3179; Ndoto na Juhudi.
Rafiki yangu mpendwa,
Kwenye programu ya CHUO CHA MAUZO ambayo tunaiendesha, tupo kwenye ngazi ya washiriki kufundisha masomo mbalimbali ya programu hiyo.
Hivi karibuni washiriki wameshirikisha mambo waliyojifunza kwenye kijitabu kidogo nilichoandikws kinachoitwa; JINSI YA KUPATA CHOCHOTE UNACHOTAKA (A MESSAGE TO GARCIA).
Kwenye kijitabu hicho, watu wanagawanyika kwenye makundi (divisions) matano.
š„Division One; Wanafanya kitu sahihi bila kuambiwa. Hawa wanapata mafanikio makubwa sana.
š„Division Two; Wanafanya kitu baada ya kuambiwa mara moja. Hawa wanapata mafanikio ya wastani.
š„Division Three; Wanafanya kitu baada ya kuambiwa zaidi ya mara moja. Hawa wanapata mafanikio kidogo.
āļøDivision Four; Wanafanya kitu pale anapokuwa na shida/uhitaji. Hawa hawapati mafanikio kabisa.
š®Division Zero; Hawafanyi hata baada ya kuambiwa, kuonyeshwa na kusimamiwa kwa karibu. Hawa huishia pabaya.
Kwenye uwasilishaji wa somo hili, mmoja wa washiriki alienda mbali zaidi na kulinganisha makundi hayo kwa ndoto na juhudi. Kwa namna alivyopanga, inaeleza wazi kwa nini kunakuwa na tofauti ya mafanikio kwenye makundi hayo.
Mshiriki huyo aliyapangilia makundi hayo kama ifuatavyo;
š„Division One; Wana ndoto kubwa na zinazoeleweka na pia wanaweka juhudi kubwa na kwa msimamo kuziendea ndoto hizo.
š„Division Two; Wana ndoto kubwa ambazo zinaeleweka na wanaweka juhudi za wastani kuziendea ndoto hizo.
š„Division Three; Wana ndoto za kawaida na zisizoeleweka na pia wanaweka juhudi za kawaida zisizo za msimamo.
āļøDivision Four; Wana ndoto ndogo na wanaweka juhudi ndogo.
š®Division Zero; Hawana ndoto zozote na wala hawaweki juhudi zozote.
Kwa kutumia vigezo hivyo vya ndoto na juhudi, tunaona jinsi ambavyo watu wanatofautiana kwenye matokeo wanayoyapata kwenye maisha yao.
Rafiki yangu mpendwa, ni wakati mwingine wa kujitafakari kwenye hayo makundi na kujua upo kundi gani.
Kwa kundi unalosema upo, toa ushahidi kwa nini umejiweka kwenye kundi hilo.
Shirikisha hayo kwa kuandika kwenye maoni hapo chini.
Shirikisha unajiona kwenye kundi lipi na ushahidi wako ni upi unaokuweka kwenye kundi hilo.
Karibu ukamilishe hili.
#NidhamuUadilifuKujituma
#AfyaUtajiriHekima
#KaziUpendoHuduma
#UpekeeUdadisiUbunifu
#UshirikianoUtegemeanoUwajibikaji
#BilioneaMafunzoni
#NajengaBiashara
#HakunaKingineMuhimu
#LazimaNitoboe
#NawekaKaziNifanikiwe
Najiona Division One. Sababu ni mipango na mikakati niliyonayo na juhudi ambazo naendelea kuziweka. Sio mara zote nafanikiwa kutimiza yote ninayopanga lakini najitahidi kujiboresha kufikia viwango vya juu zaidi kwa mwendelezo.
LikeLike
Umesema vyema, kujitahidi kujiboresha kila wakati ili kufikia viwango vya juu zaidi. Kaa humo kwa uhakika.
LikeLike
Ndoto nilizonazo ni kubwa na naendelea kuweka juhudi kuzifikia.Nafikiri nami ni wa division one
LikeLike
Mbona unasema bila ya kujiamini?
Unapaswa kusema kifua mbele, kisha kutekeleza kweli kwa vitendo.
LikeLike
Division Two. Ninazo ndoto zinazoeleweka na ninaweka juhudi kufikia ndoto hizo. Ushahidi wangu ni ukaaji wa kwenye mchakato wa bilionea mafunzoni.
Asante.
LikeLike
Vizuri, ongeza juhudi kwenye ndoto na kwa msimamo ili uwe division one.
LikeLike
Mini najiona divion one make nina ndoto kubwa na napambania ndoto hiyo na ntaifikia na kuwa halisia
LikeLike
Sema kwa kujiamini na dhihirisha kwa matendo.
LikeLike
Najiona Division one,au kundi namba mbili,nikiwa naelekea kundi namba moja,nina ndoto na naitekeleza hata maono na ndoto Nilizonazo zinatekelezeka.
Pia nashkr maana hata jana Mimi na team yangu tulikuwa tunasoma kijitabu hiki.
LikeLike
Sawa, sema kwa kujiamini kisha dhihirisha kwa matendo.
LikeLike
Kwa sasa nipo Division two. Nina ndoto kubwa lakini juhudi zangu bado ni za wastani . Na naweka juhudi na kufanya baada ya kuambiwa kitu mara moja.
LikeLike
Sawa, ongeza zaidi juhudi ili kufika division one
LikeLike
Nipo division twoo, nitaweka juhudi zaidi ili niweze kuwa division one
LikeLike
Sawa, ongeza juhudi zaidi.
LikeLike
Nipo Division 2. Napambania kufikia Division 2 ambayo inahitajika kuweza kufikia malengo makubwa
LikeLike
Ongeza zaidi juhudi zako.
LikeLike
Asante Kocha;
Niko division one; Nina ndoto kubwa na zinazoeleweka na pia ninaweka juhudi kubwa na kwa msimamo kuziendea ndoto hizo. Ushahidi; uandishi wa makala, vitabu na utoaji mafunzo kwa watu na taasisi mbali mbali.
LikeLike
Vizuri, endelea kupambania hiyo nafasi na matokeo makubwa yatakuja.
LikeLike
Kulingana na viwango hivi kwa kuzingatia Ndoto, kabla sijajiunga na kisima cha maarifa kwa hakika nilikuwa division three, baada ya kujiunga na kisima cha maarifa na kuwa na lengo la pamoja kufikia utajiri wa dola bilioni moja najiona katika daraja la pili. Ukiachilia lengo Hili la kipato mwenendo wangu najiona nikiwa bado nipo daraja la Tatu. SASA hapa najiwasha Moto tena, kwa kupunguza kabisa Yale ninayoyafanya. Naachana na kuzurura kifikra nabaki na lengo moja kubwa, kufikia ubilionea. Napambana sana kuweza kufikia daraja la Kwanza.
LikeLike
Umefanya tafakari nzuri, sasa fanyia kazi haya maazimio yako mapya.
Na kazana usiwe mtu wa kurudi rudi nyuma kila wakati.
LikeLike
Nipo division one na ushaidi wa Hilo ni hapa nilipo sasa baada ya kuangaika sana na maisha na kushindwa sana ikafika mahali na kuamua kubadilisha mfumo wa maisha yangu, sasa habari ni tofauti sana.
Asante sana.
LikeLike
Hongera sana, endelea kung’ang’ania hapo division one.
LikeLike
Mimi najiona kuwa division two kwa sababu nafanyia kazi kitu baada ya kuambiwa Mara moja. Nina ndoto kubwa ila juhudi ninazoweka Ni za wastani. Nikitoka tu kwenye ajira nitapambania Division One!
LikeLike
Vizuri kwa kutambua ulipo.
Lakini huhitaji kusubiri mpaka utoke kwenye ajira ndiyo uwe division one, anzia hapo hapo ulipo sasa.
Tayari ndoto kubwa unazo, kilichobaki ni kuweka juhudi kubwa kabisa.
LikeLike
Asante kocha,Nipo division two,nikiwa ninamaanisha bado najifunza mambo mengi hapa kisima cha maarifa na ninatakiwa kuweka nguvu kubwa ili niwe division one.ninapambana ili nifikie malengo na uhuru wa kifedha.
LikeLike
Sawa, pambania hilo.
LikeLike
Nipo division two Nina ndoto kubwa ila juhudi ninazoweka ni za wastani, najitahidi ili nifikie jui zaidi.
LikeLike
Ongeza juhudi zaidi.
LikeLike
Najiona division two,nafanya kitu baada ya kuambiwa mara moja.
LikeLike
Nini kinakuzuia usiwe division one?
LikeLike
Najiona kwenye Divisio 1 Ila Matendo yangu ni division 2. Nataka kutoka huko nirudi kundi langu.. Kufanya kwa juhudi kubwa na bila kuacha
LikeLike
Sawa, rudi kwenye kundi sahihi.
LikeLike
Binafsi najiona nipo division two kwasababu nina ndoto kubwa lakini pia nafanya baada yakuambiwa
LikeLike
Kwa nini usiazimie kuwa division one?
LikeLike
Ninajiona division 2; Ndoto kubwa lakini juhudi za wastani sana. Sababu ni kudhani kuwa safari ya kuifikia ndoto ni kuambatana na wengine hasa familia. Kumbe mitazamo ni tofauti, hivyo hapa ni kutimiza wajibu wako inavyohitajika. Ndoto ni yako na kuifikia ni jukumu lako kwa kuwa na timu imara na waielewe ndoto yako kwa ufasaha.
LikeLike
Pambana kuongeza juhudi ili kufika division one.
LikeLike
Division two nnazo ndoto zinazoeleweka Na ninaweka juhudi kuzifiki ndoto hizo ushahidi ni jinsi ninavyokaa kwenye mchakato
LikeLike
Sawa, pambana ufike division one.
LikeLike
Division two. niweza kumiliki biashara zaidi ya miaka 10 pamoja kupitia mengi,kufanya mengi na kufeli,
Sasa nafanya kitu kimoja tu kujenga kampuni mpaka niwe division one.
LikeLike
Tekeleza.
LikeLike