3232; Umepanga kulipaje?
Rafiki yangu mpendwa,
Tunajua kwamba hakuna kitu cha bure.
Kwa chochote kile tunachotaka kwenye maisha, huwa kuna gharama ambayo lazima tuilipe.
Zipo njia mbili za kulipa gharama ya kupata kile tunachotaka.
Njia ya kwanza ni kulipa kwa fedha.
Hapa unatoa fedha na kuwalipa wale ambao wanakusaidia kupata kile unachotaka.
Njia hii japo inaweza kuonekana ya gharama kubwa, ndiyo njia bora ya kulipia mambo mengi kwenye maisha.
Kwani ni njia inayokuacha na muda wa kuweza kufanya yale unayoyafanya vizuri zaidi.
Njia ya pili ni kulipa kwa muda, machozi, jasho na damu.
Hii ni njia ambayo wewe mwenyewe unaingia kwenye kufanyia kazi kile unachokitaka.
Njia hii inaweza kuonekana ni ya gharama nafuu, lakini siyo iliyo bora. Kwa sababu mambo mengi unayohangaika nayo huna ubobezi wa kuweza kuleta matokeo mazuri unayoyataka.
Utaweka juhudi kubwa na kwa mateso, lakini utaishia kupata matokeo madogo na ya kawaida, ambayo hayakufikishi kule ulikotaka kufika.
Kama unataka kupata mafanikio makubwa kwenye maisha yako, tumia njia ya kwanza kwenye mambo yote ambayo hayahusiani moja kwa moja na shughuli zako kuu.
Yaani pale unapokuwa na kitu unachopaswa kufanya, kama siyo kile ulichobobea, basi walipe wengine wafanye.
Hilo litakuacha wewe ukiwa na muda, nguvu na umakini unaoweza kuutumia kwenye eneo ulilobobea na kuzalisha matokeo bora kabisa.
Lakini pia njia ya kwanza ndiyo unayoweza kuitumia kupata mafanikio unayoyataka.
Unachofanya ni kutatua tatizo kubwa ambalo linawakabili watu wengi, kisha kuwatoza watu fedha ili uweze kuwatatulia.
Kama unaanzia chini ambapo huwezi kumudu kulipa kwa fedha, lipa kwa muda, machozi, jasho na damu huku ukijijengea nguvu ya kuweza kulipa kwa fedha.
Kwenye maisha, unaweza kutumia muda ili kuokoa fedha au kutumia fedha ili kuokoa muda.
Kipi kipaumbele kwako inategemea ngazi yako ya mafanikio.
Unapokuwa unaanzia chini, unakuwa na muda mwingi na fedha kidogo, hivyo utatumia muda kuokoa fedha.
Unapokuwa umepiga hatua za mafanikio, unakuwa na fedha nyingi na muda kidogo, hivyo utatumia fedha kuokoa muda.
Mara zote hatua nzuri ni kutumia fedha kuokoa muda, kwa sababu muda una ukomo, lakini fedha hazina ukomo kabisa.
Pambana sana kufika hatua ambayo mambo mengi unayatatua kwa fedha ili ubaki na muda wa kutosha kuweka kwenye yale muhimu zaidi.
#NidhamuUadilifuKujituma
#AfyaUtajiriHekima
#KaziUpendoHuduma
#UpekeeUdadisiUbunifu
#UshirikianoUtegemeanoUwajibikaji
#BilioneaMafunzoni
#NajengaBiashara
#HakunaKingineMuhimu
#LazimaNitoboe
#NawekaKaziNifanikiwe
Hatua inayofuata ni kutumia fedha kuokoa muda!
LikeLike
Safi sana.
LikeLike
Kutumia muda kuna ukomo. Lakini fedha haina ukomo. Hivyo kupambana kufikia hatua ya kutatua matatizo mengi kwa njia ya fedha.
LikeLike
Hakika
LikeLike
Mara zote hatua nzuri ni kutumia fedha kuokoa muda kwa sababu muda una ukomo lakini fedha hazina ukomo.
LikeLike
Ndiyo
LikeLike
Ninatumia fedha zangu kuokoa muda hasa kwenye shughuri zile ambazo zinatumia muda wangu Mimi naajili mtu na kumlipa na huo muda naendelea na jambao lingine muda haulipiki lakini fedha zinalipika
LikeLike
Vizuri sana.
LikeLike
Asante Kocha,
Nitapambana kwa nguvu kubwa kufika hatua ambayo mambo mengi nitayatatua kwa fedha ili nibaki na muda, nguvu na umakini kwenye yale muhimu yanayohitaji uwe po wangu wa moja kwa moja.
LikeLike
Kila la kheri.
LikeLike
Asante Kocha.
Kutumia fedha kuokoa muda ndiyo lengo langu la maisha. Nitapambana kuhakikisha nalifikia hili lengo kwa kuwa na fedha nyingi.
LikeLike
Kila la kheri.
LikeLike
Mara zote hatua nzuri ni kutumia fedha kuokoa muda, kwa sababu muda una ukomo, lakini fedha hazina ukomo kabisa.
LikeLike
Kabisa
LikeLike
Tumia fedha kuokoa muda kutatua tatizo
Asante sama
LikeLike
Ndiyo
LikeLike
Natakiwa nipambane kuwa na hela ndefu ili niweze kuokoa muda. Asante sana.
LikeLike
Kabisa
LikeLike
hatua nzuri ni kutumia fedha kuokoa muda, muda una ukomo lakini fedha hazina ukomo. asante sana kocha kwa hili, nitatumia fedha mara zote kuokoa muda wangu wa thamani sana
LikeLike
Kweli kabisa.
LikeLike
Napambana sana ili kufika hatua mambo mengi nitayatatua kwa fedha ili nibaki na muda wa kutosha kuweka kwenye yale muhimu zaidi.
LikeLike
Kila la kheri
LikeLike