3212; Epuka kujidanganya mwenyewe.
Rafiki yangu mpendwa,
Mwanafizikia Richard Feynman amewahi kunukuliwa akisema wajibu wako wa kwanza kwenye maisha ni kuhakikisha hujidanganyi, kwa sababu ni rahisi sana mtu kujidanganya mwenyewe.
Mtu unaweza kuchukulia kauli hiyo kirahisi na kuona huwezi kujidanganya, kwani unajiambia ukweli mara zote.
Lakini huo huo ukweli unaodhani unajiambia, ndiyo umejaa kujidanganya ndani yake.
Tuangalie mfano ili tuelewane vizuri.
Ni mara ngapi umeweka mipango mbalimbali, ambayo umekokotoa kwa usahihi kabisa, halafu wakati wa utekelezaji mambo yakawa tofauti?
Jibu ni karibu mara zote.
Mipango yoyote tunayoweka kuhusu mambo ya mbele, haiwezi kwenda vile ambavyo tumepanga.
Hata kama tutakuwa tumekokotoa kwa usahihi kiasi gani, kuna vitu vya mbele ambavyo hatuwezi kuviona mapema.
Hivyo basi, ili kuhakikisha hatujidanganyi kwa kuona tupo sahihi, tunapaswa kuiboresha mipango yoyote tunayoweka.
Kuna vitu vitatu tunavyopaswa kuviboresha kwenye mipango yetu ili angalau tuwe ndani ya ukweli.
Kitu cha kwanza ni gharama utakazotumia.
Ukishakokotoa gharama ambazo utatumia kwenye mipango yako, zidisha mara mbili.
Mara zote gharama huwa ni kubwa kuliko unavyopanga.
Hivyo unapozidisha gharama mara mbili, angalau unakuwa ndani ya kujiambia ukweli kuliko kwenda na hizo hizo za mipango.
Kitu cha pili ni muda utakaohitajika.
Ukishapanga muda ambao itachukua kukamilisha mipango yako, zidisha mara tatu.
Mara zote mipango huwa inachukua muda mrefu kuliko tunavyokuwa tumetegemea.
Unapozidisha muda mara tatu, unajiweka kwenye uhalisia zaidi kuliko matumaini hewa unayokuwa nayo mwanzoni.
Kitu cha tatu ni manufaa unayotegemea kupata.
Kwa manufaa uliyokokotoa kwamba utayapata, gawa nusu na hayo ndiyo utegemee.
Huwa tunaona manufaa ni makubwa na ya uhakika, lakini huwa haiwi hivyo, tunachokipata huwa ni kidogo kuliko tulichotarajia.
Unapogawa manufaa nusu, angalau unakuwa umepunguza kujidanganya.
Kama ambavyo tumeona kwenye hivyo vitu vitatu, tunajidanganya siyo kwa makusudi, bali kwa matumaini makubwa tunayokuwa nayo ila hayaendani na uhalisia.
Tahadhari, unakokotoa kwanza kwa hesabu zako sahihi, kisha jibu unalopata ndiyo unaliboresha kwa hizi kanuni tulizoshirikishana hapa.
Lakini wakati wa kutekeleza, fikiria mipango yako ya awali.
Kwa sababu ukitumia mipango uliyoboresha, unazidi kujidanganya.
Unapaswa kuendelea kupambania mipango yako ya mwanzo, lakini ukijua kuna nafasi ya mambo kwenda tofauti na ulivyotegemea.
Lengo la kuboresha hii mipango ni kukuweka kwenye fikra sahihi na kuondoa matumaini hewa yanayoweza kupelekea ukate tamaa pale mambo yanapokwenda tofauti na mipango yako.
#NidhamuUadilifuKujituma
#AfyaUtajiriHekima
#KaziUpendoHuduma
#UpekeeUdadisiUbunifu
#UshirikianoUtegemeanoUwajibikaji
#BilioneaMafunzoni
#NajengaBiashara
#HakunaKingineMuhimu
#LazimaNitoboe
#NawekaKaziNifanikiwe
Ninapaswa kuacha kujidanganya.Gharama zitakuwa mara mbili ya ninavyofikiria,muda utakuwa mara 3 ya ninavyotegemea na manufaa ni nusu ya ninavyotegemea.Asante kwa kunikumbusha hili.
LikeLike
Karibu
LikeLike
Na kweli mara nyingi huwa ndivyo inavyokuwa. Ni muhimu kwangu kuangalia hilo.
LikeLike
Vizuri
LikeLike
ni kweli hasa kwenye muda ndio changamoto unaweza kusema nitapita ofisi ya mtu na nitatumia nusu saa mala foleni mara utasikia wakuidhinisha ametoka. unajikuta umetumia masaaa 3
LikeLike
Hakika
LikeLike
Nimeipenda hii,,
1. Gharama ulizokadiria zidisha mara mbili
2. Muda uliojipangia zidisha mara tatu
3. Matokeo unayotarajia gawa nusu.
Kanuni hii nitakuwa naitumia mara kwa mara ili kuepuka kujidanganya mwenyewe.
LikeLike
Kila la kheri.
LikeLike
Asante Kocha,
Hiki ni kikokotoo cha kunisaidia sana kupunguza matumaini hewa, hivyo nisikate tamaa pale mambo yana pokuwa kinyume na matarajio yangu.
LikeLike
Vizuri
LikeLike
Hivi vitu vitatu ni sugu sana, swala la muda limekuwa lina ni sumbua sana kuna wakati napatia mara nyingine nashindwa sasa nimepata standard.
LikeLike
Itumie vyema.
LikeLike
Asante kocha,Nimuhimu kupambania mipango yangu ya maisha kila siku lakini kuna wakati mipango inabadilika hivyo sitakiwi kukata tamaa.
LikeLike
Ndiyo
LikeLike
Asante sana kocha,hizi kanuni nitazifanyia kazi, maana si vizuri kuendelea kujidanganya
LikeLike
Hakika
LikeLike
Hii kanuni ipo vizuri . Ili nisijidanganye na kujipa matumaini napaswa nifuate hizi kanuni.
1. Nikiweka mipango nitazidisha mara mbili.
2. Kwenye muda nitazidisha mara tatu ya ule muda niliopanga.
3. Kwenye mategemeo nitagawa nusu
LikeLike
Safi sana.
LikeLike