3190; Unachokosea kwenye msimamo.
Rafiki yangu mpendwa,
Moja ya vitu ambavyo tumekuwa tunasisitizana sana kwenye hii safari yetu ya mafanikio makubwa ni msimamo.
Ambapo ni kufanya bila ya kuacha, liwake jua au inyeshe mvua.
Bila ya kufanya jambo kwa msimamo bila ya kuacha, huwezi kupata mafanikio makubwa.
Wapo watu wanasikia hili la msimamo na kuona ni rahisi, wanaona kurudia rudia tu kufanya siyo kitu kinachoweza kuwashinda.
Na hivyo wanarudia rudia kufanya kitu mara zote.
Halafu wanashangaa kwa nini hawapati mafanikio makubwa wanayotaka.
Hawa wanakuwa wanafanya kosa moja kubwa ambalo Albert Einstein aliliita ujinga. Ambapo alisema; ujinga ni kufanya jambo lile lile, kwa namna ile ile halafu kutegemea matokeo ya tofauti.
Wanachokosea watu wengi kwenye msimamo ni kurudia rudia tu kitu kwa namna ile ile bila kuacha.
Huo siyo msimamo ambao utakufikisha kwenye mafanikio makubwa unayoyataka.
Msimamo unaohitajika kwenye safari ya mafanikio ni kutokuacha, yaani kuendelea kufanya.
Lakini inapokuja kwenye ufanyaji wenyewe, huwezi kuwa unafanya vile vile.
Badala yake unapaswa kuwa unaenda ukiboresha kile unachofanya.
Hilo linafanya mrejesho kuwa muhimu sana kwenye ufanyaji. Kila unapofanya, unapaswa kujitathmini kisha kuona namna gani unapaswa kuboresha zaidi.
Hupaswi kufanya leo kwa sababu jana ulifanya.
Unapaswa kufanya kwa namna bora zaidi, kulingana na tathmini uliyoifanya na mrejesho uliopata wa moja kwa moja au usio wa moja kwa moja.
Kama kurudia rudia kufanya pekee ingekuwa ndiyo mafanikio, kila anayejua kuendesha gari angeweza kushinda mashindano ya magari, kwa sababu anaendesha kila siku.
Au kila anayekimbia kila siku angeshinda mashindano ya mbio.
Lakini hivyo sivyo inavyokuwa, kwa sababu wengi wanaofanya jambo kila siku bila kuacha, wanafanya kwa mazoea, bila hata ya kufikiria.
Mafanikio makubwa yanataka urudie rudie kufanya jambo kwa muda mrefu bila kuacha, ila kwa kuboresha kwenye kila ufanyaji.
Unaanza kwa hatua ndogo na kujitathmini, kisha kufanya maboresho zaidi.
Halafu unaendelea hivyo bila kuacha, kufanya kwa kuboresha na kurudia.
Ili uboreshe kila hatua unayochukua unahitaji vitu viwili;
Cha kwanza ni kujitathmini kwa kila matokeo unayopata kisha kuangalia wapi pa kuboresha ili matokeo yawe mazuri zaidi.
Cha pili ni kupata mrejesho kutoka kwa wengine kuhusu ufanyaji wako.
Mrejesho wa wengine unaweza kuwa wa aina mbili;
Aina ya kwanza ni mrejesho wa moja kwa moja, ambapo watu wenye uelewa kwenye jambo hilo wanakuambia maeneo gani uboreshe.
Aina ya pili ni mrejesho usio wa moja kwa moja, ambapo jinsi watu wanavyopokea kile unachofanya unajua kama umefanya kwa usahihi au la. Mapokezi yanapokuwa mazuri unajua umefanya vizuri na kuendelea na kile kinachofanya kazi. Na kama mapokezi hayatakuwa mazuri, unajua kuna kitu hujafanya sawa hivyo kuhitaji kuboresha zaidi.
Kwa kujitathmini mwenyewe na kupokea mrejesho wa wengine kisha kuboresha zaidi na kuendelea kufanya ndiyo utaweza kupata matokeo bora kabisa.
Ubaya ni pale unapoacha kabisa kufanya kwa sababu ukijitathimini unaona matokeo unayopata ni ya chini sana kuliko ulivyotegemea.
Au pale mrejesho wa wengine unapokuwa siyo mzuri na wewe kuishia kukata tamaa na kuacha kabisa kufanya.
Kurudia tu kufanya siyo msimamo utakaokupa mafanikio makubwa.
Bali kurudia kufanya huku ukiwa unaboresha kadiri unavyokwenda.
Kwenye mauzo kuna vitu vingi sana ambavyo watu huwa wanafanya kwa kurudia rudia bila kuacha na bado hawapati mafanikio makubwa.
Mfano upigaji wa simu, mtu anaweza kuwa anapiga simu nyingi sana kwa wateja, lakini mauzo yake yakawa chini.
Atakuwa na msimamo kwenye kufanya bila kuacha, lakini hakuna hatua ambazo anapiga.
Hiyo inakuwa ni kwa sababu hajifanyii tathmini kwenye simu anazopiga na kuona ni wapi pa kuboresha kwenye hilo zoezi ili kupata matokeo mazuri.
Yeye anapiga tu simu ili kukamilisha idadi, lakini anachoongea kwenye simu zake ni kile kile.
Harekodi simu zake na kumwomba mwenye uelewa zaidi wa mauzo azisikilize na kumpa mrejesho wa namna gani aboreshe zaidi zoezi lake la upigaji simu.
Pale wateja wote anaowapigia simu wanapompa sababu rahisi za kutokununua, kama vile uchumi ni mbaya au wakiwa tayari watamtafuta, yeye anakubaliana nao kirahisi. Anaendelea kupiga simu na kupewa sababu hizo hizo, ambazo anaendelea kuzipokea.
Mwisho wa siku anakuwa amepiga simu kwa msimamo, lakini hauzi kwa ukubwa kama ilivyotegemewa.
Kadhalika kwenye michakato mingine ya mauzo kama kutembelea, kufuatilia, kuomba mauzo ya ziada na rufaa.
Kama hupati matokeo unayotaka, licha ya kufanya kwa msimamo bila kuacha, basi jua unakosea.
Unachokosea ni unarudia kitu kile kile mara zote, badala ya kufanya kwa kuboresha kadiri unavyokwenda.
Kwenye kufanya kwa msimamo, tathmini na mrejesho ni viungo muhimu.
Kurudia makosa yale yale hakuwezi kukupa ushindi unaotaka.
Ni kufanya bila kuacha, lakini kwenda ukiboresha kwenye kila ufanyaji.
Kanuni kuu ya mafanikio kwenye jambo lolote ni usiache kufanya, ila fanya ukiboresha kila wakati kulingana na matokeo unayoyapata.
Na ndiyo maana kujifunza ni endelevu, hakuna wakati utafika na kusema tayari umeshamaliza kila kitu, kwa sababu kwenye kila hatua kuna vitu unaweza kuboresha zaidi.
Fanya bila kuacha, lakini fanya ukiboresha, kulingana na matokeo unayopata na mrejesho wa wengine.
Hiyo ndiyo njia ya uhakika ya kupata mafanikio yoyote makubwa unayoyataka kwenye maisha yako.
#NidhamuUadilifuKujituma
#AfyaUtajiriHekima
#KaziUpendoHuduma
#UpekeeUdadisiUbunifu
#UshirikianoUtegemeanoUwajibikaji
#BilioneaMafunzoni
#NajengaBiashara
#HakunaKingineMuhimu
#LazimaNitoboe
#NawekaKaziNifanikiwe
Fanya kwa msimamo lakini fanya ukiboresha kutokana na mrejesho unaopata kutokana na ufanyaji.
LikeLike
Ndiyo namna ya kupata matokeo bora.
LikeLike
Kufanya kwa msimamo huku ukipata mrejesho na kuboresha na pia kuendelea ukiwa unaendelea kupata matokeo mazuri kushinda jana
LikeLike
Ndiyo
LikeLike
Asante sana kocha kuhusu somo la msimamo ukizingatia tunaenda kuanza mwaka mwingine wa kisima cha maarifa,ambapo tunaenda kuwa wagumu zaidi ya ZAIDI.
LikeLike
Kabisa, tunaenda ngazi za juu zaidi.
LikeLike
Unafanya bila kuacha lakini unafanya kwa kuboresha kulingana na matokeo unayoyapata na mrejesho toka kwa wengine.
LikeLike
Hakika
LikeLike
Kanuni kuu ya mafanikio kwenye jambo lolote ni usiache kufanya, ila fanya ukiboresha kila wakati kulingana na matokeo unayoyapata.
LikeLike
Ndiyo.
LikeLike
msimamo kwa kurudia rudia na huku ukiboresha
LikeLike
Maboresho ni muhimu sana.
LikeLike
Asante kocha,Nitafanya bila kuacha,lakini nikiwa ninajitathimini kila siku nakuboresha zaidi.
LikeLike
Kila la kheri.
LikeLike
Fanya bila kuacha, lakini fanya ukiboresha, kulingana na matokeo unayopata na mrejesho wa wengine.
Hiyo ndiyo njia ya uhakika ya kupata mafanikio yoyote makubwa unayoyataka kwenye maisha yako. Asante Kocha Kwa sentence hii ni muhimu Sana kuzingatia.
LikeLike
Karibu
LikeLike
Asante Kocha,
Nitaendelea kufanya shughuli zangu kwa msimamo ili nione namna ya kuwa bora mara zote.
LikeLike
Kila la kheri.
LikeLike
Asante Kocha,
Nitaendelea kufanya shughuli zangu kwa msimamo ili nijue namna na sehemu ya kuboresha ili nipate mafanikio makubwa.
LikeLike
Vizuri
LikeLike
Fanya bila kuacha lakini Fanya ukiboresha, kulingana na matokeo unayopata kwa wengine
LikeLike
Hakika
LikeLike
Swala la msingi ni SAWA UNAFANYA KWA MSIMAMO, JE KUNA MABORESHO KWENYE MSIMAMO HUO..? Asante nimejua natakiwa kuzingatia ubora kwenye ufanya wangu.
Kila hatua ya urudiaji nabiresha kuwa na mafanikio
LikeLike
Hakika
LikeLike
Kurudia tu kufanya siyo msimamo utakaokupa mafanikio makubwa.
Bali kurudia kufanya huku ukiwa unaboresha kadiri unavyokwenda.
Asante sana
LikeLike
Maboresho ni lazima.
LikeLike
Nakubali kwa ulichoandika hapa sina shaka kabisa
LikeLike
Fanyia kazi.
LikeLike
Kurudia nakuboresha Asante sana kocha
LikeLike
Karibu
LikeLike
Asante sana Kocha,kwenye kila hatua kuna vitu naweza kuboresha zaidi.
LikeLike
Hakika, maboresho hayana mwisho.
LikeLike
Msimamo Unaenda moja kwa moja na kufanya kwa ubora zaidi ya Jana.
LikeLike
Ndiyo.
LikeLike
Kanuni kuu ya mafanikio kwenye jambo lolote ni kutokuacha kufanya, bali kufanya kwa msimamo bila kuacha huku ukiboresha kila wakati kulingana na matokeo yanayopatikana.
LikeLike
Msimamo wa maboresho endelevu.
LikeLike