Barua ya XVII; Kuhusu Falsafa Na Utajiri.
Rafiki yangu Mstoa,
Watu wengi wamekuwa wanachukulia falsafa na utajiri kama vitu ambavyo haviwezi kwenda pamoja.
Kama ambavyo wengi wanavyochukulia imani na utajiri haviwezi kwenda pamoja.
Hivyo wale wanaochagua falsafa wanaamua kuachana kabisa na mambo ya utajiri.
Huku wale wanaohangaika na utajiri wakipuuza kabisa falsafa.
Lakini falsafa ya Ustoa ni tofauti kabisa na falsafa nyingine.
Hii siyo falsafa ya nadharia na mijadala.
Bali ni falsafa ya vitendo, yenye hatua za kuchukua ili mtu kuwa na maisha bora.
Hivyo mahusiano ya falsafa ya Ustoa na utajiri siyo ya kuupuuza kabisa, bali kuhakikisha mtu huwi mtumwa wa utajiri.
Mtu unaweza kujenga utajiri unaoutaka, lakini siyo kwa tamaa au kuutegemea. Bali kama sehemu ya kuishi maisha yako kwa ukamilifu.
Kwenye barua yake ya 17 kwa rafiki yake Lucilius, mwanafalsafa Seneca alishirikisha mambo ya kuzingatia kuhusu falsafa na utajiri.
Hapa tunakwenda kujifunza mambo hayo na hatua za kuchukua ili kujenga maisha bora kabisa kwetu na kwa wengine pia.
1. Falsafa ni muhimu kwenye maisha ya kila siku.
Seneca anaanza kwa kueleza jinsi ambavyo watu wengi wanachukulia falsafa kama kitu cha ziada.
Wanaona ni kitu ambacho wataanza kujihusisha nacho baada ya kuwa wameshayajenga maisha yao.
Lakini hilo siyo sahihi, falsafa siyo kitu cha ziada kwenye maisha, bali ndiyo nguzo ya maisha yenyewe.
Seneca anasisitiza kwamba falsafa ni muhimu sana kwenye maisha ya kila siku.
Kwani ni falsafa ndiyo yenye majibu sahihi kwa kila tunachokuwa tunapitia kwenye maisha.
Hatua ya kuchukua;
Usiahirishe kuwa mwanafalsafa mpaka pale unapokuwa umeyajenga maisha unayoyataka. Bali tumia falsafa kama nguvu ya kujenga maisha unayoyataka. Anza kuishi kwa misingi ya falsafa sasa.
Nukuu;
“You do indeed grasp the all-important thing, the great benefit which philosophy confers, but you do not yet discern accurately its various functions, nor do you yet know how great is the help we receive from philosophy in everything, everywhere,” – Seneca
“Unaonekana kuelewa umuhimu wa falsafa, lakini hujaelewa kwa usahihi jinsi ilivyo na msaada mkubwa kwenye kila kitu na kila mahali.” – Seneca
2. Umasikini siyo kikwazo.
Seneca anaendelea kueleza kwamba sababu ambayo wengi wamekuwa wanatumia kuahirisha kuishi kwa misingi ya falsafa ni kuona kwanza wanatakiwa kupambana na umasikini.
Kwamba waondokane na umasikini kwanza ili wawe huru kuishi kwa misingi ya falsafa.
Lakini Seneca anatahadharisha kwamba hakuna kitu ambacho kinawafunga wengi na kuwa kikwazo kwao kama utajiri.
Anaonyesha kwamba mtu akishajenga utajiri anajikuta akiwa mtumwa wa kulinda utajiri huo ili usipotee.
Hivyo uhuru ambao mtu alidhani ataupata akishakuwa na utajiri, haupati.
Utajiri umekuwa unakuja na uwajibikaji mkubwa ambao unavuruga kabisa matumaini ambayo mtu alikuwa nayo.
Hivyo badala ya kusubiri mpaka uwe tajiri ndiyo uishi kwa misingi ya falsafa, anza kuishi kwa misingi hiyo na hata utakapojenga utajiri, utakuwa huru zaidi.
Hatua ya kuchukua;
Usisubiri mpaka uwe tajiri ndiyo uanze kuishi kwa misingi ya falsafa. Bali anza kuishi misingi ya falsafa mapema ili kila hatua unayopiga ikuweke huru zaidi kuliko kuzidi kukufanya mtumwa kama inavyotokea kwa wengi.
Nukuu;
“Riches have shut off many a man from the attainment of wisdom; poverty is unburdened and free from care.” – Seneca
“Utajiri umekuwa kikwazo kwa wengi kupata hekima; umasikini siyo kikwazo na unamfanya mtu kuwa huru kwa sababu hakuna anachojali.” – Seneca
3. Igiza umasikini.
Kama ambavyo tumeona hapo juu, nia ya wengi ya kujenga kwanza utajiri ili wawe huru imekuwa haitimii. Kwani wanapopata utajiri, ndiyo wanazidi kuwa watumwa kwenye kulinda utajiri huo ili usipotee.
Na hapo ndipo Seneca anapotuma ushauri muhimu wa jinsi ya kulikabili hilo.
Anasema ili mtu kupata utulivu wa kiakili, ana machaguo mawili; kuwa masikini au kuigiza umasikini.
Sisi chaguo la kuwa masikini tunaachana nalo na tunaenda kwenye chaguo la kuigiza umasikini.
Kwenye chaguo hilo tunakuwa tayari kupoteza kila kitu bila ya kuruhusu hilo lituvuruge.
Na ili kuonyesha kwamba tunaweza hilo, tunachagua kuishi maisha ambayo hatuna utegemezi mkubwa kwenye utajiri wowote ambao tumeujenga.
Yaani licha ya utajiri mkubwa tunaopambana kuujenga, maisha yetu yanaendelea kuwa ya kawaida, rahisi na yanayoegemea kwenye mahitaji machache ya msingi.
Hatutengenezi utajiri mkubwa kwa tamaa, bali kwa sababu ya uwezo mkubwa ulio ndani yetu ambao tumeamua kuutumia.
Hatua ya kuchukua;
Jenga utajiri mkubwa kadiri ya uwezo wako, lakini chagua kuishi kama masikini ili uendelee kuwa huru. Usikubali utajiri unaoujenga ukufanye kuwa mtumwa wa kuulinda usipotee. Utachukua hatua za kulinda utajiri wako, lakini hata kama utaupoteza, hutatetereka kwa chochote kile.
Nukuu;
“If you wish to have leisure for your mind, either be a poor man, or resemble a poor man. Study cannot be helpful unless you take pains to live simply; and living simply is voluntary poverty.” – Seneca
“Kama unataka kuwa na utulivu wa kiakili, chagua kuwa masikini au kuiga umasikini. Kujifunza hakuwezi kumsaidia mtu ambaye hawezi kuishi kirahisi na kuishi kirahisi ni kuwa masikini kwa hiari.” – Seneca
4. Ukianza na falsafa, mengine yatakaa sawa.
Seneca anaendelea kurudia kwamba bado watu wanazuiwa kuishi falsafa pale wanapoona bado hawajaweza kujitosheleza kimaisha.
Wengi huona wanaweza kuahirisha kwanza falsafa mpaka pale watakapojitosheleza kimaisha.
Lakini Seneca anauliza, utajuaje umejitosheleza kama huna falsafa?
Anasisitiza falsafa ndiyo kitu cha kuanza nacho kwani ndiyo itatuongoza kwenye nini kinachotutosheleza.
Usipokuwa na kipimo sahihi, ambacho unakipata kwa falsafa, hutafikia utoshelevu, hata upate utajiri mkubwa kiasi gani.
Na pia kuhusu wasiwasi kwamba mtu anaweza kukosa mahitaji ya msingi ya maisha, Seneca anakataa kwamba hilo haliwezi kutokea.
Kwa sababu mahitaji ya msingi ya maisha ni machache na yapo ndani ya uwezo wa kila mtu.
Hatua ya kuchukua;
Bila kujali una nini au umekosa nini, anza kuishi kwa misingi ya falsafa. Hiyo ndiyo itakayokuongoza kwa usahihi kwenye yote unayoyafanya.
Hapo ulipo sasa tayari unajitosheleza kuweza kuishi kwa misingi ya falsafa ya Ustoa. Na hiyo itakusaidia kuwa na maisha bora zaidi.
Nukuu;
“Nay, your plan should be this: be a philosopher now, whether you have anything or not, – for if you have anything, how do you know that you have not too much already? – but if you have nothing, seek understanding first, before anything else.” – Seneca
“Mpango wako unapaswa kuwa hivi; kuwa mwanafalsafa sasa, iwe una kitu au huna, – kwa sababu kama una kitu, unajuaje kama tayari hakijakutosheleza? – na kama huna kitu, anza na ufahamu kwanza kabla ya kingine chochote.” – Seneca
5. Tatizo siyo utajiri au umasikini, tatizo ni akili.
Seneca anamnukuu Epicurus ambaye amewahi kusema; kwa walio wengi, kupata utajiri hakujawa mwisho wa matatizo yao, bali kumekuwa ni kubadilika kwa matatizo.
Seneca anasema hilo halishangazi, kwa sababu kile kinachofanya umasikini uwe mzigo kwetu, ndiyo hicho hicho kinachofanya utajiri nao kuwa mzigo kwetu.
Anatumia mfano wa mtu mgonjwa, iwe atalazwa kwenye kitanda cha mbao au cha dhahabu, haitabadili hali ya ugonjwa wake, kwa sababu upo ndani ya mwili wake.
Maana yake ni kwamba matatizo mengi ya watu yapo kwenye fikra zao. Hivyo kubadili hali yao kutoka umasikini kwenda utajiri haibadili tatizo kuu ambalo lipo ndani yao, badala yake inazidi kulikuza.
Hivyo ili kuwa na maisha bora na tulivu, tuanze kwa kutibu akili zetu kwanza kabla ya mengine yote.
Na tunaijua tiba ya akili ni falsafa pekee.
Hatua ya kuchukua;
Kabla hujahangaika na utajiri au umasikini, anza kuhangaika na akili yako kwanza. Ifanye akili yako kuwa huru kwanza na ndiyo utaweza kuwa huru iwe una umasikini au utajiri.
Kama akili yako haipo huru ukiwa masikini, jua pia haitakuwa huru ukiwa tajiri.
Ishi kwa misingi ya falsafa ya Ustoa kuifanya akili yako kuwa huru wakati wote.
Nukuu;
“For the fault is not in the wealth, but in the mind itself. That which had made poverty a burden to us, has made riches also a burden.” – Seneca
“Tatizo halipo kwenye utajiri bali kwenye akili yenyewe. Kwa sababu kinachofanya umasikini kuwa mzigo kwetu ndiyo hicho hicho kinafanya utajiri nao kuwa mzigo kwetu.” – Seneca
Rafiki yangu Mstoa, kupitia barua hii tumejifunza siyo tu kwamba falsafa haipingani na utajiri, bali utajiri unahitaji sana falsafa.
Kama utaanza na harakati za kukimbizana na utajiri kabla hujajenga misingi ya falsafa, utazidi kupotea.
Kwani kile unachokikimbia kwenye umasikini, ndiyo hicho hicho utaenda kukutana nacho kwenye utajiri.
Tumeshaona kwa wengi ambao wamehangaika na utajiri bila ya misingi sahihi walivyoishia pabaya.
Sisi tusirudie makosa yao, twende kwa usahihi, tuishi kwa misingi ya falsafa ya Ustoa na hiyo ndiyo ituongoze kwenye kila kitu.
Kwa njia hiyo tutaweza kuwa na maisha bora yenye mafanikio makubwa.
Kutoka kwa Mstoa mwenzako,
Kocha Dr Makirita Amani.
Hivyo ili kuwa na maisha bora na tulivu, tuanze kwa kutibu akili zetu kwanza kabla ya mengine yote.
Na tunaijua tiba ya akili ni falsafa pekee.
LikeLike
Ndiyo
LikeLike
Asante kocha nimejifunza kwamba tiba ya akili ni falsafa kwa hiyo tuanze kutibu akili ndiyo tuangaike na mengine
LikeLike
Kabisa.
LikeLike
Tatizo halipo kwenye utajiri bali kwenye akili yenyewe. Kwa sababu kinachofanya umasikini kuwa mzigo kwetu ndiyo hicho hicho kinafanya utajiri nao kuwa mzigo kwetu.” – Seneca
LikeLike
Hakika
LikeLike
Ahsnate sana kocha, Tatizo halipo kwenye utajiri bali kwenye akili yenyewe.
LikeLike
Ndiyo
LikeLike
Asante sana kocha Kwa makala hii nzuri inayotutaka kubadili kwanza kile kiachotuzua kuufikia Uhuru tunaoutafuta.
LikeLike
Karibu
LikeLike
Ahsante.
1. uwezi kujikimbia mwenyewe kwa kutumia lift ya utajiri au umasikini(kinachotakiwa ni kuzibadili fikra zako)
na kinachobadili fikira zako ni falsafa
tuigize umasikini kwa kuwa umasikini ni uhuru na hakuna cha kupoteza
LikeLike
Kabisa.
LikeLike
Tatizo halipo kwenye utajiri bali kwenye akil8 yeneww
LikeLike
Ndiyo
LikeLike
Asante Kocha,
Ili maisha yawe bora, nitaitibu kwanza akili yangu.
LikeLike
Vizuri
LikeLike
Kama akili yako haipo huru ukiwa maskini jua pia kwamba haitakuwa huru ukiwa tajiri.
LikeLike
Huo ndiyo ukweli.
LikeLike
Ukiishi misingi ya falsafa ya
Ustoa unaweza kupata utajiri ambao hautakuwa mzigo kwako
Asante sana
LikeLike
Hakika
LikeLike
Asante kocha,Inabidi niishi maisha ya ustoa mapema sio mpaka niwe tajiri ndo niishi ustoa.vyote kwenye mafanikio inabidi viende kwa pamoja.
LikeLike
Hakika.
LikeLike
Matatizo unayo kimbia kwenye umasikini utakutana na matatizo kwenye utajiri, tiba ni falsafa ni ya kwenda nayo kwenye utajiri na wakati nautafuta.
LikeLike
Ndiyo
LikeLike
Jenga utajiri mkubwa lakini chagua kuishi kama maskini
LikeLike
Ndiyo.
LikeLike