3185; Mateso unayoyafurahia.
Rafiki yangu mpendwa,
Huwa kuna kauli inayosema watu waliofanikiwa wanakuwa wamefanya vitu ambavyo wasiofanikiwa hawapendi kuvifanya. Pia ni vitu ambavyo wao wenyewe hawapendi kuvifanya, ila wanakuwa hawana namna bali kuvifanya.
Ukweli ni kwamba huwezi kupata mafanikio makubwa kwa kufanya yale ambayo kila mtu anayafanya, tena kwa namna ambavyo anayafanya.
Kile ambacho kinafanywa na wengi huwa hakina mafanikio makubwa.
Ukiwaangalia watu wote walioweza kujenga mafanikio makubwa kwenye maisha yao, kuna namna wanakuwa wamepata mateso wanayoyafurahia.
Kuna vitu wanavyokuwa wanafanya kwa mapenzi makubwa, licha ya kuwa ni vitu ambavyo ni mateso kwa kila mtu.
Mateso ya vitu hivyo yanaweza kutokana na ugumu wa kitu au uchoshi wake.
Vitu vigumu ni vile ambavyo mtu anakuwa anavifanya kwa mara ya kwanza hivyo anakosea kuvifanya. Wengi hukata tamaa na kuacha kufanya. Lakini wanaofanikiwa sana huwa wanaendelea kufanya bila kuacha.
Vitu vyenye uchoshi ni vile ambavyo ni vya kawaida kabisa ila inabidi virudiwe rudiwe kufanywa kwa msimamo kila kuacha. Ni katika kurudia rudia huko kufanya ndiyo matokeo makubwa na mazuri yanazalishwa.
Walio wengi huwa wanapenda kufanya vitu vinavyowapa msisimko kila wakati kutokana na upya wake au mvuto wake kwa nje.
Lakini vitu vyenye mafanikio makubwa ni vile vya kawaida kabisa ambapo inabidi virudiwe rudiwe kufanywa kwa muda mrefu bila kuachwa.
Wasiofanikiwa huwa ni rahisi kuyumbishwa na vitu vipya na vya kusisimua vinavyowajia kila wakati.
Na huko kuyumbishwa kirahisi ndiyo kunakuwa kikwazo kwao kufanikiwa kwa kiasi kikubwa.
Wasiofanikiwa huwa wanatamani sana kuyaona maisha ya waliofanikiwa kwa undani, wakiamini kuna siri fulani wanakuwa nazo.
Lakini pale wanapopata nafasi ya kuyaangalia maisha ya waliofanikiwa kwa karibu ndivyo wanavyojionea hakuna jipya.
Wanashangaa jinsi ambavyo wale waliofanikiwa kuliko wao wanavyofurahia kufanya mambo ambayo wao hawataki hata kuyaona.
Unajua kabisa kwamba unachotaka ni mafanikio makubwa.
Na unajua ili kuyapata ni lazima ufanye vitu ambavyo unaweza usiwe unapenda kufanya.
Lakini inabidi uvifanye, iwe unapenda au hupendi, unajisikia kufanya au hujisikii.
Baraka kubwa kabisa kwenye maisha ni kupata mateso ambayo unafurahia kuyafanya.
Ukiweza kufanya kitu licha ya kwamba kinakutesa, unakuwa umewazidi wengine wengi ambao wanaacha kufanya kwa sababu wameshindwa kuyavumia mateso yaliyopo kwenye kitu hicho.
Unapaswa kuujua mchakato wa msingi kabisa unaopaswa kuutekeleza kila siku bila ya kuacha na kisha kuutekeleza kweli.
Ni msimamo wako kwenye utekelezaji wa mchakato wa msingi kila siku bila kuacha ndiyo unaokupa mafanikio makubwa.
Kitu kimoja tunachoendelea kukiona ni jinsi ambavyo mafanikio na mateso haviwezi kutengana.
Na hapo pia tunaona jinsi ambavyo wale wanaofanikiwa sana kuna namna akili zao zinakuwa za tofauti na ambao hawafanikiwi.
Kwa sababu ni mtu wa aina gani ambaye atakuwa tayari kuyafurahia mateso?
Kwa hakika lazima awe mtu wa ajabu, kwa vipimo vya kawaida na kulinganisha na wengine.
Kwenye safari ya mafanikio makubwa hufanyi kwa kuangalia wengine au unajisikiaje wewe.
Bali unafanya kwa kuziangalia namba zinakuletea matokeo gani.
Unaenda ukiboresha yale yanayokuletea matokeo unayoyataka.
Na hivyo ndivyo watu wanavyoweza kupiga hatua kubwa kwenye maisha yao.
Namba hazijali sana wewe unajisikiaje au unataka nini.
Bali zinatokana na juhudi zinazokuwa zimewekwa.
Kwa juhudi kuongezwa, namba nazo zinakuwa bora zaidi.
Ni mateso gani ambayo wewe unafurahia kuyafanya?
Vitu gani ambavyo wengine wanakwepa kuvifanya ila wewe upo tayari kuvifanya mara zote?
Karibu ushirikishe kwenye maoni hapo chini.
#NidhamuUadilifuKujituma
#AfyaUtajiriHekima
#KaziUpendoHuduma
#UpekeeUdadisiUbunifu
#UshirikianoUtegemeanoUwajibikaji
#BilioneaMafunzoni
#NajengaBiashara
#HakunaKingineMuhimu
#LazimaNitoboe
#NawekaKaziNifanikiwe
Mateso ambayo mimi navumulia kuyafanya ni kuweka akiba na kuwekeza pia mambo ambayo wengine wanakwepa kufanya na mimi nafanya ni kuishi kwa nidhamu kubwa katika kile ambacho nakifanya..
LikeLike
Vizuri, endelea hivyo.
LikeLike
Mateso ninayoyafurahia ni kufanya kazi muda wote na kuondokana na vitu vinavyonipa furaha ya muda mfupi.
Vitu ambavyo wengine wanakwepa kuvifanya lakini mimi niko tayari kuvifanya ni pamoja na kutojali wengine wanasemaje, kuzishinda hofu, kutofuata mkumbo na kufanya maamuzi sahihi hata ikiwa ni maamuzi magumu.
LikeLike
Safi sana, simama humo.
LikeLike
ahsante kocha
mateso ninayofurahia
ni kuamka mapema na kuianza siku yangu
kupiga simu kwa wateja na kujenga mahusiano nao
LikeLike
Vizuri, usiache hayo.
LikeLike
Mafanikio na mateso ni mapacha huwezi kuvitenganisha.
Asante sana
LikeLike
Kabisa
LikeLike
Ni kuamka asubuhi ndiyo kubwa kabisa ambalo sikua naamka na wote hapo nyumbani wanaona ni mateso sana kwangu huku mimi baada ya kuzoea nayafurahia sana
Pia kujifunza kile ambacho ulikua nacho miaka mingi mkifanya na wengine kwa mazoea sasa wanaona unateseka kujifunza wakati mambo ni yaleyale kumbe wao hawajui ninachofurahia kwa sasa kwa maarifa haya nawaacha mbali sana
Lingine ni kutoka wafanyabiashara wengi hawatoki nje ya biashara zao kuona wengine wanafanyaje lakini kukutana nao wao wanaona kulala nje ya nyumbani na mbali na biashara ni mateso kumbe ni raha saana
LikeLike
Safi sana kufurahia haya muhimu ambayo kwa wengine ni mateso makubwa.
LikeLike
Kitu kinachonipa furaha ni pesa. Ili kuipata inabidi niweke thamani, maarifa na mda. Kutafuta na kujenga wateja wa biashara ndiyo jukumu langu kubwa.
Napenda Sana kuuza na kushawishi wengine kununua
Sintajali wengine wanasemaje kuhusu Mchakato wangu
LikeLike
Vizuri sana.
LikeLike
Mateso ambayo mimi nayafurahia kuyafanya ni kuamka mapema asubuhi na kuendelea na ratiba zangu za siku na vitu ambavyo wengine wanakwepa kuvifanya na mimi nipo tayari kuvifanya mara zote ni kutembelea wateja na kuwasiliana na wateja
LikeLike
Vizuri, endelea.
LikeLike
Kitu ambacho ninavumilia, ninafanya hata kama sijisikii vyema ni kulala na kuamka mapema
LikeLike
Safi
LikeLike
Mateso ninayofurahia ni kuamka mapema,kujifunza,kutoa elimu,kupiga simu,kufanya kazi masaa mengi zaidi.
LikeLike
Vizuri
LikeLike
Mwanzo tunafanya vitu kwa shauku na kwa msisimko mkubwa, linapokuja swala la consistency hapa ndipo jasho na damu huja, na siku moja ukiacha ni mlango wa kuharibu mchakato wa ubilionea.
Ubilionea upo katika ung’ang’anizi
Nadumu katika mchakato kwa ung’ang’anizi.
LikeLike
Umesema vyema, ung’ang’anizi ni muhimu sana.
LikeLike
Mateso ambayo naendelea kuyafanya ni kufanya uwekezaji UTT kwa msimamo bila Kuacha.
Pia nimeamuamua kufanya biashara bila ya kukata tamaa mpaka niweze kuwa Bilionea
LikeLike
Safi sana, kila la kheri.
LikeLike
Kukaa kwenye mchakato na kufanya Yale yote yanayotakiwa kufanywa bila kuleta sababu
Hayo ni mateso lakini inabidi tufanya hakuna namna
Asante sana
LikeLike
Hakika
LikeLike
Mateso ambayo nafurahia kuyafanya;-
1. Kuamka asubuhi saa kumi – kitu ambacho sikuwahi kuamini kuwa nitaweza maishani.
2. Mchezo wa namba za biashara na binafsi na mchakato mzima wa mauzo
3. kuweka akiba na kuwekeza UTT, Bank na kwenye Hati fungani za serikali
4. Kuwa chini ya usimamizi wa kocha katika mambo yahusuyo fedha, biashara na uwekezaji
Asante sana
LikeLike
Vizuri sana, endelea kwa msimamo.
LikeLike
Asante kocha,Mambo ambayo yananitesa sana ni kukaa masikini,hivyo lazima nikae kwenye mchakato ili niwe tajiri.
LikeLike
Kila la kheri.
LikeLike
Mateso ninayoyafurahia
-Kuamka asubui mapema
-Kuchelewa lufunga ofisi
-Kukosa baadhi ya burudani
-Kutoeleweka na jamii
LikeLike
Upo kwenye njia sahihi.
Kuwa na msimamo.
LikeLike
.Kuonekana Nina roho mbaya
2.Kutokujali wengine wanasema nini
3.Taking risk
4.kujifunza endelevu, nimechagua kujifunza siku zote nitakazokuwa hai hapa duniani
5.Maamuzi Magumu.
6.Kuwa na malengo makubwa sana
LikeLike
Mateso ninayo furahia nikufanya ni kufanya KAZI kutokujali wengine wanasema nini
LikeLike
Vizuri sana.
LikeLike
Mateso ninayoyafurahia.
Ratiba yangu ya siku ninayokuwa nayo ambayo so ruhusu mtu kuingilia kuanzia familia na watu wengine ninaojihusisha nao.hapa nipo tayari kukosana na kila mtu lakini ratiba yangu iende kama nilivyoipangilia.Asante.
LikeLike
Safi sana, msimamo ni muhimu ili kutekeleza uliyopanga.
LikeLike