3218; Upotevu mkubwa wa muda.
Rafiki yangu mpendwa,
Kuna muda ambao huwa tunaupoteza tukiwa tunajua kabisa ya kwamba tunapoteza muda.
Hapa ni pale ambapo unakuwa unafanya vitu ambavyo havina mchango wa wewe kufika kule unakotaka kufika.
Upotevu huu wa muda huwa unaweza kujishtukia na kuacha kupoteza muda.
Halafu sasa, kuna muda ambao huwa tunaupoteza tukiwa hatujui kama tunapoteza muda.
Na huu ndiyo upotevu mbaya zaidi wa muda ambao wengi huwa hawaugundui mpaka pale wanapokuwa wameshaumia sana.
Kwenye upotevu huu wa muda, watu wanakuwa wanafanya vitu ambavyo wanadhani vina mchango wa kufika kule wanakotaka kufika, lakini matokeo yake huwa ni ya tofauti kabisa.
Moja ya upotevu huo wa muda ni kuwalazimisha watu ambao hawataki kukua wakue.
Unakuwa unaona watu hao wanao uwezo wa kukua na unaona wakikua wote mtanufaika, hivyo unaona kuwalazimisha wakue ni matumizi mazuri ya muda wako.
Huu ni upotevu mkubwa wa muda kwa sababu hata umlazimishe mtu kiasi gani, kama hataki kukua, hatakua.
Hata ukaweka nguvu kwa muda mrefu, utakachoambulia ni kuzipoteza tu nguvu hizo.
Na hilo ndiyo linafanya upotevu wa muda kuwa mkubwa, kwa sababu unakuwa hujapata matokeo na muda na nguvu ulizoweka huwezi kurudisha.
Huwa kuna hali ya huruma, hasa kwa watu wa karibu kwa kuona labda tukiweka juhudi zitaleta mabadiliko kwao.
Lakini matokeo huwa ni kinyume, juhudi zote tunazoweka tunakuwa tumezipoteza.
Lazima tukubali kwamba baadhi ya watu hawatakwenda kupata ushindi mkubwa kwenye maisha yao.
Lazima tukubali kila mtu kuna namna ya kipekee anayaona na kuyachukulia maisha.
Na lazima tukubali kila mmoja yupo sawa kwa mtazamo wake binafsi.
Wajibu wako wa kwanza kwenye maisha ni kupata ushindi wako binafsi, kwa kuwa kile unachopaswa kuwa, kutumia kile kilicho ndani yako kufanya makubwa.
Wengine wanafanya nini au wanapaswa kufika wapi hilo siyo jukumu ambalo lipo ndani ya udhibiti wako.
Kama wao wenyewe watakuwa nao wametaka ushindi na wakawa tayari kuupambania, unaweza kuambatana nao.
Lakini kama watu hawajataka ushindi na wala hawaupambanii, wewe kuwalazimisha wapate ushindi ni kujizuia wewe mwenyewe usipate ushindi.
Una wajibu wa kuhakikisha hakuna mtu yeyote ambaye atakuzuia kupata ushindi unaoutaka, kwa sababu wao hawataki ushindi.
Peleka muda wako na nguvu zako kwenye mambo ambayo unaweza kuyadhibiti na kuyaathiri moja kwa moja.
Na jambo la kwanza ni ushindi wako kwenye maisha yako na siyo ya wengine.
Ushindi wako unaanza na ukuaji wako binafsi na siyo ukuaji wa wengine.
Muda wako ni mfupi,
Nguvu zako zina ukomo,
Usitawanye rasilimali hizo kwa vitu ambavyo havikupi matokeo unayotarajia, hasa yale ambayo yapo chini ya udhibiti wako.
Pambana kupata ushindi na wale ambao nao wanataka kupata ushindi, wataambatana na wewe.
Lakini pia ushindi una ukomo tofauti kwa watu tofauti.
Kuna wanaoanzia chini na wakifika ngazi fulani wanaridhika. Hawa nao wanaweza kuwa kikwazo kwako kuendelea, hivyo wajue na hakikisha hawawi kikwazo.
Kuna ambao wamejitoa hasa kupata ushindi, wapo tayari kuupambania kwa kila namna na mara zote wanakua bila ya ukomo. Hao ambatana nao, kwa sababu wanakupa nguvu kwenye safari hiyo inayokuwa ngumu kwako.
#NidhamuUadilifuKujituma
#AfyaUtajiriHekima
#KaziUpendoHuduma
#UpekeeUdadisiUbunifu
#UshirikianoUtegemeanoUwajibikaji
#BilioneaMafunzoni
#NajengaBiashara
#HakunaKingineMuhimu
#LazimaNitoboe
#NawekaKaziNifanikiwe
Asante Kocha,
Nguvu na muda wangu nitaelekeza kwenye yale ninayoweza kuyadhibiti na kuyaathiri moja kwa moja ili nipate ushindi wangu kwanza. Wale wanaowania nao ushindi nitaambatana nao nikishajiridhisha kwamba wao si kikwazo kwangu.
LikeLike
Vizuri
LikeLike
Wajibu wako wa kwanza kwenye maisha ni kupata ushindi wako binafsi, kwa kuwa kile unachopaswa kuwa, kutumia kile kilicho ndani yako kufanya makubwa.
Wengine wanafanya nini au wanapaswa kufika wapi hilo siyo jukumu ambalo lipo ndani ya udhibiti wako
LikeLike
Kazana na ushindi wako na utaweza kuwavutia wengine.
LikeLike
Wajibu wangu wa kwanza kwenye maisha ni kupata ushindi wangu binafsi kwa kuwa kile ninachopaswa kuwa na Kutumia kile kilicho ndani yangu kufanya makubwa. Natambua kuwa MUDA ni MFUPI na NGUVU zina UKOMO.
LikeLike
Hakika
LikeLike
Wajibu wangu wa kwanza ni kupata ushindi kwwnye maisha yangu na ntaendelea kufanya kwa vitendo vikubwa katika biashara yangu
LikeLike
Kila la kheri
LikeLike
asante sana kocha Makirita Aman….
LikeLike
Karibu.
LikeLike
Pambana kupata ushindi na wale ambao nao wanataka kupata ushindi, wataambatana na wewe
LikeLike
Hakika
LikeLike
Asante sana
LikeLike
Karibu
LikeLike
Ambatana na wale wanaotaka ushindi ili mtoke pamoja hayo ndio maisha ya mafanikio
Asante sana
LikeLike
Hakika
LikeLike
Asante kocha wajibu wangu wa kwanza ni mimi kupata ushindi,na wale ambao nao wanataka ushindi wataambatana na mimi
LikeLike
Vizuri
LikeLike
Kama mtu hajataka mafanikio na haweki juhudi kuyatafuta mafanikio yake, wewe kumlazimisha upambanie mafanikio yake ni kupoteza muda wako pia ni kujichelewesha wewe mwenyewe kupata mafanikio.
Asante kocha
LikeLike
Hakika.
LikeLike
Asante kocha,Ushindi wangu binafsi unaanza na mimi na sio watu wengine.
LikeLike
Ndiyo
LikeLike
Haya mafunzo yanatufanya kuwa jasiri sana hasa kwenye suala la kujitambua, mfano kama najua ushindi unaanza na mimi maana siwezi kuhangaika na watu,nitasumbuka na yule anaetaka kuwa kikwazo ili nimwondoe au niepuke naye kwenye njia ya safari yangu ya ushindi.
LikeLike
Hakika.
LikeLike
Ushindi una ukomo tofauti kwa watu tofauti
LikeLike
Ndiyo
LikeLike
Ahsante sana kocha
LikeLike
Karibu
LikeLike