3215; Maswali na ngazi zake.
Rafiki yangu mpendwa,
Unaweza kuijua ngazi ambayo mtu amefikia kwenye safari yake ya mafanikio kupitia maswali anayokuwa anauliza kuhusu kile anachofanya au kutaka kufanya.
Wachanga kabisa huwa wanauliza maswali ya NINI.
Swali kuu likiwa NINI wafanye kwenye hatua fulani waliyopo au ili kupiga hatua fulani.
Hii ni ngazi ya chini kabisa ambayo watu hawajui hata cha kufanya.
Unaweza kudhani ukimwamjibu mtu cha kufanya atakuelewa na kufanya, lakini bado ataendelea na maswali yake ya NINI.
Ukweli ni hataki sana kupata majibu, bali maswali hayo yanadhihirisha ngazi aliyopo.
Walioanza kuchukua hatua huwa wanauliza maswali ya VIPI wafanye.
Hapa wanakuwa wameshaamua NINI wafanye, ila wanakuwa hawajajua wanafanya VIPI.
Hawa wanakuwa wamevuka hatua muhimu kabisa ya kuanza, ambayo ndiyo kikwazo kwa walio wengi.
Lakini bado wanakuwa wamekwama kwenye kufanya wao peke yao na hivyo kuna hatua nyingi wanazokuwa zinawasumbua.
Kwenye hatua hii unaweza kuwajibu watu jinsi wanavyopaswa kufanya, lakini bado watashindwa kupiga hatua kwa sababu ni wao peke yao wanaofanya kila kitu.
Wabobezi huwa wanauliza maswali ya NANI wa kufanya kile kinachopaswa kufanyika.
Wanakuwa wameshajua NINI cha kufanya, kinafanyika VIPI, ila hawataki kufanya wao peke yao, hivyo wanakuwa wanataka kujua NANI sahihi wa kufanya ili wapate wanachotaka.
Swali la NANI ndiyo swali muhimu zaidi kwa sababu lina ukuaji mkubwa ndani yake.
Tofauti ya wanaokua na wanaodumaa ni kwenye NANI.
Kuna ambao wanaishia kufanya peke yao, hawa wanadumaa kabisa.
Kuna ambao wanachukua yeyote anayepatikana kwa urahisi, hawa hupata ukuaji kidogo.
Na kuna ambao wanachukua wale walio bora kabisa na hawa hupata ukuaji mkubwa.
Waliofuzu wanauliza maswali ya KWA NINI wanafanya au wafanye kile wanachopaswa kufanya.
Hili ni swali la juu kabisa kwenye ufanyaji, ambalo linampa mtu msukumo wa kuendelea kufanya hata pale anapokutana na magumu.
Maswali ya KWA NINI ndiyo yanayofungua kusudi la mtu na maono makubwa anayokuwa nayo ndani yake.
Maswali ya KWA NINI huwa hayana majibu ya nje, bali huwa yanatokea ndani.
Na wengi huwa hawafiki ngazi hii au hata wakifika hawapati majibu sahihi kwa sababu wanakuwa hawajajitambua wao wenyewe.
Walio kwenye njia ya pembeni ya mafanikio huwa wanaanza na NINI, kisha kwenda kwenye VIPI, halafu nani na hatimaye KWA NINI.
Wengi sana kwenye njia hii huwa wanaishia kwenye VIPI, wachache hufika kwenye NANI ila napo hawafanyi vizuri.
Wachache sana kwenye njia hiyo wanaofika kwenye KWA NINI huwa wanafika wamechoka sana kiasi cha kushindwa kufanya makubwa.
Walio kwenye njia kuu ya mafanikio huwa wanaanza na KWA NINI, kisha NANI, VIPI na NINI.
Wanaanza kwa kujiuliza KWA NINI wanafanya au kupaswa kufanya kile wanachofanya. Hili linawapa kusudi na maono makubwa.
Wanafuata na kujiuliza NANI anayeweza kufanya yale yanayopaswa kufanyika, kwa ubora zaidi. Hapa wanapata njia ya kufanya kwa ukubwa.
Wakishajua wa kufanya, kinachofuata ni kujua VIPI wanaweza kuwapata watu hao bora ambao watafanya yake yanayopaswa kufanyika. Hapa wanapa njia ya kuwapata wale walio bora.
Na mwisho wanajiuliza NINI watu hao waliowapata wanahitaji ili waweze kuzalisha matokeo bora kama inavyohitajika. Hili linawapa njia bora ya kwenda nao.
Maswali kwako ni je upo kwenye njia ipi, ya kando au kuu?
Kama umejibu njia ya kando, jibu mpaka sasa ulikuwa umekwama kwenye swali la ngazi ipi.
Na kama umejibu upo njia kuu, jibu ngazi zote kwa majibu sahihi kwako.
#NidhamuUadilifuKujituma
#AfyaUtajiriHekima
#KaziUpendoHuduma
#UpekeeUdadisiUbunifu
#UshirikianoUtegemeanoUwajibikaji
#BilioneaMafunzoni
#NajengaBiashara
#HakunaKingineMuhimu
#LazimaNitoboe
#NawekaKaziNifanikiwe
Njia kuu ndiyo njia inayoleta mapinduzi duniani kwa njia ya kuuliza swali la kwa nini.
Kwa nini ndiyo inatoa sababu ya kweli ya mtu kutoka ndani.
Asante sana
LikeLike
Hakika
LikeLike
Jibu ni njia kuu ndio inayoleta matokeo makubwa
Asante
LikeLike
Vizuri
LikeLike
Asante Kocha,
KWA NINI (WHY?); KUSUDI, MAONO
NANI (WHO?); UBORA, UKUBWA
VIPI (HOW?); KUWA NA WALIOBORA
NINI (WHAT?); WALIOBORA WANAHITAJI NINI?
Naamini hii ndiyo namna ya kuwa njia kuu. Mimi ninataka kujikwaua kutoka ngazi ya 2, NANI?
LikeLike
Vizuri, kila la kheri.
LikeLike
Asante kocha,Kwa nini ni swali la juu zaidi ambalo nikijiuliza linanipa msukumo mkubwa ambao nitaendelea kuufanyia kazi ili nipate matokeo bora zaidi.
LikeLike
Vizuri sana.
LikeLike
Njia kuu.Kwa kuanza kuuliza swali kwa nini linafanya ufanye kitu toka ndani yako.
LikeLike
Hakika
LikeLike
Asante sana. Nimepita njia ya kando kufika hapa nilipo.
Nilianza Kwa kujiukiza nifanye Nini? Na hili ndilo lilipelekea kukutana na Wewe. Hapa ndiyo nikapata ushauri kutoka kwako wa baadhi ya biashara ambazo mwanachuo anaweza kufanya kutoka kwenye blogu ya amka mtanzania.
Kisha niliuliza swali la vipi. Na hili ndilo lilipelekea kujiunga na programu Yako ya uandishi (professional bloggers) na baadaye kisima Cha maarifa
Swali la nani. Hili ni swali ambalo nimechelewa kujiuliza. Au pengine nilikuwa najiuliza ila nilikuwa sichukui Hatua. Isingekuwa program ya bilionea mafunzoni na mwongozo wa nwakanhuu unaoisha kwakba kila MTU anapaswa kuajiri, nisingejiuliza sana hili swali au hata kama ningechukua Hatua, ingekuwa ya chini kabisa
Sasa Hivi nimeshakaa njia kuu kocha. Kilichobaki ni kuchukua Hatua kubwa
LikeLike
Vizuri sana, kila la kheri.
LikeLike
Niko njia kuu.
LikeLike
Kaa hapo.
LikeLike
Hii kweli safari ni ndefu nakumbuka nilivyomuuliza kocha biashara gani,NINI naweza kufanya,kumbe kuuliza maswali ni muhimu kwa ngazi tofauti.
LikeLike
Swali la nini wanahitaji ili kupata matokeo ndio swali ambalo najiuliza sana kwa sasa kocha. Asante.
LikeLike
Vizuri, fanyia kazi.
LikeLike