3180; Sitaki upate amani.
Rafiki yangu mpendwa,
Siku za karibuni nilikuwa nampigia mmoja wetu hapa simu.
Akaniambia nikiona simu yako nakosa amani.
Nikamwambia hivyo ni vizuri kabisa, kwa sababu hicho ni kiashiria kwamba programu inafanya kazi.
Japokuwa jina langu ni Amani, hicho ndiyo kitu ambacho sitataka ukipate kabisa.
Kwa sababu kupitia kujifunza kwa usomaji na hata kwa baadhi ya watu ambao wamepita kwenye hizi programu na kupotea, nimeona mlolongo ambao umekuwa unajirudia.
Mtu anaanza akiwa chini kabisa, anakuwa na msukumo mkubwa wa kujifunza. Anazingatia mafunzo yote na kuyafanyia kazi kwa uhakika.
Msukumo huo mkubwa wa kujifunza unawafanya waanze kupata ushindi. Kwa ushindi huo wanatoka chini walipokuwa na kuanza kupanda juu.
Ushindi wanaoanza kupata, unawafanya wawe na mazoea. Wanaona wameshajua kila kitu na hawahitaji tena kujifunza, au hakuna kipya cha kujifunza.
Hata uchukuaji wa hatua unabadilika, hawachukui tena kwa msukumo mkubwa, bali kwa mazoea.
Sifa wanazokuwa wanapata zinawapanda kichwani, kichwa kinakuwa kikubwa na hakisikilizi tena.
Mazoea na ujuaji vinapelekea mtu kushindwa na kujikuta anarudi kule alikotoka.
Pamoja na yeye mwenyewe kuwa amechangia kwenye hatua hiyo, bado hatakubali kwamba amekuwa na mchango.
Bali atatafuta sababu za kumfurahisha kwa nini ameshindwa.
Na hapo mwendo anakuwa ameumaliza.
Mfumo wa programu yetu wa kuhakikisha hupati amani mara zote ni wa kuanza na lengo kubwa. Kisha kupambana kwa kila namba kulifikia.
Kabla hujalifikia lengo hakuna kitu umefanya, hivyo unakuwa na msukumo mkubwa wa kulipambania.
Ukilifikia lengo tu, unapata pongezi, halafu hapo hapo lengo unalikuza mara mbili na hilo kuwa ndiyo lengo lako jipya.
Unarudi tena kwenye msukumo wa kufikia lengo kwa sababu unaona bado kuna kitu hujafikia.
Kama unajiuliza mwisho wa hili ni lini, kuna habari mbili;
Moja lengo tulilonalo ni kubwa, hivyo mapambano yake lazima yawe makubwa sana.
Mbili, hilo halitakuwa na mwisho, kwa sababu tunajua kwenye maisha kuna kwenda mbele au kurudi nyuma, hakuna kusimama.
Ukisimama, wakati dunia inaenda mbele, unakuwa unarudi nyuma.
Hivyo inabidi ukimbie mara mbili ili uende zaidi ya pale ulipo.
Hivyo basi, kwenye hii safari, sahau kuhusu amani. Amani utaipata ukifa.
Niliona kauli mahali inauliza kwa nini watu wakifa wanaambiwa wapumzike kwa amani (Rest In Peace) badala ya walio hai kuambiwa wakae kwa amani (Stay In Peace).
Na nadhani jibu lipo wazi, dunia haina amani, amani pekee utaipata ukifa.
Mpaka utakapofika huo wakati, ni kuendelea na mahangaiko bila amani.
#NidhamuUadilifuKujituma
#AfyaUtajiriHekima
#KaziUpendoHuduma
#UpekeeUdadisiUbunifu
#UshirikianoUtegemeanoUwajibikaji
#BilioneaMafunzoni
#NajengaBiashara
#HakunaKingineMuhimu
#LazimaNitoboe
#NawekaKaziNifanikiwe
Kusimama wakati dunia inaenda mbele ni kurudi nyuma, hivyo kwenye safari ya mafanikio inabidi kusahau kuhusu amani. Amani inapatikana baada ya kifo.
LikeLike
Mwendo ni rest in peace, vinginevyo ni fujo tu.
LikeLike
Ni mpambano mkali kuelekea kwenye lengo kubwa na hakuna amani hadi tutakapokufa ndiyo kuna neno rest in peace ukiwa hai mapambano
LikeLike
Mapambano hayapoi, adui anabadili mbinu kila mara, ukipumzika, umeisha.
LikeLike
Asante sana ni hakika umenena vyema kabisa na hii ndio dhana kubwa kwenye kile ambacho sisi tunakipambania.
LikeLike
Ndiyo.
LikeLike
Kusimamia ni kurudia nyuma na hakuna Amani mpaka kufaa maana dunia haina huruma na ikisimama unarudi kule ulikotoka.
LikeLike
Adui anabadili mbinu kila wakati, tukilegeza tu tumempa ushindi.
LikeLike
Asante sana kocha,acha tu niendelee kupambana bila kujipanga ya kwa kutumia kauli ya wanajeshi:piga kazi kama da ukifa utapumzika,nawezaje kupumzika nikiwa hai wakati dunia yenyewe haina Amani wala sina nilichonacho.
LikeLike
Utapumzika ukifa, tofauti na hapo ni mapambano.
LikeLike
Asante sana Kocha.
LikeLike
Karibu
LikeLike
Asante sana kocha kwa kurasa huu ambao inatufanya kuwa bora na kutoridhika hovyo na kujiona umefika, kuna mtu niliwahi kukutana nae miaka 2 iliyopita aliniambia alinunua hisa 100000 kwa mara moja na haendelei tena kununua mara kwa mara , kipindi hicho nilikua nina hisa chini ya 10000 za CRDB kwa hatua ndogo ambazo nikichukua, lakini ulivyoanzisha zidisha kwa 2 malengo imenipa nguvu ya kufika na kuvuka hisa 100000 bila mashaka yoyote Asante sana
LikeLike
Safi sana, ni mwendelezo, hakuna kusimama.
LikeLike
Hovyo basi, kwenye hii safari saharanpur amani.
LikeLike
Amani ni kujipoteza.
LikeLike
Duniani mchakamchaka amani baada ya kifo
Asante sana
LikeLike
Huu mchaka mchaka haupoi.
LikeLike
Duani hakuna amani amani utaipata mpaka ukifa
LikeLike
Hakika
LikeLike
Ni kweli kabisa mwisho wa vita ni kifo tu
LikeLike
Ndiyo, kama bado hujafa, mapambano yanaendelea.
LikeLike
Hapa Ni kupambana na kufikia lengo na kujipongeza na kuzidisha lengo Mara mbili na kupambana tena. Kwa mtindo huu najikosesha amani. Amani nitaipata nikifaaaa!
LikeLike
Kabisa, amani ukiwa hai ni kutafuta matatizo.
LikeLike
Dah hili ni andiko Bora Sana hakika.
Ushahidi unaonyesha AMANI inaendana na vitu Kama
Mazoea
Uzembe
Uvivu
Ambavyo ni chanzo Cha Umasikini. Hapa ninapofanya kazi watu hawapendi Presha, mabadiriko Wala kutimiza wajibu. Napenda presha kwa Sasa nitapata amani NIKIFA
LikeLike
Presha ndiyo inageuza mkaa kuwa almasi, tuipende.
LikeLike
Hili limenifikirisha sana. Kama sehemu sahihi ya kupumzika ni baada ya kifo! basi ninakosea sana kuanza kupumzika hapa duniani. Kuanzia sasa ni mchakamchaka mwanzo mwisho hakuna kupoa.
LikeLike
Safi sana.
LikeLike
Amani ni chanzo cha kifo katika mafanikio
LikeLike
Ndiyo
LikeLike
“dunia haina amani, amani pekee utaipata ukifa.
Mpaka utakapofika huo wakati, ni kuendelea na mahangaiko bila amani.”
LikeLike
Ndiyo
LikeLike
Kwenye haya maisha ukiona hauna mtu ambaye ukiona calls yake haukosi amani jua umeshapotea,,,lazima uwe na mtu anaekuwajibisha vinginevyo umepotea ukiwa na amani
LikeLike
Uwajibikaji ni muhimu sana ili tuweze kupiga hatua.
LikeLike