3171; Usilipie unachoweza kupata bure.
Rafiki yangu mpendwa,
Kwenye ukurasa uliopita wa 3170, tumejifunza kuhusu kulipa ada kupitia makosa mbalimbali tunayofanya kwenye maisha yetu.
Pia tukaona hekima ni kujifunza kupitia makosa ya wengine ili usiyarudie.
Kwenye ukurasa huu tunakwenda kuangalia zaidi kuhusu kujenga hekima kupitia makosa ya wengine.
Ndiyo maana ukurasa unaitwa usilipie unachoweza kupata bure.
Maana yake ni badala ya kufanya makosa wewe mwenyewe na yakakugharimu, unapaswa kujifunza kwa wengine ili usiyarudie makosa hayo.
Warren Buffett na Charlie Munger ni wawekezaji mabilionea ambao wana mafanikio makubwa sana.
Kwa zaidi ya miaka 50 wamekuwa wanapata matokeo mazuri kwenye uwekezaji.
Japo kwa miaka yote kumekuwa na wawekezaji ambao wanapata marejesho makubwa kuliko wao, kupitia kuchagua uwekezaji unaolipa zaidi.
Lakini hao wawekezaji, mara kwa mara wamekuwa wakipoteza kwa ukubwa.
Kwenye vipindi mbalimbali, Buffett na Munger wamekuwa wanakataa kuwekeza maeneo ambayo yalikuwa na marejesho makubwa lakini yenye hatari kubwa pia.
Miaka ya 1990 mwishoni kulikuwa na ukuaji wa kasi wa makampuni ya teknolojia. Watu wengi waliwekeza huko na kupata marejesho makubwa kwa kipindi kifupi.
Lakini Buffett na Munger walikataa kuwekeza kwenye makampuni hayo. Watu waliwasema vibaya kwamba wanapitwa na fursa nzuri kwa sababu ya kuwa wagumu kubadilika.
Lakini haikuchukua muda makampuni hayo ya teknolojia yalipata hasara kubwa na wote waliowekeza kupoteza mitaji yao.
Buffett na Munger walibaki bila ya hasara yoyote.
Buffett na Munger wanapoulizwa kuhusu falsafa yao ya uwekezaji wamekuwa wanajibu vitu viwili vikubwa;
Moja ni wanawekeza kwenye yale maeneo ambayo wana uelewa nayo na pale unapotokea uwekezaji ambao una faida kubwa ila hawana uelewa nao huwa hawakimbilii kuwekeza, badala yake wanasubiri huku wakiangalia.
Na mbili ni badala ya kutaka kuonyesha wana akili sana, wao wamekuwa wanakazana kuepuka kuwa wapumbavu.
Na ndiyo maana wamekuwa hawapati marejesho makubwa kwa mara moja kama wawekezaji wengine, ila mwisho wa siku wamekuwa wanapata matokeo mazuri.
Kitu kikubwa tunachojifunza hapa ni kutokukubali kufanya makosa wewe mwenyewe, bali kujifunza kupitia makosa ya watu wengine.
Watu wengi waliofanikiwa huwa wanaonekana kama ni mgando, wanaozingatia misimamo yao ambayo kwa haraka inaweza kuonekana kuwapa hasara.
Lakini kwa muda mrefu, waliofanikiwa wanazidi kupata mafanikio makubwa, huku wale walioshindwa, ambao kila mara wanahangaika na mambo mapya wakizidi kushindwa.
Tofauti hapo ni makosa, waliofanikiwa wanajifunza kupitia makosa ya wengine na hivyo kutokuyarudia. Wakati walioshindwa wakirudia makosa yote peke yao.
Kwenye kujifunza kupitia makosa ya wengine kuna kitu kinaitwa hekima ya kundi. Kwamba ndani ya kundi, kila mtu kuna makosa ambayo anakuwa anayafanya.
Kama kila aliyepo kwenye kundi husika atajifunza kupitia makosa ya wengine na kutokuyarudia, ndani ya muda mfupi makosa kwenye kundi hilo yanakuwa madogo na watu wote kwa ujumla kupata matokeo bora.
Ndani ya kundi letu la Bilionea Mafunzoni tuna hazina kubwa ya makosa mengi ambayo watu wameshayafanya.
Kama tutajifunza makosa hayo kwa kina na kuepuka kuyarudia, tutaishia kupata matokeo makubwa sana.
Muhimu ni tusiwe na tamaa za muda mfupi na wakati mwingine tuwe tayari hata kupoteza faida kubwa za haraka ili kubaki na faida ndogo za muda mrefu.
Kwa maana hiyo basi tunakwenda kushirikishana makosa ambayo tayari tumeshayafanya na hatuwezi kuyarudia tena wala kuwashauri wengine kuyafanya.
Kwenye sehemu ya maoni hapo chini, orodhesha makosa yote ambayo umewahi kuyafanya wewe binafsi kwenye mchakato wa Bilionea Mafunzoni ambayo kamwe hutakuja kuyarudia na unashauri wengine wasiyarudie.
Pia shirikisha makosa uliyojifunza kupitia watu wengine ambao wameyafanya na yakawagharimu sana. Hivyo wewe umejizuia usiyarudie makosa hayo hayo.
Kila mmoja wetu ashirikishe aina hizo mbili za makosa, uliyofanya binafsi na uliyojifunza kwa wengine kwenye huu mchakato ili tuweze kutengeneza hekima ya kundi.
Kupitia uzoefu wa kila mmoja tutakuwa na orodha ya mambo ambayo hatupaswi kuyafanya.
Tutajenga msimamo mkali kwenye kuepuka mambo hayo ili tusirudie makosa ambayo yameshawagharimu wengine.
Haina maana kulipia kitu ambacho unaweza kukipata bure.
Japo wengi huwa hawathamini vitu vya bure, lakini kwenye makosa, kuna manufaa makubwa sana ya kujifunza kutoka kwa wengine.
Karibu ushirikishe kwenye maoni hapo chini makosa uliyowahi kufanya mwenyewe na kamwe hutakuja kuyarudia.
Pia shirikisha makosa uliyojifunza kwa wengine ambayo kamwe hutayafanya tena wewe mwenyewe.
#NidhamuUadilifuKujituma
#AfyaUtajiriHekima
#KaziUpendoHuduma
#UpekeeUdadisiUbunifu
#UshirikianoUtegemeanoUwajibikaji
#BilioneaMafunzoni
#NajengaBiashara
#HakunaKingineMuhimu
#LazimaNitoboe
#NawekaKaziNifanikiwe
Asante sana Kocha Dr Makirita Amani kwa kazi nzuri unayoendelea kuifanya.
LikeLike
Karibu
LikeLike
Makosa niliyofanya ni kuchukua mkopo mkubwa mara Kwa mara ndani ya ajira na kunifanya kushindwa kuachana na ajira. Kuamini zaidi wengine bila kuwasimamia Kwa dhati na kuangusha biashara nilizokuwa nimeanzisha.
Toka Kwa wengine: kuacha kazi Kwa mihemko pasipo kuwa na mpango madhubuti na kuishia kuwa na maisha magumu zaidi kuliko awali. Funzo ni kuweka mpango na kuutekeleza Kwa dhamira kubwa kabla ya kutoka Kazini.
LikeLike
Asante Zake kwa kushirikisha haya.
LikeLike
Makosa niliyowahi kufanya ambayo sitayarudia ni kuamini watu na kuruhusu wafanye maamuzi muhimu bila kufahamu historia yao ya nyuma, kwa sababu tu nimewazoea.
Makosa niliyojifunza kutoka kwa wengine ambayo kamwe sitayafanya mimi mwenyewe ni kufanya makosa kwenye mahusiano ya kimapenzi ya muda mrefu kwa maana ya ndoa.
LikeLike
Asante sana Sebastian kwa kushirikisha haya.
Tafadhali fafanya zaidi namba mbili, makosa yapi watu wamekuwa wanafanya kwenye hilo eneo la ndoa?
LikeLike
Kuwaamini ndugu na kudhani kwamba nikiwapatia fedha wanaweza kufanya biashara zinazoweza kutunufaisha sisi some.
Makosa ya wengine.
Wafanyakazi wengi kazini kukimbilia mikopo ili tu waonekane wana magari na nyumba.Wanaamini sana mafanikio yapo kwenye vitu hivyo.
LikeLike
Asante sana Innocent kwa kutushirikisha makosa haya.
LikeLike
Makosa niliyofanya ni kuhangaika na mambo mengi Kwa Kwa wakati Mmoja. Ningeweka nguvu SONGAMBELE CONSULTANTS tangu nipo chuoni na kupuuza mengine yote. Ingekuwa Mbali sana.
Makosa ya wengine.
Ni kujifunza kutoka Kwa baba mdogo wangu. Aliyefanya harusi Kwa mkopo alitaka kuwaridhisha watu. Alitegemea zawadi za harusi zitatudisha Hela, ila haikuwa hivyo
Hili deni limemtesa Kwa miaka Sasa tangu 2018. Maana alifikia hatua ya kukopa hapa na kulipa pale.
LikeLike
Asante sana Godius kwa kutushirikisha haya.
LikeLike
Makosa niliyofanya nikutafuta Utajiri wa haraka niliwahi kupata fursa ya kuuza bangi kuitoa congo kuichukua Kampala mara ya kwanza nikapata faida ya milioni mbili lakini mara ya pili nilipoteza milioni 6 police walinishika nakunipeleka gerezani kwasababu yakufanya biashara ambayo haikubaliki na serekali na ilikuwa kwasababu ya mimi kutafuta njia ya mfupi yakufanikiwa,pia tusiwaamini sana watu kwasababu yule ambaye alipelekaga ripoti kwenye Police kwamba nauza bangi alikuwa ni huyo huyo Boss ambaye alikuwa nainunua hiyo bangi kwa hiyo hapa KCM tupo sehemu sahihi yaani kila siku kocha huwa anatusisitiza kwamba tukatae njia ya mfupi yakufanikiwa yaani tuepuke sana short cut tuendelee kukaa kwenye mchakato ni swala la muda tuu tutafanikiwa.
Makosa ya wengine ni wengine kujionyesha kwamba wamefanikiwa kununua magari za kifahari kujenga manyumba za kifahari kumbe hela ni za mkopo kwa hiyo nimejifunza kwamba Utajiri ni kitu ambacho huwa hakionekane yaani nikiwekeza hela zitaleta faida kuliko kununua gari za kifahari na manyumba za kifahari
LikeLike
Vizuri sana Kizito kwa kushirikisha haya.
LikeLike
Makosa niliyofanya ni kumuamini mfanyakazi wangu kwenye biashara mwisho wa safari akaniibia.
Makosa ya wengine ni kwa wafanyakazi waliojiriwa kutegemea Pension na kiinua mgongo baada ya kustaafu kama pesa ya kuendeleza maisha matokeo yake ndio chanzo cha Stresi za maisha na kufa mapema.
LikeLike
Asante Ali.
LikeLike
Makosa niliyowai kufanya i) kusubiri kila kitu kikamilike ndipo nianze ii)Kusubiri kipato kiwe kikubwa ndipo niweke akiba
Makosa waliyofanya wengine ambayo mimi nimejifunza i)Kukopa mkopo mkubwa kwa lengo la kukua haraka kibiashara ii)Kutoa hela mapema kwenye biashara na kuanza kujenga kabla biashara haijakomaa.
LikeLike
Asante Fabian
LikeLike
Makosa niliyowahikufanya ni kufanya kazi kwa kuwaridhisha wengine huku mambo yangu yakilala. 2. Kufanya mambo mengi kwa wakati mmoja badala ya kuweka nguvu kwenye mambo machache yenye tija; mfano: Nilikuwa rais wa Frisbee Tanzania, Mwanzilishi wa NGO, Mwanasayansi, Mkulima; Mwandishi wa vitabu na mfanyabiashara.
Makosa ya wengine.
Makosa niliyojifunza kutoka kwa wengine ni; eneo la mahusiano kutoka kwa Mzee wangu ambaye kutokana na makosa aliyokuwa akiyafanya; kila mwaka alikuwa akioa na kuacha mpaka kufikia wanawake 12 na wote hao walikuwa wanaondoka na mimba au watoto. Hali hii ilikuwa inamfanya kuanza upya kila mara, na hivyo kutokuwa sawa kiuchumi.
LikeLike
Asante Felician kwa ushirikisho hasa huo wa namba mbili. Kuna funzo kubwa sana hapo.
LikeLike
Makosa nilyowahi kufanya ni kukimbilia fursa za kupata heka harakaharaka na ambazo ni rahisi hasa za mitandaoni ambazo zilinifanya nipoteze pesa. Pia kumwaminj mtu ambaye nilimpa mzigo wa bidhaa kwa mali kauli na baadae akauza wote na hela akawa hana ya kurejesha.
Makosa ambayo nimejifunza kwa wengine ambayo sitayafanya ni kukopa mikopo ambayo siyo ya biashara
LikeLike
Asante Petro.
LikeLike
Makosa niliyowahikufanya ni kuchelewa kuoa kwa kutarajia mambo yatakua mazuri ndio nioe. Mambo hayakwenda kama nilivyotaraji na muda mwingi ulipotea.
Tunatakiwa kuwekeza nje ya biashara kwa inapotokezea dharura hatutaanza chini kabisa
LikeLike
Asante Hassan
LikeLike
Asante sana kocha, binafsi hasa ni kuhusiana na matatizo ya mahusiano,niliishi kwenye mahusiano yaliyonitesa kwa takribani miaka 15,nikidhani kwa kuwa mimi na mwenzangu tunatoka eneo moja,kabila moja,dini moja,nikaamini ni mambo ya kupita tutaa kaa sawa na maisha yaendelee ukizingatia wakati huo tayari tumeishapata watoto watatu ambao ndiyo yalikuwa malengo yangu/yetu, mateso haya ni Hadith ndefu sana niliishia kesi nyingi mno,mwishowe Mungu alisimama,kocha akiwa sehemu kubwa ya mshauri wangu,sasa nimeoa tena,na maisha ya furaha na Amani,sikuwasikuwahi kufanya biashara kutokana na karaha hizo,za kila mara,sasa nafanya biashara na maisha yanaonyesha mwanga, muhimu tumtumie kocha na kumwamini sana kwa vitu vingi hata binsfs.
Kujifunza kupitia wengine, kupitia kipindi cha kitimoto hapo ndipo watu wanafunguka zaidi, Napenda historia ya ndg yangu Datius alipoenda kuanza biashara akajikuta ananunua mzigo kwa bei ya kuuzia ili auze naye,ni historia fupi,lakini wengi mara nyingi tunapokuwa tunaanza biashara tunakutana na hali hiyo,nini cha kujifunza
Kutokata tamaa kuhakikisha lengo na nia uliyonayo unaifikia, maana baadae kocha alimkutanisha na mchungaji yule muuza mitumba wa Mbeya jina kidogo nimelisahau,akajishusha,akakubali kujifunza maisha yanaendelea.
Asante sana kocha.
LikeLike
Asante sana ndugu yangu
LikeLike
Asante sana Beatus na hongera kwa kuvuka changamoto iliyokusumbua kwa muda mrefu.
LikeLike
Makosa ambayo nimewahi kufanya
1 Kuanzisha biashara ya pamoja na mtu ambaye nipo mbali naye wakati huo biashara akiwa anaiendesha yeye huko hapa utatamani ulie na kumfukuza huwezi
2 Kosa jingine ambalo huwa linaiumiza ni kushindwa kuanzisha biashara sehemu furani mkoani kwenye fremu baada ya wiki Moja mtu akichukua na kuanzisha biashara ile ile niliyokuwa nimepanga kuanzisha
Makosa niliyojifunza kwa wengine
1 Kuanza ujenzi kabla biashara haijaimalika
2 kutumia fedha ya mkopo kujengea
3 Kuwa na mali ambazo zinachukua fedha nyingi kuliko inayoingia kupitia mali hizo
LikeLike
Asante Bosco
LikeLike
Kosa kubwa ambalo nimewahi kufanya ni kufanya biashara ya duka na ndugu huku nikiwa mbali kwa kwelii
Nilipoteza pesa yote sikupata hata senti moja. Nimeapa sintarudia Tena kosa Hilo.
Kosa ambalo nimejifunza kwa wengine ni kubadili badili kazi au biashara , jamaa zangu ambao wamekuwa hawatulii na Jambo moja kwa wakati wote Hadi Leo hii wanamafanikio kidogo Sana , nimejifunza kutoka kwao hatari iliyopo ya kubadili biashara au kazi kunavyo chelewesha mafanikio, hivyo siwezi kufanya makosa hayo.
LikeLike
Asante Miraji.
LikeLike
Makisa niliyowahi kufanya ni kuchelewa kuchukua hatua kubwa katika kufanya Uwekezaji mapema katika maeneo muhimu ambayo leo yangekuwa fulsa kubwa zaidi kwangu.
Kosa ambalo nimejifunza kutoka kwa wenzangu ni kushindwa kuanza kuwekeza mapema na umri umekwenda na nafasi hakuna tena ya kufanya uwekezaji
LikeLike
Makosa Ambayo Nimewahi Kufanya; Kuchelewa Kufanya Maamuzi Sahihi.
Makosa Ambayo Nimejifunza Kwa Wengine.
1. Kuchanganya Mambo.
2. Kutokuwa na msimamo.
3. Kushindwa kufanya maamuzi sahihi, ni hatari kwa maisha ya mtu.
LikeLike
Asante Mseco kwa makosa uliyishirikisha.
Umeyashirikisha kwa ujumla sana, yaani juu juu. Tafadhali nenda ndani zaidi, mfano unaposema kuchelewa kufanya maamuzi sahihi, unamaanisha nini? Toa mfano ili tuelewe vizuri.
LikeLike
Asante Patson.
LikeLike
Kosa nililofanya; kutokuwa makini na mfuatiliaji kwa vile tu ni ndugu/mwenza/sifa fulani na mwisho wa siku mtu anajali maslahi yake tu. Nitashirikiana na yule tu tunaeaminiana na kujali maslahi yake na yangu pia.
Kosa la wengine: kumchagulia mtoto mwenza wa kuoa/kuolewa naye kwa kigezo cha kabila, rangi, dini, elimu, utajiri na mengine kama hayo. Sitafanya hivyo kwa mtoto/watoto wangu.
Asante sana Kocha.
LikeLike
Makosa niliyofanya kwenye maisha yangu ni kuwaamini watu hasa wafanyakazi na kupelekea kurudi nyuma kimaisha pia kuchukua mikopo isiyokuwa na tija
Makosa niliyojifunza Kwa wengine ni kutawanya nguvu kutokutulia na kitu kimoja
Asante saba
LikeLike
Asante Ernest
LikeLike
Kosa nililofanya nikumwamini ndugu yangu na kumpa fedha ili ananue bidhaa kwa ajiri ya biashara ya pamoja na yeye akiwa. Pesa yote ililiwa na hakuna bidhaa iyoonekana.
Makosa niliyojifunza kwa wengine. Mama mkwe wangu ana shule. Alipata mwalimu mmoja mkorofi sana na hafanyi kazi zake vizuri. Basi aliamua kumfukuza kazi yule mwalimu. Laki mama yangu alipelekwa mahakamani na yule mwalimu na kushindwa kesi. Kisa alikuwa hajamwandikia barua yoyote ya kuomuonya. Akawa amehukumiwa kuwa ni mnyanyasaji. Ilibidi mama amlipe yule mwalimu mamilioni ya pesa kama fidia kwa usumbufu
LikeLike
Asante Kashinje, hilo la pili ni muhimu sana, kila mmoja alizingatie.
LikeLike
Makosa niliyowahi kufanya mwenyewe na kamwe sitakuja kuyarudia.
1. Kutokuanza uwekezaji mapema
2. Kutokufanya biashara mapema
3. Kutokujiamini katika maamuzi ninayofanya na kusubiri comments za watu.
Makosa niliyojifunza kwa wengine ambayo kamwe sitayafanya tena mimi mwenyewe.
1. Kujifunza na kutokuweka kwenye matendo
2. Kukata tamaa badala ya kuendelea kujifunza
3. Kudharau mtu wakati kuna kitu cha kujifunza kutoka kwake
LikeLike
Asante Huvira.
LikeLike
Makosa Niliyofanya
1.Kuchelewa kufanya Uwekezaji kwa Msimamo kwenye Liquid Asset kwa Msimamo
2. Kutokaa kwenye fursa moja kwa muda mrefu mpaka ifanye kazi
3. Kuchukua mikopo kwa wingi sehemu tofauti
4. Kufanya kilimo cha simu ambapo nilipoteza 5m kwa kuamini hadithi za mtu ambaye nillisoma nae sekondari kwa kukosa msingi wa kusimamia fursa
Kwa wengine
1. Biashara inataka kazi kubwa na kujitoa bila hivyo unapotea haraka.
2. Usipokuwa na Uwekezaji biashara ikianguka unapata anguko kubwa
3. Kuna umuhimu wa kuzingatia mchakato kwani ukitolewa unakuwa unaona kuna kitu kikubwa umepoteza
4. Kuacha kazi lazima uwe na cashflow ambayo utaweza kukidhi mahitaji yote ya msingi ili usitamani kurudi nyema tena
LikeLike
Asante Martin.
LikeLike
Makosa niliyowahi kufanya
1. Wasaidizi kutumia namba zao binafsi kuwasiliana na wateja
2. Kuamini shule na ajira vitanifikisha kwenye mafanikio makubwa
Makosa niliyojifunza kutoka kwa wengine
1.Madhara ya kuchelewa kuondoka kwenye ajira
2.Madhara ya kuchelewa kuanza uwekezaji mapema
LikeLike
Asante Reinfrid.
LikeLike
MAKOSA YA WENGINE,
1/Kujiingiza kwenye matatizo ya wengine, yaani kutaka kutatua changamoto za wengine wakati mimi mwenyewe nina matatizo,
2/Kuamini wengine kirahisi zaidi, na hili kupelekea kutapeliwa mara mbili kwa awamu mbili tofauti hasa kwenye biashara ya mpesa,.
3/Kosa jingine ambalo linanitesa mpaka leo ni la kuifunga biashara ya mke na kumruhusu aje kwenye biashara yangu tushirikiane,,(mgumu kufuata utaratibu wa biashara,(anakuwa mzigo).
MAKOSA YA WENGINE,
1/kuacha kazi ya kuajiliwa inayo lipa vizuri na kuanza ujasiliamali wakati hujawa tayari..
2/Kukurupuka kutaka maisha ya anasa bila kuwa na kiasi kikubwa cha fedha cha kuweza kumudu gharama..
3/Kufukuza fukuza wafanyakazi kwenye biashara bila hata kuwapa adhabu kwanza kuona kama wanaweza jirekebisha…
4/Kuleta ujuaji wako kwa coach ama mwalimu wako, wakati unazipenda mbinu za mwalimu..
5/Kuhangaika na mengi sio njia ya kupata unachokitaka,, unaweza baki na kimoja na ukanufaika nacho.
LikeLike
Asante Helanane, hilo la kushirikiana na mwenza kwenye biashara limewagharimu wengi. Tujifunze sana hapo.
LikeLike
Makosa yangu
Kwanza kabisa sikua najua wa kulaumiwa ni mimi mwenyewe na siyo mwingine pale kazi inapoharibika
11.nimekua natoa mtaji wa biashara kupeleka kununua nyumba viwanja na magari makubwa na hiyo kupelekea biashara kuyumba sana
Ukirudi upande wa hivyo nilivyonunua havileti hela dukani na havizalishi
2.kutumia hela za biashara kwenda kufanyia kilimo na ufugaji jambo ambalo ni baya sana kibiashara
3.kosa la tatu ni kutawanya muda wa kazi na wakati mwingine kutokuonekana hata wiki kazini na siyo jukumu la biashara
4.kuwaamini watu na kuwaachoa biashara bila kuwa nao karibu
Makosa hayo yote yamepelekea mimi kufeli sana kibiashara
Niliyojifunza
Baada ya kuingia bm
1.nilijifunza kufanya jaambo moja tu hadi lilete matokeo na kuzaa lingine
2.kusaka kwa msimamo na kufuatilia wateja kwani hawawezi kuja wenyewe make wamevurugwa sana na watu
Kuweka akiba na uwekezaji mimi nilikua ziro kabisa
Na jingine nililopàta ni kuwa na ushirikiano na kundi la bm
Jambo la tatu ni kujenga nidhamu kali
LikeLike
Asante sana Dickson.
LikeLike
MAKOSA YNG
Kutaka kufanya Mambo mengi
👉Kilimo ili kupata hela haraka
👉 Kuzalisha bila msimamo
👉Kutoa huduma za kitaaluma N.k
MAKOSA YA WENGINE
👉 Kutopenda kuwekeza nguvu kwenye kitu kimoja kwa
muda mrefu mpk kilete matokeo
👉Kutokuweka vipaumbele,AKIBA ,KUJIFUNZA na
uwekesaji
LikeLike
Asante Mwijage.
LikeLike
Makosa yangu ni
1. Kutawanya nguvu Kwa kufanya Mambo mengi tofauti Kwa wakati mmoja
2. Kutokusema.hapana kitu kimenifanya kuwa busy sana na mambo yasiyo ya msingi
3 . Kutokuwekeza Kabisa.na kukosa akiba kabisa
4. Kutokuwa na budget ya matumizi yangu na kwenda na linalokuja mbele na kukosa vipaumbele
5. Kushindwa kuchukua hatua Kwa wafanyakazi kitu ambacho kilijenga utamaduni mmbaya kwenye biashara
Vitu nilivyo jifunza ni
Kufanya Jambo moja mpaka liweze kujiendesha lenyewe
Pili nimejua maana ya kusema hapana kwenye baadhi ya mambo
Tatu kuweka budget kwenye kila Jambo unalofanya
Na mwisho ni kujifunza kufukuza mara moja na kuajiri taratibu. Na pamoja na kuwa na nidhamu kwenye kila unachofanya
LikeLike
Asante Elihuruma.
LikeLike
Makosa ambayo nimewahi kufanya ni kukopesha fedha kwa rafiki yangu wa karibu sana nikiwa naamini bila ya shaka yoyote kuwa atanirudishia fedha hiyo, mwisho wa siku ikawa ni uadui, fedha hakurudisha ni urafiki ukaishia hapo hapo. Tangu siku hiyo nilijisimea kuwa sitarudia tena kumuamini mtu yeyeto kwenye maswala ya fedha.
Makosa ya wengine.
■Kukopa mikopo na kununua vitu ambavyo vitaonekana kwa wengine ili kujionesha kuwa tayari wameyapatia maisha.
■Kujipendendekeza kwa viongozi ili kuweza kupata fursa mbalimbali zinazotokea.
■Kushindwa kusimamia haki hata kama inaonekana wazi wazi kuwa sehemu fulani kuna uonezi. Mtu anashindwa kusimamia kile kilicho sahihi kwa sababu ya kuogopa kupoteza nafasi aliyopewa.
LikeLike
Asante Datius.
LikeLike
LikeLike
Asante Yusuph
LikeLike
Jifunze kupitia makosa ya watu wengine
LikeLike
Tafadhali shirikisha kama nilivyoelekeza kwenye makala.
LikeLike
Makosa niliyowahi kufanya Mimi binafsi
1.kuwasaidia watu nikiona kama nisipo fanya hivyo wataniona ni naroho mbaya
2.kumwamini sana mwanadamu kuwa hakosei kama mume kumbe nae kunawakati anakosea
3.kuwaeleza watu Siri ZANGU za maumivu nikijua watanisadia kumbe wananitangaza
4.kuwa mwoga Mahalia pa kazi Kila kiongozi anaponiita nakutakia kunisema nilikuwa nalia sana na kumwomba msamaha wakati kosa halieleweki
5.kufungua biashara ovyo ovyo Kila mtu akinishauri kufanya biashara nafanya akisema huku Kuna FURSA nakwenda na mwisho nikapoteza hela
Makosa ya wezangu
1.kupoteza muda kuijadili serikali hasa watumishi Kila siku kuisema serikali haijali maslai na hatua hawachukui za kupata maendeleo.
2.kutojali mahusino kuonda kuwa single kwa sababu wanakipato
3.kuishi kwa anasa kutaka kuonyesha watu unamaisha mazuri kumbe sio kweli
4.kuacha kujifunza wakati dhama zinabadilika .
LikeLike
Asante (naamini hapa ni Christina).
LikeLike
asante sana Selaman hapo kwa kuamini mtu unamwelezea ishu zako kumbe anakwenda kukutangaza vibaya ni shida kweli
LikeLike
Makosa yangu
~kukimbilia kila fursa inayokuja pasipo kufanya uchunguzi, hapa nimepigwa mihereka yakutosha kuanzia bunge la uchumi, JUTA, na biashara ya vocha, fursa hizi zimenifanya nipoteze mamilion ya fedha siyo chini ya million kumi
~kosa lingine nikujiripua katika kutumia bidhaa Kwa maelezo ya wengine pasipo kijalibu mwenyewe kidogo kidogo hapa napo nimepigwa na kitu kizito sana,
~kukopa fedha yaliba kubwa Kwa matarajio ya fedha iliyopo mikononi mwa serikali, Daaa! Hili limegharimu mwaka mzima wakulipa madeni, Madeni, madeni, madeni ni adui mkubwa WA maendeleo hapa nimejifunza sana.
Makosa ya wengine.
~kutokusamehe na kuachilia mambo
~kusikikiza ushauri WA watu pasipo kufanyia uchunguzi
~kukurupuka katika kufanya maamuzi muhimu
LikeLike
Asante Mapunda.
LikeLike
Makosa niliyoyafanya mimi;
1. Kuchelewa kuanza kujenga timu nikiamini ninrahisi sana kupata wafanyakazi sahihi wa biashara. Hii ilikuja kuonakana tofauti pale nilianza kutafuta timu na kugundua kuwa kuna watu wengi wanaotafuta kazi, lakini waliotayari kufanya kazi ni wachache sana.
Niliyojifunza kutoka kwenye makosa ya wengine.
1. Kutotengeneza mazingira mazuri kwa wafanyakzi wa biashara, kunapelekea wafanyakazi kutoamini maono makubwa ya biashara na hivyo kutobaki kwenye biashara zetu.
Asante Kocha
LikeLike
Asante Alfred.
LikeLike
Makosa ambayo niliwahi kufanya ni kununua ardhi badala ya kuwekeza fedha hiyo kwenye mfuko wa UTT. Ardhi ambayo Iko mbali na ni kijijini gharama za kusafisha ni kubwa ukilinganisha na niliyonunua nimeona bora liende na hiyo hela niwekeze utt.
Usikimbilie kununua viwanja, wekeza fedha hiyo kwenye mfuko wa uwekezaji iendelee kuzaa.
Makosa ambayo nimejifunza kutoka kwa wengine ni kustaafu kazi mapema.
Baba yangu mdogo amestaafu kazi mapema huku akiwa hajajiandaa hivyo maisha yanampiga kwa sasa na kupelekea kurudi kijijini.
Aliamini akipata fedha ya mafao, maisha yake yataenda vizuri.
Usistaafu kazi, fanya kazi mpaka siku yako ya mwisho hapa duniani.
Asante sana
LikeLike
Asante sana Mwl Deo.
LikeLike
Makosa niliyo wai kuyafanya
1.nilikuwa nikiwapa ndugu zangu hela huku nikiamini kua wote tuta toboa kwenye kuongea hivi wanaonesha niwatu makini na wenye uhakika kwa wanachoenda kukifanya ila kwenye vitendo ni tofauti kabisa nilipoteza hela nyingi sana kwa kupitia njia hio
2.baada ya kuwa namuazimisha kaka angu hela akaanza ujenzi nimimi nikajioji yakuwa kaka angu alikuwa anasoma marahii kaanza kujenga alafu mimi bado sijafanya chochote huku nikisahau kuwa hela anazo jengea ni pamoja na hela niliyo muazimisha nami nikaanza kujenga huku nikiwa mkopo mkopo nikayumba mnoo ilibaki kidogo nipotee kabisaa
MAKOSA YA WENGINE
Nimejifunza kwa watu waopo kwenye kisima na walio toka hua wanapata maarifa makubwa ambayo wasinge yapata popote ila wanajisahau na kuona maarifa hayo walikua nayo tokea mda jambo ambalo sio kweri sio sawa
2.watu mbali mbali ambao wamepata maanguko ya kibishara na chanzo kikubwa kikiwa usimamizi wa biashara mbovu au kutoa fedha kwenye biashara kwenda kufanyia vitu vingine kama ujenzi na kazalika,
LikeLike
Asante sana Cosmas.
LikeLike
Makosa niliyofanya kwenye maisha yangu ni kuwaamini watu hasa wafanyakazi na kupelekea kurudi nyuma kimaisha pia kuchukua mikopo isiyokuwa na tija
Makosa niliyojifunza Kwa wengine ni kutawanya nguvu kutokutulia na kitu kimoja
Asante sana
LikeLike
Vizuri
LikeLike
Asante kocha,
Makosa yangu ninayoyajutia,
(1), Kuamini ndugu na kuweza kuwaachia biashara zangu kuwa wataweza kusimamia vyema,matokeo yake wakawa wananiibia fedha za biashara.
(2), Kuingia kwenye mikopo bila kuwa na malengo na kujikuta natumia pesa kwa ujenzi na anasa bila kufanyia biashara na nikaanza marejesho ambayo yalinisababisha mpaka kutaka kukimbia mji na kurudi kijijini.
(3), Kuingia kwenye kilimo na kupoteza pesa nyingi bila kurudisha chochote.nilipata hasara kubwa.
Makosa niliyojifunza kwa wengine ni,
(1),Kutofanya uwekezaji mapema,
(2),Kufanya mambo mengi baada ya kuweka nguvu kwenye kitu kimoja.
(3),Kutokaa kwenye mchakato wa bm.
LikeLike
Asante Didas.
LikeLike
Kwanza kabisa nakupongeza kocha kwa kuandika ukurasa huu,lakini pili nikuombe radhi kwani nimechelewa kutoa mrejesho ili kuweza kutengeneza hekima ya Kundi lakini sasa nakwenda kushirikisha kama ifuatavyo;
1.MAKOSA NILIYOFANYA.
A.Kuweka nguvu kubwa kwenye kuisaidia biashara iweze kukua kwa kujifunza na kuongeza mtaji huku nikisahau kuweka nguvu kwenye team.
B.Kuchanganya fedha za biashara na fedha zangu binafsi kwenye matumizi.
C.Kuajiri mtu bora ana pumua na siyo mfanyakazi bora.
D.Kununua biashara ambayo siyo ya ndoto yangu na kuyumba kwenye biashara ya ndoto yangu.
Niliyojifunza kupitia wengine.
1.Kuishi kwa bajeti na kuto tumia juu ya bajeti.
2.Namna bora ya kusema hapana na kuleta mafanikio makubwa.
3.Uvumilivu unalipa sana baada ya kuweka kazi na kujipa muda.
Hayo ni machache kati ya mengi asante sana kocha.
LikeLike
Asante sana Kelvin
LikeLike
Makosa niliyofanya ni kuajiri bila kuzingatia vigezo vyovyote watu wenye uwezo mdogo kwenye biashara yangu na kuwa na huruma ya kuwaondoa hata baada ya kuniingizia hasara.
Makosa ya wengine ni watu kutoa fedha kwenye uwekezaji wao hasa wa UTT ndani ya muda mfupi na kila mara kuwa watu wa kuanza kufanya uwekezaji na hivyo kupoteza ukuaji wa riba mkusanyiko. Asante sana kocha kwa somo hili.
LikeLike
Asante Basil.
LikeLike
Vizuri Awadhi kwa haya uliyoshirikisha.
LikeLike
Makosa yangu
1. Kuamini wafanyakazi katika masuala ya kifedha na hivyo kunigharimu
2. Kuchelewa kufanya maamuzi ya kutenga Zake Advocates na TLG
3. Kupuuzia michakato ya kodi TRA kiasi cha kunigharimu
Makosa ya wengine
1. Kutawanya nguvu katika kazi mbalimbali
2. Kutofanya uwekezaji mapema
3. Kutoka kwenye mchakato wa BM
LikeLike
Vizuri Zake kwa haya uliyoshirikisha.
LikeLike
Makosa Niliyowahi kuyafanya ni mengi.Ikiwemo
Kuchelewa kujua umuhimu wa kujifunza,
Kuanzisha biashara kwa mtazamo wa mkono kwenda kinywani.
Kuchukua mikopo kwa Lengo la kutumia kwa matumiz yasio muhimu
Kuamini Watu na baadae kunigharimu.
LikeLike
Vizuri Rashidi kwa kushirikisha haya.
LikeLike
Asante sana Kocha.
Makosa yangu.
Kukubali kushawishika kwa haraka na kuingia kwenye mapenzi na baba aliyeoa kwa kudanganywa na pesa Hadi nikazaa nae mtoto. Kosa hili limenigharimu Hadi wa Leo nikifikiria najichukia sana.
Kosa la wengine.
Kosa kubwa nimejifunza kutoka kwa baba yangu alikuwa anaahidi sana kwamba atatekeleza hilo na hili lakini mwisho wa siku hakuna anachofanya, alikuwa anapenda sana kusema lakini kwenye utendaji hakuwa anatenda. Anaweza ahidi kuwa atalipa karo wiki ijayo lakini inapofika analeta visingizio kuwa kama haingekuwa hili angekuwa amekamilisha, kumbe ameshatumia fedha hizo kwa njia mbaya. Nimefunza kuwa nitakuwa mzazi wa kutegemewa na ninapoahidi kitu kwa mwanangu lazima nitekeleze kama ninavyoahidi. Sitapenda kuwa msemaji bali mtendaji zaidi.
LikeLike
Vizuri Maureen kwa kutushirikisha haya ambayo ni maumivu ya ndani kabisa.
Yamebeba funzo kubwa ndani yake.
LikeLike
Kosa kubwa nililowahi kufanya ni kurudia makosa na kufanya uzembe kwenye eneo la kufanya maamuzi.
Makosa niliyojifunza kutoka kwa watu wengine ni kutokua na udhibiti
LikeLike
Asante Kasanda
LikeLike
MAKOSA TOKA KWANGU.
1.Kuruhusu hisia kutawala zaidi kuliko kufikiri haswa kwenyr mambo ya mahusiano kimapenzi.
2.kuondoa fedha ya uwekezaji UTT kwenda kwa mambo mengine,na kuvuruga nguvu ya uwekezaji kwa msimamo.
3.kutokua na mental model kufikiri mambo nje ya yale tuliyozoea kuyaona.
4.Matumizi ya vilevi kupelekea kupoteza fedha na hasara zingine.
5.Kutokua na ratiba ya kuniongoza siku yangu iende vipi kwa mpangilio kwa mambo yakufanya.
Makosa kutoka kwa wengine.
1.kukimbilia mikopo haswa waajiriwa kwenda kujenga nyumba kwa mkopo haraka haraka,au magari au kuanza biashara kwa mkopo.
2.kuendesha biashara bila mfumo kwa kufikiri biashara ni mtaji tu nunua kwa bei ndogo uza kwa bei kubwa upate faida.
3.kutokuwekeza hata kwa kiwango kidogo cha 10000 kwa kufikiri uwekezaji ni mpaka uwe na fedha nyingi.
4.Kuamini serikali inawajali sana watu wake .
5.kutokua na kocha wa kukusimamia na kukuonyesha unapokosea kwenye safari ya mafanikio.
6.kufurahia siku za mapumziko na kujiingiza kwenye starehe zilizopitiliza na kupoteza fedha.
LikeLike
Asante Hendry kwa kushirikisha haya.
LikeLike
MAKOSA NILIYOFANYA AMBAYO WENGINE WANAWEZA KUJIFUNZA KWANGU
1. Kuchelewa kuanza kuwekeza UTT na hata nilipoanza kuwekeza nikawa naweka kidogo Sana wakati nilikuwa na uwezo wa kuwekeza zaidi. Lakini pia sikuwekeza kwa Msimamo, mpaka Sasa ningekuwa na uwekezaji mkubwa.
2. Kutokuweka akili ya kupoteza kitu Cha thamani, kitu kilichonigharimu kwa kupata maumivu makali baada ya kumpoteza mpenzi wangu.
3. Kupenda kupata utajiri wa haraka, kwa kujiunga na biashara za mtandaoni , japo Mimi niliopata faida lakini waliojiunga chini yangu wakapoteza na kunilaumu na wengine kutishia kuvunja mahusiano kama marafiki.
Kuamini zaidi kusoma na kuajiriwa kuliko biashara, kwasababu ya kukosa elimu ya biashara. Hili limenichelewesha Sana kujua kiuchumi japo nilikuwa naitamani Sana kujua.
MAMBO NILIYOJIFUMZA KUTOKANA NA MAKOSA YA WENGINE
1. Kukopa Fedha ya matumizi ambayo jaizalishi na kujikuta Hana Raha kwa kudaiwa kwa kitu ambacho alishatumia na bado matumizi yanamdai Tena.
Kuto kuthamini mahusiano na kupambana na mambo ya uchumi na kuiongeza kipato Huku akisahau familia. Hatari hii unakuta ameacha kupambana na kupiga vita adui umaskini Sasa anapambana kutatoa migogoro yao ya kifamilia.
Ulevi na ukahaba unavyoweza kuharibu maisha ya mtu pamoja na uchumi wa familia.
LikeLike
Asante Enelisa kwa kushirikisha haya.
LikeLike
#Makosa niliyofanya mimi
1. kuridhika na kujihisi tayari nina pesa.
2. kutokujua ninakoelekea kibiashara.
3. kuwekeza kwa kiwango kidogo sana na kuwekeza kwenye maeneo ambayo sina uzoefu nayo.
makosa ya wengine.
kushindwa kufanya maamuzi kwa kuogopa ndugu.
kuridhika na kujisahau.
kutokupanda mbegu ya ujasiliamali kwa watoto wao.
kuwaacha watoto wasomee fani wanazopata badala ya kuwachagulia kulingana na mahitaji ya familia yao.
LikeLike
Vizuri Selemani kwa haya uliyoshirikisha.
LikeLike
Makosa yangu
Kuanza biashara kwa mkopo hii ilipelekea mtazamo wangu kumtegemea mkopo tuu Ili kuendesha biashara
Kutaka kufanya Kila kitu peke yangu na kuamini hakuna anaeweza kufanya kama Mimi hii ilinichelewesha kupata timu Bora
Kuajiri ndugu ambao waliishia kufanya biashara kwa mazoea na sikuwa na uwezo wa kuwawajibisha
Kutumia pesa za biashara kwa matumizi binafsi na kushindwa kukuza mtaji
Makosa ya wengine
Kukosa elimu ya fedha na uwekezaji hivyo kushindwa kuwekeza
Kudharau umuhimu wa Kocha na kuishia kukosa usimamizi sahihi kwenye biashara
Kukimbilia kutoa/kuolewa kwasababu ya sababu zisizo za msingi kama maneno ya watu,umri,muonekano wa nje na hata pesa au Mali na kuacha kuangalia vitu muhimu kama utayari wa mtu,maono/makusudi, Imani za msingi(values) na tabia binafsi.
LikeLike
Vizuri Rejoyce kwa kushirikisha.
LikeLike
Makosa yangu binafsi
– Kuchagua kuamini maneno badala ya kutazama matendo, nilikuwa mwepesi sana kuamini watu na baada ya kuwasililiza na kuamini watafanya kama ambavyo kwa nafasi yangu ningefanya lakini nikagundua kuwa mwishi was iku napata hasara ya fedha na marafiki kila mara nimekuwa nataka mtu alete matokeo na si tu kuamini lomoni nyingi.
MAKOSA YA WENGINE
– kukimbilia mikopo biashara ikiwa changa na ukiwa hujalielewa soko vizuri, nimeshuhudia watu wakiingi9a katika matatzo makubwa huhu wakiwa katika hatari ya kupoteza mali zao walizo ziweka kama dhamana.
Kujidanganya mwenyewe,
Hili ni jambo rahisi sana kutokea kwa binadam hasa pale ambapo unapokuwa unaishi katika taswira kichwani na kujiambia mambo bila kuangalia uhalisia mwisho wa siku unafanya maamuzi makubwa ya maisha kwa fcts zisizo sahihi mwho wake ni majuto, “BE HUMBLE YOU MIGHT BE WRONG’
LikeLike
Asante Deodatus.
LikeLike
Baadhi ya makosa yangu; Kuajili ndugu kwa lengo kuwasaidia, Kutokuwa na follow na Tabia na utendaji kz wa niliowapa kz, Kutofuata vision na mission. Kuwa Malengo ma dogo na ya kawaida, Kupenda kula good time, Kutokufuata bajeti
Baadhi ya makosa ya wengine. Kuanzisha biashara kwa kuiga by 100%, Kusema uongo usio na tija, Kufanya mapenzi wafanyakazi, Ulevi uliopindukia
LikeLike
Asante Faraji kwa kushirikisha haya.
LikeLike
Makosa yangu
Kushindwa kufocus kwenye kitu kimoja kwa muda mrefu, Hali hiyo imenifanya mpaka sasa pamoja na kuwa na kipato kutokuwa na kitu kikubwa nilichokijenga. Kwa sasa nmeaxhana na kuhangaika na vitu vingi.
Makosa ya wengine.
Kuishi kwa kuamini kuwa mafanikio yanapatikana kwa njia ya miujiza. Wakati ni kitu kisichowwzekana
LikeLike
Asante Samizi.
LikeLike
Makosa yangu ambayo sita kuja kuyarudia kwenye maisha yangu nikufanya biashara ya ubia na mtu mwingine kwa sababu nilifanya hivyo lakin tulishindwana na akatoweka nahela zangu million 2500,000 na mbaka leo hii sijui alipopotelea,
LikeLike
Asante Emanuel
LikeLike
Kosa kubwa ambalo sitaki kurudia ni kuamini msaidizi na kutofuatilia hesabu za fedha.
Ilinigharimu na kupoteza fedha za biashara.
LikeLike
Asante Lusewa kwa kushirikisha hili.
LikeLike
Makosa niliyoyafanya
1.kujali watu wengine sana hasa ndugu zangu na kuwapa kipaombele kuliko mimi nikidhani kwa kufanya hivyo wangeweza kufanya kama nilivyofanya mm lakin matokeo yake yamekuwa tofaut kabisa
2.kuwaamin ndugu na kuwapa biashara wanisaidie kusimamia lakin mwisho wakaishia kunipa hasara kubwa mno
3.kutokuwa na mategemeo kwenye kitu kimoja hasa watumishi kwa kuajiri watumishi wengi kwenye biashara yangu ili anapoondoka mmoja kazi isisimame kwa kuondoka kwake
Makosa ya wengine
1.kuishi maisha ya maigizo hasa kwa waajiriwa kwa kukopa maghari na vitu vinhine ili kuonekana wana hela ila kiuhalisia hela hawana
2.kitokuwa na elimu ya uwekezaji na kuona uwekezaji ni kitu cha kufanywa na wazee wanaokaribia kustaafu
3.kuishi maisha ya kujilinganisha na wengime badala ya kuishi maisha yako halisi
LikeLike
Asante Notbruga kwa kushirikisha haya uliyojifunza.
LikeLike