3147; Tumia sababu zote za kushindwa.
Rafiki yangu mpendwa,
Wote tunakumbuka wakati tupo shuleni.
Tulijua kuna mitihani ambayo inakuja.
Pale tulipojiandaa vyema na mitihani hiyo na ikatokea tukafanya vibaya, huwa hatuumii sana, kwa sababu tunajua tumefanya kila kitu.
Lakini pale ambapo hatukujiandaa vyema na ikatokea tumefanya vibaya, huwa tunaumia sana.
Tunajiambia kama tungejiandaa vyema, huenda tungefanya vizuri.
Kwa kifupi tunakuwa na majuto pale ambapo hatujafanya maandalizi mazuri.
Na hivyo ndivyo ilivyo kwenye maisha yetu yote.
Huwa tunatengeneza majuto makubwa kwenye maisha pale tunapokuwa tunajua tunachopaswa kufanya ila hatukifanyi.
Tunapoishia kuwa na maisha ambayo hatuyataki, tunajiambia kama tungechukua hatua, tusingeishia kwenye maisha ya aina hiyo.
Leo nataka ujifunze na uchukue hatua ambayo itafuta kabisa majuto kwenye maisha yako.
Na hilo linahusisha hatua kadhaa za kufanyia kazi.
Kwanza kabisa unaanza na kile hasa unachotaka kupata kwenye maisha yako. Wapi ambapo unataka kufika. Nini ukifikia utayahesabu maisha yako kuwa ya mafanikio?
Pili orodhesha sababu zote zinazoweza kukuzuia kupata hicho unachotaka. Orodhesha kila kitu kinachoweza kukukwamisha.
Tatu ni kuzifanyia kazi hizo sababu za kushindwa. Hapo unachukua hatua kuzishughulikia sababu zote zinazoweza kuwa kikwazo kwako.
Hii ni hatua inayohitaji kazi kubwa sana.
Hupaswi kuacha chochote kinachoweza kukuzuia kupata ushindi na ukaja kukitumia kama sababu.
Baada ya hatua hizo, kinachofuata ni kuwa na subira kwenye kupata matokeo.
Matokeo yanapokuja vizuri, unafurahia kwa juhudi zote ulizoweka.
Na pale matokeo yanapokuja vibaya, huwi na majuto wala sababu, kwa sababu unajua umefanya kila kilichopaswa kufanyika.
Kama umeshindwa siyo kwa uzembe wako, bali kwa mambo yaliyo nje ya uwezo wako.
Timu inayotoka uwanjani ikiwa imeshindwa na kutoa sababu za kushindwa ni timu iliyoingia uwanjani ikijua kabisa inaenda kushindwa.
Kama ingekuwa imejiandaa kwa ushindi kamili, isingekuwa na sababu pale inaposhindwa.
Hivyo ndivyo unavyopaswa kuyaendesha maisha yako ya mafanikio.
Hakikisha pale unaposhindwa unakuwa huna sababu yoyote ya kuelezea kushindwa kwako.
Unakuwa umetumia sababu zote kabisa.
Hilo linakutaka ujitume kupitiliza, zaidi ya wengine wote wanavyojituma.
Halafu kitu kizuri ni kadiri unavyojituma, ndivyo unavyojiweka kwenye nafasi nzuri zaidi ya kupata ushindi kwa uhakika.
Unaweza usiamini hili, lakini wewe mwenyewe umekuwa unajihujumu usishinde.
Unajua kabisa sababu zotakazochangia kushindwa, lakini bado huzifanyii kazi.
Na pale inapotokea umeshindwa, unatumia sababu hizo hizo, ambazo ulizijua tangu mwanzo ila hukufanya chochote.
Unakuwa kama mwanafunzi ambaye hasomi, halafu anapofeli mtihani anajiambia kama angesoma angefaulu.
Kwani nini kilimzuia asisome?
Mwanafunzi kazi yake si kusoma?
Ukiifanya kazi yako vizuri, kwa kutekeleza kila kinachopaswa kutekelezwa, unakuwa umetumia sababu zote za kushindwa.
Unakuwa umejiweka kwenye nafasi kubwa ya kupata ushindi.
Na hata kama hutapata ushindi, hutakuwa na majuto yoyote.
Badala yake utaendelea na kufanya yaliyo sahihi mpaka upate unachotaka.
Ukishindwa hakikisha huna sababu.
Ukishakuwa tu na sababu ya kushindwa, basi jua umejitakia wewe mwenyewe kushindwa.
Unakuwa hujaifanya kazi yako kwa uhakika.
#NidhamuUadilifuKujituma
#AfyaUtajiriHekima
#KaziUpendoHuduma
#UpekeeUdadisiUbunifu
#UshirikianoUtegemeanoUwajibikaji
#BilioneaMafunzoni
#NajengaBiashara
#HakunaKingineMuhimu
#LazimaNitoboe
#NawekaKaziNifanikiwe
Hakuna sababu yeyote muhimu pale unapokuwa umeshindwa. Jambo moja kubwa nikuongeza jitihada zaidi ili kufikia malengo makubwa..
LikeLike
Hakika.
LikeLike
Ukifanya vizuri Kwenye Kazi yako umeondoa sababu zote za kushindwa.
LikeLike
Hakika.
LikeLike
Asante kocha nikishindwa sitakuwa na sababu yoyote badala yake nitachukua hatua ya kufanya kazi kuliko wote sitaruhusu mutu anishinde kufanya kazi
LikeLike
Vizuri
LikeLike
Tuhakikishe tunatumia sababu kushinda na kutumia kufanya kazi kwa bidii hadi itupe ushindi tunaoutaka
LikeLike
Ndiyo.
LikeLike
Ukishindwa hakikisha huna sababu ya kushindwa.
Ukishakuwa tu sababu ya kushindwa basi jua umejitakia mwenyewe kushindwa.
Unakuwa hujaifanya kazi yako kwa uhakika.
LikeLike
Ndiyo.
LikeLike
Wewe.mwenyewe umekuwa unajihujumu usishinde kwani tayari sababu za kushinda na kushindwa zote kwa pamoja unazijua
LikeLike
Hakika
LikeLike
Sababu za kushindwa na kushinda kwangu hadi sasa nazijua muhimu siitaji kuendelea kujihujumu
LikeLike
Vizuri
LikeLike
Ni muivu ,akubwa sana kujua cha kufanya ushinde halaf hufanyi na hushindi, NITAJIKAMATA kila ninaoona sizifati kwa uaminifu njia hatua za unshindi.
LikeLike
Vizuri
LikeLike
Ninafanya kazi yangu vizuri na ninatekeleza kila kinachopaswa kutekelezwa hata kama matokeo yatakuja si mazuri nisiwe na majuto kwani nakuwa nimefanya kile nilichopaswa kufanya.
Asante kocha.
LikeLike
Vizuri
LikeLike
Asante kocha,Ni kweli sababu ninazijua ambazo zinanifanya nishindwe lakini nitaweka kazi mbele bila kukata tamaa ili niweze kufanikiawa.
LikeLike
Kila la kheri.
LikeLike
Ukiifanya kazi yako vizuri, kwa kutekeleza kila kinachopaswa kutekelezwa, unakuwa umetumia sababu zote za kushindwa.
Unakuwa umejiweka kwenye nafasi kubwa ya kupata ushindi.
Na hata kama hutapata ushindi, hutakuwa na majuto yoyote.
LikeLike
Hakika
LikeLike
soma ukijua kuna mtihani mbele hata ikitokea hujutii kama yule ambaye hakusoma kabisa
nitaweka kwenye matendo yote ninayojifunza,
asante kocha.
LikeLike
Kila la kheri.
LikeLike
Iili tufaniikiwe Kwa chochote like tunachotaka tunatakiwa kufanya Yale yote yanayotakiwa kufanywa na matokeo yanapokuja tuyapokee Kwa namna yanavyokuja
Ufanyaji upo ndani ya uwezo wetu Ila matokeo yapo nje ya uwezo wetu
Asante
LikeLike
Kabisa.
LikeLike
Nitafanya kila ninachotakiwa kufanya ili nisije toa sababu baaada ya kushindwa.
LikeLike
Vizuri
LikeLike
Nitajitahidi kila wakati katika majukumu YANGU kufanya maandalizi ili niweze kufanya kwa mafanikio kila jukumu
Langu. Maandalizi hayo yatanifanya nisijute Kama nikupata matokeo mabaya.
Asante Sana kocha
LikeLike
Kila la kheri.
LikeLike
Ukishindwa hakikisha huna sababu.
Ukishakuwa tu na sababu ya kushindwa, basi jua umejitakia wewe mwenyewe kushindwa.
Unakuwa hujaifanya kazi yako kwa uhakika.
Asante sana Kocha Dr Makirita Amani
LikeLike
Hakika
LikeLike
Kufanyia kazi sababu za kushindwa ni maandalizi ya kushinda vita
LikeLike
Ndiyo
LikeLike
Niataweka kazi yangu vizuri kwa kutekeleza ninachopaswa kutekeleza ili nijiweke kwenye nafasi kubwa ya kupata USHINDI.
Na kama sitapata USHINDI sita kuwa na majuto yoyote.
LikeLike
Vizuri
LikeLike
Nahakikisha Sina sababu ya kushindwa, sababu kuu ni kushindwa kukaa kwenye mchakato, nakaa kwenye mchakato kwa asilimia 100 Ili kuondoa sababu hiyo
LikeLike
Vizuri, tekeleza hilo.
LikeLike
Nakwenda kuweka juhudi kubwa kuhakikisha naondoa sababu zote zinazoifanya nishindwe kufikia malengo yangu
LikeLike
Kila la kheri
LikeLike