanya hivyo kwa sababu kama hajanunua, hajui au hakumbuki.
Na kama utamuuliza mteja na akakuambia tayari anajua, hakuna ulichopoteza. Utamwambia unapenda kuhakikisha wateja wako wanapata manufaa zaidi kwenye biashara yako.
Na hapo pia unaweza kukamilisha mauzo moja kwa moja.
Kwa kumwambia vizuri sana kwa kujua, leo unachukua ngapi?
Halafu unakaa kimya na kumwacha aongee.
Kama amejivunia kwako kwamba tayari anajua, ataona ana wajibu wa kununua kama anao uhitaji.
Uliza maswali haya kila mara na hakikisha timu yako ya mauzo inafanya hivyo pia ili kuweza kufanya mauzo makubwa zaidi kwa wateja ambao tayari wapo kwenye biashara yako.
#NidhamuUadilifuKujituma
#AfyaUtajiriHekima
#KaziUpendoHuduma
#UpekeeUdadisiUbunifu
#UshirikianoUtegemeanoUwajibikaji
#BilioneaMafunzoni
#NajengaBiashara
#HakunaKingineMuhimu
#LazimaNitoboe
#NawekaKaziNifanikiwe
Safi sana Kocha Dr Makirita Amani, ni maswali mazuri ya kusaidia kuongea mauzo kwenye biashara.
Hivi unajua?
Swali la pili ni; Ni vitu gani vingine unavyonunua kwa wafanyabiashara wengine ila hupati huduma nzuri kama kwetu?
LikeLike
Tutatumie kwa manufaa.
LikeLike
Upo sahihi kocha nakubaliana nawewe wateja wengi wanajua vitu vichache sana kuliko tuvyoviuza ntafanyia kazi kwa wakati wote ili biashara yangu kuongeza ufanisi zaidi
LikeLike
Kila la kheri.
LikeLike
Hivi unajua ……..?
Ni huduma gani unapata kwa watoa huduma wengine ambazo hupati hapa kwetu?
LikeLike
Tukae humo.
LikeLike
Asante kocha,Nitajitahidi kuuliza haya maswali mawili kwa wateja na kuifundisha timu yangu ili niweze kukuza mauzo, 1.Hivi unajua…..?
2.Ni vitu gani vingine unavyonunua kwa wafanyabiashara wengine ila hupati huduma nzuri kama kwetu?
LikeLike
Kila la kheri
LikeLike
Sawa kabisa kocha. Wateja ni watu wa kuwakumbusha mara Kwa mara. Nakumbuka Kuna kipindi nilikuwa nikijenga nyumba Ile tu namaliza mteja anamleta fundi wa kupaua. Na nilipomwuliza mbona umeleta fundi mwingine alinijibu sikujua wewe pia unaezeka. Lakini nakumbuka mwanzoni nilimwambia.
Hilo lilinifanya kuwa makini sana na wateja Hivyo nikawa na tabia ya kuwapigia stori ya upauaji huku tukijenga boma .kabla ya boma kuisha namwambia kinachofuata hapa ni sisi kukupaulia jengo lako .tunaamini hutatunyima Kazi hii na hili limesaidia sana.
LikeLike
Asante kwa mfano huu mzuri.
Ni muhimu sana tuendelee kuwakumbusha, maana wana mambo mengi.
LikeLike
Nina wajibu wa kuwauliza na kuwakumbusha wateja kuhusu bidhaa nyingi ambazo ninauza.Kupitia hilo nitaweza kufanya mauzo ya ziada ama rufaa na mwisho wa siku kuongeza mauzo
LikeLike
Fanya hivyo.
LikeLike
Nahakikiksha nauliza maswali haya mawili kwa kila mteja nitakaekutanan nae au kuzungumza nae kwani si kila mteja anakumbuka bidhaa zote ninazouza na kwakufanya hivi itanisaidia kuongeza mauzo kwenye biashara yangu.
Asante kocha kwa somo hili
LikeLike
Vizuri, fanya hivyo.
LikeLike
Ahsante kocha.
Swali la kwanza lina Nguvu zaidi. Unaweza ukaweka vitu nje na bado wateja wasione Ila unapouza na wao wakajibu. Unakuwa umewashirikisha na waowameshiriki.
LikeLike
Ni kweli kabisa, tusikae kimya kwa kudhani wanaona, tuwakumbushe mara kwa mara.
LikeLike
Asante sana kocha,nitayafanyia kazi maswali haya ili kuweza kuyatumia ktk mauzo yangu.
LikeLike
Kila la kheri.
LikeLike
Asante sana kocha
Nitayatumia maswali hayo mawili ili Wateja wanunue zaidi ya Kile walichozoea kununua.
LikeLike
Vizuri sana.
LikeLike
Kuna maswali mawili ya kumuuliza mteja ili aweze kujuwa unachouza.
1. Jee unajua?
2. Ni vitu gani vyengine unavyonunua kwa watu wengine.
LikeLike
Muhimu sana.
LikeLike
Ni vyema kuwa tunauliza haya maswali ili kuongeza kukumbukaa na pia kujulikana kile tunachouza hivi unajua nauzaga vyoo vizuri sana ambavyo vinakufaa kwa nyumba yako?
LikeLike
Muhimu sana tuulize kwa msimamo.
LikeLike
Ni rahisi kwa mwenye biashara kukumbuka vitu vyote unavyouza ila sio kwa mteja.
LikeLike
Ndiyo.
LikeLike
Ni kweli wateja wengi hawana taarifa za kutosha kuhusu kile tunachouza, nitayatumia maswali haya mimi na timu yangu ili kuweza kuongeza mauzo na kufanya mauzo ya ziada. Asante sana
LikeLike
Hakika
LikeLike
Hivi unajua ?
Ni vitu gani vyengine unanunua lakini hupati huduma nzuri kama kwetu?
LikeLike
Maswali muhimu m
LikeLike
Maswali mazuri sana haya katika kuongeza mauzo na kuwakumbusha wateja juu ya bidhaa tunazouza. Asante sana kocha
LikeLike
Tuwakumbushe mara kwa mara.
LikeLike
Haya ni maswali ambayo napaswa kuwauliza wateja wangu mara kwa mara,na pale ntakapoyatumia vizuri yanakuwa na matokeo makubwa upande wa mauzo;
1- Hivi unajua …. ?
2- Ni vitu gani vingine unavyonunua kwa wafanyabiashara wengine ila hupati huduma nzuri kama kwetu?
3-mwisho ni kukamilisha mauzo
Kwa kumwambia vizuri sana kwa kujua, leo unachukua ngapi?
LikeLike
Tuzingatie.
LikeLike
Maswali muhimu ambayo napaswa kuwauliza wateja wangu mara kwa mara.
1. Hivi unajua?
2. Ni vitu gani vingine unavyonunua kwa wafanyabiashara wengine ila hupati huduma nzuri kama kwetu?
LikeLike
Tuyaulize.
LikeLike
1.hivi unajua…..?
2.Vitu gani unanunua Kwa wafanyabiashara wengine ambavyo hupati huduma nzuri kama unavyopata kwetu
Asante sana nitatumia maswali haya kwenye biashara yangu ili nipate matokeo mazuri zaidi
Asante
LikeLike
Vizuri, yatumie kwa uhakika.
LikeLike
Ni kweli wateja wanajuwa vitu vichache Kati Ya tunavyouza
LikeLike
Ndiyo
LikeLike
Ahsante sana kocha nitayatumia maswali hayo mawili kwa wateja wangu
LikeLike
Kila la kheri.
LikeLike
MISINGI YETU
NidhamuUadilifuKujituma
#AfyaUtajiriHekima
#KaziUpendoHuduma
#UpekeeUdadisiUbunifu
#UshirikianoUtegemeanoUwajibikaji
#BilioneaMafunzoni
#NajengaBiashara
#HakunaKingineMuhimu
#LazimaNitoboe
#NawekaKaziNifanikiwe
LikeLike
Tukae humo.
LikeLike
Muhimu sana.
LikeLike
Asante sana hivi unajua kuwa kwasasa unaweza kupata VIFARANGA Bora Kwa kroila?
LikeLike
Safi sana.
LikeLike
Kweli penda kuhakikisha wateja wako wanapata manufaa zaidi kwenye biashara yako. Na itasaidia Sana kuleta wengine
LikeLike
Hakika
LikeLike