3151; Tayari tumeshashinda.

Rafiki yangu mpendwa,
Kwenye mchezo wa aina yoyote ile, kushinda au kushindwa huwa kunaanzia nje ya uwanja.
Yaani timu inaingia uwanjani ikiwa tayari ina matokeo.
Kinachokwenda kufanyika uwanjani ni kukamilisha tu mchezo kama ulivyopangwa.
Hiyo haimaanishi kwamba wamependelewa kupewa ushindi, bali inamaanisha hawapo tayari kupokea kingine isipokuwa ushindi.

Lakini pia kuna timu ambazo katika hali yake zinakuwa zimeshapata ushindi mkubwa na hivyo kuwa zinasubiri kukamilisha tu michezo.
Kwa timu kukusanya ushindi mwingi na mkubwa mwanzoni, inapata nafasi ya kupumzika na kusubiri kukabidhiwa ushindi.

Ushindi wetu upo kwenye ukaaji wa kwenye mchakato.
Tunapokaa kwenye mchakato kwa ukamilifu na msimamo bila kuyumba, tunakuwa tumejipa ushindi tayari.
Kinachokuwa kinasubiriwa hapo ni muda kukamilika ili mtu kupata kile anachotaka.

Ni muhimu sana tujijengee mtazamo huu wa ushindi kwa sababu wengi sana wamepotezwa kwa kutaka ushindi wa haraka.
Kila inapotokea mtu ana tamaa ya kupata ushindi wa haraka, huwa anaishia kufanya mambo ambayo baadaye yanamsumbua na kuwa kikwazo kwake.

Lakini mtu ukishajua tayari umeshashinda, hutahangaika na njia za mkato za kupata ushindi, njia ambazo zinaishia kukupoteza zaidi.

Hatutafuti ushindi, bali tumeshaupata.
Kilichobaki ni kusubiri kukabidhiwa ushindi kwenye wakati sahihi.
Ukaaji wa kwenye mchakato ndiyo ushindi kamili ambao unatupa ushindi mwingine wote tunaotaka kweye maisha.

Dhihirisha ushindi wako kwa kukaa kwenye mchakato kwa ukamilifu na msimamo bila kuacha.
Na hapo utakuwa umebaki na swala la muda tu wa kukabidhiwa ushindi wako.

#NidhamuUadilifuKujituma
#AfyaUtajiriHekima
#KaziUpendoHuduma
#UpekeeUdadisiUbunifu
#UshirikianoUtegemeanoUwajibikaji
#BilioneaMafunzoni
#NajengaBiashara
#HakunaKingineMuhimu
#LazimaNitoboe
#NawekaKaziNifanikiwe