3167; Msukumo sahihi.

Rafiki yangu mpendwa,
Sisi binadamu huwa hatufanyi maamuzi na kuchukua hatua kama hakuna msukumo ndani yetu.
Ni lazima kuwe na msukumo kwanza, tena ambao unagusa hisia ndiyo tuweze kuamua na kuchukua hatua.
Kadiri maamuzi na hatua tunazochukua zinavyokuwa kubwa, ndivyo msukumo unavyopaswa kuwa mkubwa pia.

Kabla ya kuendelea nitakupa mfano wa kichekesho ambacho kimebeba dhana nzima tunayotaka kujifunza hapa.
Bwana mmoja alikuwa anataka kupunguza uzito wa mwili wake.
Alienda sehemu ya mazoezi na kueleza mpango wake.
Aliambiwa kuna programu tatu, ya chini, ya kati na ya juu.
Aliamua kuanza na ya chini.
Alipelekwa kwenye programu hiyo na huko alikutana na binti mrembo ambaye alimwambia ukinikimbiza na kunikamata, nakuwa wako.
Yule bwana akaanza zoezi la kumkimbiza, alifanya hivyo kila siku kwa wiki nzima ndiyo akafanikiwa kumkamata.
Akawa amepunguza kilo 2.

Bwana huyo alivutiwa sana na mpango wa eneo hilo. Aliyaona matokeo haraka.
Basi akasema anataka programu ya kati.
Akapelekwa eneo la programu hiyo ya kati.
Hapo alikutana na binti mwingine mrembo zaidi ambaye pia alimwambia ukinikimbiza na kunikamata nakuwa wako.
Binti huyo alikuwa na mbio zaidi kuliko wa kwanza.
Bwana huyo aliweka juhudi na baada ya wiki mbili akawa amemkamata. Kupima kilo nyingine 5 zikawa zimepungua.

Alizidi kuvutiwa na huo mpango na jinsi matokeo yake yalivyokuwa makubwa.
Basi akataka programu ya juu kabisa, akiwa na mategemeo ya kukutana na binti mwingine mrembo zaidi.
Alipelekwa kwenye programu hiyo ya juu na kukutana na baunsa ambaye alimwambia nitakukimbiza na nikikukamata nitakubaka.
Yule bwana alikimbia sana, maana baunsa naye alikuwa na mbio kali.
Kwa mwezi mzima alikimbia mno na baunsa hakuwa amemkamata.
Lakini pia akawa ameweza kupunguza kilo 10.

Kichekesho hicho kimebeba mfumo mzima wa sisi binadamu kufanya maamuzi.
Huwa tunasukumwa na hisia za aina mbili.
Hisia za tamaa ya kupata, ambazo zinatusukuma kuchukua hatua ili kupata kitu fulani kizuri.
Na hisia za hofu ya kupoteza, ambazo zinatusukuma kuchukua hatua ili kuepuka kukosa kitu fulani kizuri.

Katika hisia hizo mbili, hofu ya kupoteza huwa ina nguvu na msukumo mkubwa kuliko tamaa ya kupata.
Na pale unapoweza kutumia hisia zote mbili kwa pamoja, yaani tamaa ya kupata na hofu ya kupoteza, msukumo unakuwa mkubwa zaidi.

Unapofanya maamuzi lakini ukawa unaahirisha kuchukua hatua, ni kwa sababu hujajiweka kwenye nafasi ya kupoteza kitu kikubwa kama hutafanya.
Kadiri hatari ya kupoteza inavyokuwa kubwa, ndivyo msukumo wa kuchukua hatua unavyokuwa mkubwa pia.

Pia kama una matamanio makubwa sana ya kupata kitu fulani, yanaweza kukusukuma kuchukua hatua kubwa na za tofauti ili kupata matokeo unayoyataka.

Muhimu ni unapojiona unashindwa kuchukua hatua unazopaswa kuchukua, jiweke kwenye hali ambaye utapoteza kwa ukubwa kama hutafanya.

Na hata pale unapowataka wengine wachukue hatua, usitumie tu matamanio, bali wawekee hofu ya kupoteza.
Watu wanapoona wanaweza kupoteza, wanasukumwa zaidi kuchukua hatua.

Jiweke wewe mwenyewe na wengine kwenye hatari kubwa ya kupoteza na msukumo utakaotokea utakuwa mkubwa sana.
Ni msukumo huo ndiyo utakaokuwezesha kufanya makubwa zaidi.

Ni tamaa ya kupata nini ndiyo msukumo wako wa kuchukua hatua kwenye hii safari ya ubilionea?
Na je ni hofu ya kupoteza nini ndiyo inakupa msukumo wa kuchukua hatua kwenye hii safari ya ubilionea?
Kwa tamaa na hofu uliyonayo, kipi kinakupa msukumo mkubwa zaidi?
Karibu ushirikishe kwenye maoni hapo chini.

#NidhamuUadilifuKujituma
#AfyaUtajiriHekima
#KaziUpendoHuduma
#UpekeeUdadisiUbunifu
#UshirikianoUtegemeanoUwajibikaji
#BilioneaMafunzoni
#NajengaBiashara
#HakunaKingineMuhimu
#LazimaNitoboe
#NawekaKaziNifanikiwe