3245; Kabla ya kuhangaika na magumu.
Rafiki yangu mpendwa,
Kwenye safari ya mafanikio, watu huwa wanapenda kuhangaika na mambo makubwa na magumu.
Lakini unakuta watu hao hao bado hawajaweza kufanya yale ya msingi kabisa kwenye eneo husika.
Yale ya msingi huwa yanaoneka ni rahisi na yasiyo na mchango mkubwa.
Lakini ndiyo mambo magumu kutekeleza na yenye nguvu kubwa yanapotekelezwa.
Kwenye fedha, watu huwa wanahangaika na mambo makubwa na magumu ya kuingiza kipato kikubwa.
Wakati kuna mambo ya msingi kabisa yanakuwa yanawashinda, kama kuhakikisha matumizi hayazidi kipato.
Mambo ya msingi kabisa kwenye fedha ni kuhakikisha matumizi ni madogo kuliko kipato na hiyo tofauti ya kipato na matumizi ndiyo inawekwa akiba na kuwekezwa.
Kama hilo litakushinda, yaani kama matumizi yako yanazidi mapato, hakuna chochote kinachoweza kukusaidia kwenye eneo la fedha.
Kwenye biashara watu huwa wanahangaika na mambo makubwa na magumu kama matumizi ya teknolojia mpya kuja na ubunifu wa kipekee.
Lakini wanakuwa wameshindwa kufanya mambo ya msingi kabisa ambayo ni kuwa na kitu ambacho watu wana uhitaji nacho na kuwafikia watu wengi zaidi wenye huo uhitaji.
Mambo ya msingi kabisa ambayo yanapaswa kuzingatiwa kwenye biashara ni kuwa na bidhaa/huduma ambayo watu wana uhitaji nayo na kuwafikia watu wa aina hiyo wengi zaidi.
Ukishindwa kukamilisha haya ya msingi, hakuna kingine chochote kitakachoweza kukusaidia, hata utumie teknolojia gani na kuwa na ubunifu kiasi gani.
Kadhalika kwenye afya, watu wamekuwa wanahangaika na mambo mengi makubwa na magumu ili kuwa na afya bora.
Wamekuwa wanahangaika sana na nini wanakula, wanakula wakati gani na kwa namna gani.
Lakini mambo ya msingi kabisa kwenye afya ni kutumia zaidi ya unavyoingiza.
Yaani kuhakikisha mwili unatumia chakula kingi kuliko ambacho kinaingia mwilini.
Hiyo inamaanisha kula kidogo na kufanya mazoezi zaidi.
Hii ni mifano michache, lakini kwenye kila eneo la maisha kuna mambo ya msingi ambayo tunapaswa kuyakamilisha kabla ya kuhangaika na makubwa na magumu.
Watu wanaoyapuuza mambo hayo ya msingi na kukimbilia magumu, huwa hawafanikiwi, hata wahangaike kiasi gani.
Ni sawa na mwanafunzi anayeenda kwenye elimu ya sekondari kabla ya elimu ya msingi.
Kamilisha yale ya msingi na yakamilishe kwa viwango vya juu sana.
Utajikuta huhitaji hata kuhangaika na magumu.
Kwa sababu utakuwa umetingwa sana na mafanikio makubwa unayokuwa unayapata.
Mafanikio huwa hayahitaji akili kubwa, bali yanahitaji akili ya kawaida na utekelezaji wa msimamo kwenye kile ambacho mtu anafanya.
#NidhamuUadilifuKujituma
#AfyaUtajiriHekima
#KaziUpendoHuduma
#UpekeeUdadisiUbunifu
#UshirikianoUtegemeanoUwajibikaji
#BilioneaMafunzoni
#NajengaBiashara
#HakunaKingineMuhimu
#LazimaNitoboe
#NawekaKaziNifanikiwe
Asante sana kuhusu Mambo ya msingi kwenye Fedha kutumia kidogo kuliko unavyoingiza,na kwenye afya hivyo kufanya mazoezi
Asante sana kocha.
LikeLike
Karibu
LikeLike
Asante Kocha,
Nimejifunza nikikamilisha Yale yote ya msingi kikamilifu, yale magumu yatajikamilisha yenyewe.
LikeLike
Hakika
LikeLike
👉Biashara ni kuwa na bidhaa/huduma ambayo watu wanahitaji na kuwafikia wengi zaidi.
👉Vilevile mafanikio huwa hayahitaji akili kubwa,Bali yanahitaji akili ya kawaida na utekeleji kwa msimamo kwenye like mtu anafanya.
🙏🙏
LikeLike
Kabisa.
LikeLike
Kwa kweli kuna nguvu kubwa kwenye kufanya yale ya msingi kabisa na rahisi.
LikeLike
Ndiyo
LikeLike
Mafanikio makubwa yanahitaki kufanya mambo ya msingi Kwa msimamo
Asante sana
LikeLike
Karibu.
LikeLike
Mafanikio huwa hayahitaji akili kubwa, bali yanahitaji akili ya kawaida na utekelezaji wa msimamo kwenye kile ambacho mtu anafanya.
LikeLike
Ndiyo
LikeLike
Nitafanya ya kawaida kabla ya magumu.
LikeLike
Vizuri
LikeLike