3179; Ndoto na Juhudi.

Rafiki yangu mpendwa,
Kwenye programu ya CHUO CHA MAUZO ambayo tunaiendesha, tupo kwenye ngazi ya washiriki kufundisha masomo mbalimbali ya programu hiyo.

Hivi karibuni washiriki wameshirikisha mambo waliyojifunza kwenye kijitabu kidogo nilichoandikws kinachoitwa; JINSI YA KUPATA CHOCHOTE UNACHOTAKA (A MESSAGE TO GARCIA).

Kwenye kijitabu hicho, watu wanagawanyika kwenye makundi (divisions) matano.

šŸ„‡Division One; Wanafanya kitu sahihi bila kuambiwa. Hawa wanapata mafanikio makubwa sana.

🄈Division Two; Wanafanya kitu baada ya kuambiwa mara moja. Hawa wanapata mafanikio ya wastani.

šŸ„‰Division Three; Wanafanya kitu baada ya kuambiwa zaidi ya mara moja. Hawa wanapata mafanikio kidogo.

āŒļøDivision Four; Wanafanya kitu pale anapokuwa na shida/uhitaji. Hawa hawapati mafanikio kabisa.

🚮Division Zero; Hawafanyi hata baada ya kuambiwa, kuonyeshwa na kusimamiwa kwa karibu. Hawa huishia pabaya.

Kwenye uwasilishaji wa somo hili, mmoja wa washiriki alienda mbali zaidi na kulinganisha makundi hayo kwa ndoto na juhudi. Kwa namna alivyopanga, inaeleza wazi kwa nini kunakuwa na tofauti ya mafanikio kwenye makundi hayo.

Mshiriki huyo aliyapangilia makundi hayo kama ifuatavyo;
šŸ„‡Division One; Wana ndoto kubwa na zinazoeleweka na pia wanaweka juhudi kubwa na kwa msimamo kuziendea ndoto hizo.

🄈Division Two; Wana ndoto kubwa ambazo zinaeleweka na wanaweka juhudi za wastani kuziendea ndoto hizo.

šŸ„‰Division Three; Wana ndoto za kawaida na zisizoeleweka na pia wanaweka juhudi za kawaida zisizo za msimamo.

āŒļøDivision Four; Wana ndoto ndogo na wanaweka juhudi ndogo.

🚮Division Zero; Hawana ndoto zozote na wala hawaweki juhudi zozote.

Kwa kutumia vigezo hivyo vya ndoto na juhudi, tunaona jinsi ambavyo watu wanatofautiana kwenye matokeo wanayoyapata kwenye maisha yao.

Rafiki yangu mpendwa, ni wakati mwingine wa kujitafakari kwenye hayo makundi na kujua upo kundi gani.
Kwa kundi unalosema upo, toa ushahidi kwa nini umejiweka kwenye kundi hilo.
Shirikisha hayo kwa kuandika kwenye maoni hapo chini.
Shirikisha unajiona kwenye kundi lipi na ushahidi wako ni upi unaokuweka kwenye kundi hilo.
Karibu ukamilishe hili.

#NidhamuUadilifuKujituma
#AfyaUtajiriHekima
#KaziUpendoHuduma
#UpekeeUdadisiUbunifu
#UshirikianoUtegemeanoUwajibikaji
#BilioneaMafunzoni
#NajengaBiashara
#HakunaKingineMuhimu
#LazimaNitoboe
#NawekaKaziNifanikiwe