3173; Ufunguliwe au uvunje.
Rafiki yangu mpendwa,
Kama unapita mahali usiku, ambapo pana wanyama hatari na ghafla ukasikia mnyama mkali anakujia.
Ukakimbia mpaka ukakutana na nyumba, ambayo mlango umefungwa.
Unadhani ni nini utafanya ili uweze kujitoa kwenye hatari uliyopo?
Bila shaka ni utagonga huo mlango ili uweze kufunguliwa na uondokane na hatari inayokuwa inakukabili.
Na vipi kama unagonga ila hakuna anayefungua, huku mnyama mkali akizidi kukusogelea?
Hapo itabidi uvunje huo mlango na kuingia ndani.
Ukweli ni kwamba kama utagonga mlango bila kuchoka, kuna mtu ataufungua au la mlango huo utavunjika.
Lakini sivyo mambo yanavyokuwa kwa walio wengi.
Kwani wanapogonga mlango mara chache na usifunguliwe, wanaachana nao na kwenda kwenye mlango mwingine.
Na pale huo mwingine nao unakataa, wanauacha na kwenda pengine tena.
Hivyo ndivyo watu wanakuja kushtuka wamegusa vitu vingi juu juu na hakuna chochote ambacho wamezama ndani mpaka wakapata matokeo bora na ya tofauti.
Na hilo ndiyo limekuwa linawakwamisha wengi kufanikiwa.
Watu wengi wamekuwa wanaona kwamba hawafanikiwi kwa sababu mambo ni magumu.
Lakini ukweli ni kwamba hawafanikiwi kwa sahahu wanakata tamaa haraka.
Hawajitoi vya kutosha na kwa muda mrefu.
Hawadhamirii kwenye kitu kimoja mpaka watakapopata kile wanachotaka.
Mwenendo wa wengi ni kama mvua, matone mengi yaliyosambaa kwenye eneo kubwa, ambayo yanaishia kulowesha.
Lakini kama tone moja litadondoka kwenye mwamba kwa kujirudia rudia, mwamba huo utavunjika.
Kama umechagua kuweka nguvu mahali, jitoe hasa kuhakikisha nguvu hizo unaziweka kwa msimamo na kwa muda mrefu mpaka zizalishe matokeo ya tofauti.
Kama hujapata matokeo unayotaka, siyo kwa sababu matokeo hayo hayawezekani, bali kwa sababu hujayapambania vya kutosha.
Mapambano ni mpaka upate kile unachotaka na siyo chini ya hapo.
Mapambano ni kufanya kila kinachopaswa kufanyika na siyo tu kufanya kilicho ndani ya uwezo wako.
Wakati mwingine watu wanashindwa kwa sababu hawana hatari kubwa ambayo inawakabili kama watashindwa.
Kwa maneno mengine watu wanakuwa kwenye eneo la faraja kwao, ambalo halina hatari yoyote kwao.
Ndiyo maana wanakuwa na anasa ya kuhama kutoka eneo moja kwenda jingine.
Unapokuwa unakabiliwa na hatari kubwa, utajitoa hasa kwenye kile ambacho ndiyo ukombozi wa hatari hiyo kwako.
Kama umeshajigundua umekuwa mtu wa kuhangaika na mambo mengi kwa juu juu bila kuzama ndani na kupata matokeo makubwa na ya tofauti, unapaswa kujiweka kwenye hatari itakayokulazimisha ukae kwenye jambo moja kwa muda mrefu mpaka upate matokeo unayoyataka.
Unapojitoa kweli kweli ili ukipate kitu, ni lazima utakipata.
Dunia haiwezi kumzuia mtu aliyedhamiria hasa kupata kile anachokitaka.
Hakikisha unapata kile unachotaka kwa kuweka dhamira ya kweli na kujiweka kwenye hatari ambayo huwezi kutoroka.
Hakuna njia nyingine ya uhakika zaidi ya hiyo.
Gonga mlango mpaka ufunguliwe.
Na usipofunguliwa kabisa, uvunje.
Unachotaka ni kuingia ndani.
Hakuna kinachopaswa kukuzuia.
#NidhamuUadilifuKujituma
#AfyaUtajiriHekima
#KaziUpendoHuduma
#UpekeeUdadisiUbunifu
#UshirikianoUtegemeanoUwajibikaji
#BilioneaMafunzoni
#NajengaBiashara
#HakunaKingineMuhimu
#LazimaNitoboe
#NawekaKaziNifanikiwe
Mapambano ni mpaka upate kile unachotaka na sio chini ya hapo. Mapambano ni kufanya kila kinachopaswa kufanyika na sio tu kufanya kilicho ndani ya uwezo wako.
LikeLike
Ndiyo.
LikeLike
Dunia haiwezi kumzuia mtu aliyedhamiria hasa kupata kile anachokitaka.
Gonga mlango mpaka ufunguliwe.
Asante sana Kocha Dr Makirita Amani.
LikeLike
Hakika, na usipofunguliwa basi hakikisha unavunjika.
LikeLike
Asante kocha,Kufanya kitu kimoja kwa msimamo bila kuacha lazima tupate matokeo.na matokeo yanapatikana kwa kukaa kwenye mchakato.
LikeLike
Karibu.
LikeLike
Gonga mlango ufunguliwe,na usipofunguliwa kabiy,uvunje, unachotaka ni kuingia ndani, hakuna kinachopaswa kukuzuiae.
Naamu hakuna kinachopaswa kunizuia ktk safari ya mafanikio, katika safari ya biashara,ni kuvunja kila kizuizi.muhimu ni kuupata ushindi ktk mafanikio ninayoyahitaji.
Asante!!!
LikeLike
Safi sana na kila la kheri.
LikeLike
Gonga mlango hadi ufunguke usipofunguka vunja na uingie nsani
Kwenye mafanikio hakuna kukimbia changamoto ji kukabiliana nazo na kupata njia ya kufikia mafanikio hayo tupambane haddi kupata mafanikio yetu
LikeLike
Hakika.
LikeLike
Pambana kwa nguvu zako zote mpaka upate mafanikio.
Usihangsike na mambo mengi.
LikeLike
Ndiyo.
LikeLike
Ahsante sana kocha, Dunia haiwezi kumzuia mtu aliyedhamiria hasa kupata kile anachokitaka. Nimeamua na naamini nitayapata mafanikiko
LikeLike
Kila la kheri.
LikeLike
Nitakaa kwenye biashara ninayofanya kwa muda mrefu mpaka nitakapopata matokeo ninayotaka.
Asante.
LikeLike
Kila la kheri.
LikeLike
ASANTE SANA KOCHA. Ni kugonga mlango mpaka ufunguke na hakuna kingine
LikeLike
Hakika, ni labda mtu aufungue au tuuvunje, lakini lazima ufunguke.
LikeLike
Ni labda wafungue au nivunje na kuingia ndani.Nitaendelea kupambania kombe hadi kieleweke kwa kukaa kwenye mchakato hadi mwisho.
LikeLike
Kila la kheri.
LikeLike
Lazima nikazane na kitu kimoja mupaka nipate ninacho taka
LikeLike
Safi sana.
LikeLike
Ng’an’gana na mlango mpaka ufunguke
Asante sana
LikeLike
Hakuna namna
LikeLike
Nia na sababu ya mafanikio ninayo, kazi yangu ni kuzama ndani; ama kwa kufunguliwa mlango au kuuvunja mlango.
LikeLike
Ndiyo
LikeLike
Asante sana kicha Dunia haiwezi kumzuia mtu aliyedhamiria hasa kupata kile anachokitaka.
LikeLike
Hakika
LikeLike
Kugonga mlango ni sawa na kupambana
Nitapambana mpaka nipate na nitafanya kila kinachopaswa kufanyika na sio tu kufanya kilicho ndani ya uwezo wangu. (Nitagonga mlango na nisipofunguliwa basi nitauvunja)
LikeLike
Safi sana.
LikeLike
Asante sana kocha nipo tayari kugonga huu mlango mpaka ufunguke na kama hautofunguka nitauvunja niweze kuondokana na mnyama mkali umasikini. Asante sana.
LikeLike
Safi sana.
LikeLike
Unapojitoa kikweli kweli ili ukipate kitu,ni lazima utakipate.
LikeLike
Hakika
LikeLike
Mlango wangu ni billionea mafunzoni, bitagonga mapaka ufunguliwe au uvunjike kwa vyovyote lazima niiingie ndani.
LikeLike
Safi sana, pambania hilo.
LikeLike
Nitapambana na biashara yangu ya stationery mpaka ifike juu kileleni.Sitahangaika na fursa zingine hapa katikati
LikeLike
Kila la kheri.
LikeLike
Hakikisha unapata kile unachotaka kwa kuweka dhamira ya kweli na kujiweka kwenye hatari ya kuwa huwezi kutoroka.
LikeLike
Ndiyo
LikeLike
Mapambano ni kufanya kila kinachopaswa kufanyika na siyo tu kufanya kilicho ndani ya uwezo wako.
LikeLike
Ndiyo
LikeLike