3153; Kiburi cha umasikini.
Rafiki yangu mpendwa,
Tofauti kati ya matajiri na masikini imekuwa inaendelea kukua kwa kasi kubwa.
Masikini wamekuwa wanaendelea kuwa masikini zaidi na zaidi, huku matajiri wakiendelea kupata utajiri mkubwa zaidi na zaidi.
Wengi wamekuwa wanatoa sababu zao mbalimbali juu ya tofauti hiyo, lakini zimekuwa ni za juu juu tu.
Sababu halisi na kiini hasa kinachoendekea kuwatofautisha masikini na matajiri ni kiburi cha umasikini.
Masikini wamekuwa na kiburi fulani hivi ambacho kimekuwa hakiwasaidii zaidi tu ya kuwapoteza.
Kwa upande wa pili matajiri wamekuwa na unyenyekevu ambao umekuwa msaada mkubwa sana kwao.
Kwenye kujifunza, masikini wamekuwa na kiburi kwamba tayari wanajua kila kitu na hakuna kipya cha kujifunza.
Wakati matajiri wamekuwa wanyenyekevu kwenye kujifunza, hata kama ni kitu wanachorudia kujifunza.
Kwenye kuanzisha na kujenga biashara masikini wamekuwa na kiburi kwamba wanaweza kuendesha biashara zaidi ya moja kwa wakati mmoja, kitu kinachowasumbua sana.
Wakati matajiri wamekuwa wanyenyekevu wa kujenga biashara moja kwa wakati mpaka ifikie mafanikio ndiyo wanaingia kwenye nyingine.
Kwenye ukaaji wa kwenye mchakato masikini wamekuwa na kiburi kwamba hawahitaji mchakato wowote, badala yake wanafanya kwa hisia, pale wanapojisikia.
Wakati matajiri wamekuwa na unyenyekevu wa kuheshimu mchakato na kuufuata kwa msimamo bila kuacha.
Kwenye mafanikio ya wengine masikini huwa na kiburi cha kuona waliowazidi mafanikio wana bahati au walisaidiwa kufika walipofika hivyo hawahangaiki kujifunza chochote kwao.
Wakati matajiri wamekuwa na unyenyekevu wa kuona waliowazidi mafanikio kuna kitu wanakijua ambacho wao hawajui, hivyo huwa tayari kujifunza kwao na kuchukua hatua za tofauti, kitu kinachowapa matokeo ya tofauti.
Kwenye kuweka akiba na kufanya uwekezaji endelevu masikini wamekuwa na kiburi kwamba hawawezi kujitesa hivyo wanatumia kipato chao chote na cha ziada, wakiamini wataanza kuweka akiba na kuwekeza pale kipato chao kitakapokuwa kikubwa.
Wakati matajiri wanakuwa na unyenyekevu wa kuanza kuweka akiba na kuwekeza hata kipato kinapokuwa kidogo sana na wanaendelea kukuza tabia hiyo kadiri kipato kinavyoongezeka.
Kwenye kushirikiana na wengine masikini wana kiburi kwamba wao ni jeshi la mtu mmoja hivyo wanaweza kufanya kila kitu peke yao, kitu kinachowachosha sana na kuwapunguzia uzalishaji na ufanisi.
Wakati matajiri wana unyenyekevu wa kujua hawawezi kufanya kila kitu peke yao, badala yake wanahitaji ushirikiano wa watu wengine, kitu kinachowapa matokeo mazuri.
Kwenye kugatua majukumu yao masikini wamekuwa na kiburi kwamba hakuna mtu yeyote anayeweza kufanya kile wanachofanya wao kwa ubora wanaofanya, hivyo huendelea kufanya wenyewe na kufurahi pale wanapotegemewa kwenye kitu hicho.
Wakati matajiri wamekuwa na unyenyekevu kwamba wapo wengine wengi wanaoweza kufanya kile wanachofanya vizuri tu na kuwatafuta kisha kuwapa majukumu nayo na hivyo kuweza kukua zaidi.
Kwenye kukimbizana na fursa mpya kila wakati, masikini wamekuwa na kiburi kwamba wanaweza kuzitambua na kuzifanyia kazi fursa zote mpya wanazokutana nazo na hilo limekuwa linachukua muda wao mwingi.
Wakati matajiri wana unyenyekevu wa kujua kwamba fursa kuu kwao ipo kwenye kile wanachofanya na hivyo hawahangaiki na fursa mpya zinazojitokeza kila wakati.
Masikini wamekuwa na kiburi cha kuamini kuna siri ya mafanikio ambayo imefichwa na matajiri na wamekuwa wakitumia muda wao mwingi kutafuta njia ya mkato ya kufanikiwa bila kuweka kazi, mwishowe wamekuwa wakitapeliwa na kupoteza fedha na muda.
Matajiri wamekuwa na unyenyekevu wa kuamini siri kuu ya mafanikio ni kuweka kazi na hakuna njia ya mkato ya kufanikiwa, wanaweka kazi kubwa kwa muda mrefu na wanayaona mafanikio.
Tofauti hizo zinaweza kuonekana ni ndogo sana kwa tukio la mara moja.
Lakini zinavyokwenda hivyo kwa muda mrefu, mfano kwa miaka 10, ndiyo unawapata watu wawili ambao wanatofautiana sana, hata kama walianzia mahali wanapolingana.
Ni kiburi kipi cha umasikini ambacho ulikuwa nacho kwa muda mrefu kabla ya kukubali kukaa kwenye huu mchakato wa Bilionea Mafunzoni kwa uhakika na msimamo?
Karibu ushirikishe kwenye maoni hapo chini.
Amua leo kuvunja kila aina ya kiburi cha umasikini.
Achana kabisa na mtazamo wa masikini jeuri.
Kuwa mnyenyekevu na utaziona fursa nyingi za kujifunza na kuchukua hatua ili kufanya makubwa zaidi.
#NidhamuUadilifuKujituma
#AfyaUtajiriHekima
#KaziUpendoHuduma
#UpekeeUdadisiUbunifu
#UshirikianoUtegemeanoUwajibikaji
#BilioneaMafunzoni
#NajengaBiashara
#HakunaKingineMuhimu
#LazimaNitoboe
#NawekaKaziNifanikiwe
Asante sana Kocha, kiburi hakilipi. Mara zote nitakuwa kam matajiri.
Nipo tayari kujifunza.
Nafanya KAZI biashara Moja mpaka niifikishe kwenye viwango vikubwa.
Naweka akiba na kuwekeza Kwa msimamo, Kila siku (UTT na DSE)
Sikimbizani na fursa nyingine Sasa. Ninakuwa mtu wa mchakato na anayeaminika kuwa akisema anafanya jambo Fulani, lazima alifanye
LikeLike
Vizuri, kila la kheri kwenye utekelezaji.
LikeLike
Kwenye kuweka akiba na kufanya uwekezaji endelevu.
Ni kweli maskini wengi wanasumbuliwa na kiburi na ujuaji.
LikeLike
Kabisa, wanajua sana, halafu hawana matokeo.
LikeLike
Ni kweli Mimi nilikuwa muhanga wa kuona fursa nyingi na kwenda kuzifanyia kazi Ila nimeendelea kujifunza na nimeona umuhimu wa kuweka nguvu mahali pamoja kinaleta mafanikio makubwa
Asante Kocha
LikeLike
Vizuri sana kwa kutambua hilo. Sasa fanyia kazi kwa uhakika.
LikeLike
Hizi ni tofauti ndogo lakini matokeo yake ni makubwa sana nikweli kujifunza na kufanya ndio matajiri wanafanya
LikeLike
Kila la kheri
LikeLike
Viburi 2 nilikuwanavyo
1)Kuamini kupata ni majaaliwa
2)Kutokuzungukwa na watu waliofanikiwa
LikeLike
Vizuri kwa kujua ulipokwama. Sasa nenda kwa usahihi ili kupiga hatua kubwa zaidi.
LikeLike
Kaa upande wangu mimi nilikua na kiburi cha kuamini kuwa kufanya vingi ndiyo mafanikio kumbe ni kiburi cha umaskini hicho nimeacha na sasa nachimba shimo moja tu basi na pia nilikua na kiburi cha kutokujifunza kwa wale waliofanikiwa nikiwa na maana ntaweza bila kuwafuata wao kumbe ni kiburi cha umaskini na sasa natawafuata wale walionitangululia na kushauriana nao ili kupata fursa toka kwao nitaachana na kiburi cha kimaskini kuanzia leo
LikeLike
Vizuri kwa kujua hayo, sasa kaa kwenye njia sahihi.
LikeLike
kiburi cja umasikini ni uninga unaosumbua na kukufanya mtu uendelee kuwa masikini.
kauli ya kama imepangwa imepangwa huwezi badilisha.Nakataa kiburi cja umasikini
LikeLike
Hakika.
LikeLike
Mimi nilikuwa na kiburi cha kukimbizana na kila fursa nzuri ی inayojitokeza. Ila sasa nimegundua kuwa hizi fursa zilizonyingi zimejaa utapeli. Nimeachana nazo
LikeLike
Vizuri, usirudi tena nyuma.
LikeLike
Ni iburivcha akiba na uwekezaji
Na nimeweza kitubu tatizo Hilo
Asante sana
LikeLike
Vizuri, usirudi nyuma.
LikeLike
Nilikuwa na kiburi cha kutaka kufanya biashara zaidi ya moja kwa wakati mmoja.
Sikuona umuhimu wa kuwekeza na kuweka akiba.
LikeLike
Vizuri kwa kujua hayo, achana nayo kabisa.
LikeLike
kuamini wengine kuwa wanaweza kufanya zaidi yng ili nifanye yaliyo muhimu zaidi
ili kukuza biashara,sasa nitaamini waendelee kufanya bila uwepo wng.
asante kocha.
LikeLike
Vizuri sana, imarisha hilo.
LikeLike
Nilikuwa na vibuli vitatu vya kimasikini.
1-Kuamini naweza kuendesha biashara zaidi ya moja kwa wakati mmoja.
2-kukimbizana na fursa mpya ninazokutana nazo.
3-Kuamini nitaanza kuweka akiba na kuwekeza pale kipato changu kitakapokuwa kikubwa.
LikeLike
Vizuri kwa kujua hayo, achana nayo mara moja.
LikeLike
Naachana na kiburi cha kutokaa kwenye mchakato wa utajiri.
LikeLike
Vizuri
LikeLike
Naachana kabisa na mtazamo wa masikini jeuri, Nakuwa mnyenyekevu katika kujifunza na kuchukua hatua .
LikeLike
Kila la kheri.
LikeLike
Kiburi Cha umasikini nilichokuwa nacho ni kuaminika kwamba nitafanikiwa Sana katika biashara yangu.
Sikuwa najua kwamba Ili nifanikiwe napaswa kutimiza baadhi ya matakwa ya ili mtu ufanikiwe ni lazima uyatimize . Matakwa hayo ni pamoja na kujifunza endelevu , pia kuyaweka ktk vitendo mafunzo hayo.
Pia nilikua sitambui kwamba kupata mafanikio Kuna mchakato wa kufuata , nilazima ufuate mchakato kwa msimamo.
LikeLike
Vizuri kwa kujua hilo, usirudi tena nyuma.
LikeLike
Maskini wana kiburi na Matajiri Ni Wanyenyekevu.
KIBURI Cha Umasikini nilichokuwa nacho kwa muda mrefu Ni ukaaji wa kwenye mchakato kwamba sihitaji mchakato wowote, badala yake nafanya kwa hisia, yaani pale ninapojisikia.
Lakini Sasa nimekuwa mnyenyekevu na kuheshimu mchakato na kuufuata kwa msimamo bila kuacha
LikeLike
Vizuri kwa kujua hilo, usirudi tena nyuma.
LikeLike
Kiburi changu cha umaskini ni kutokugatua majukumu. Sasa katika shughuli zangu majukumu ambayo yanaweza kufanywa na wengine ninayakabidhi kwao. Muda ninaookoa hapa ninauelekeza kwenye majukumu yanahitaji zaidi umakini wangu.
LikeLike
Vizuri, tekeleza hilo.
LikeLike