💯KCM2324023; Faraja.

Tumejipata, Tunaachilia Breki.

#JumanneYaKujikubali

Mwanamafanikio,

Mwaka wa mafanikio 2023-2024 tumejipata kwa kuchagua kufanyia kazi kwa ukubwa kitu kimoja mpaka kitupe mafanikio makubwa tunayoyataka.

Tumeachilia breki kwa kufanyia kazi maeneo sita; MALENGO, KUJIKUBALI, UWAJIBIKAJI, UBUNIFU, MAWASILIANO na UTULIVU ili kujipa uhakika wa kufanya makubwa.

Ndani yako una nguvu ya kufanya makubwa sana, ifikie na kuitumia. Wasiliana sasa na 0752 977 170 kupata kitabu.



💯 Neno la leo; Faraja.

Leo ikiwa ni #JumanneYaKujikubali tunaona jinsi ambavyo faraja ya mtu ni zao la kujipa kibali yeye mwenyewe.

Watu wengi wamekuwa wanayaishi maisha yao kwa kusubiri watu wengine wawape ruhusa ya kufanya kile ambacho wangependa kufanya.

Karibu kila mtu anajua nini hasa anachotaka na anapaswa kufanya nini ili kupata kile anachotaka.
Lakini wengi hawapo tayari kusema wazi kile wanachotaka wala kuchukua hatua wanazopaswa kuchukua, kwa sababu sivyo wale wanaowazunguka wanavyofanya.

Watu wengi wanakosa uthubutu wa kuyaishi maisha ya kweli kwao na kujikuta wakiishi maisha ya kuigiza, ili tu wapate kibali kwa wengine.
Watu wanaona ni bora kukubalika na wengine kwanza hata kama wao wenyewe hawajikubali.

Wanaweza kukazana kuishi maisha ya maigizo ili kukubalika na wengine, na kweli wakakubalika, lakini hilo linakuja na gharama moja kubwa ambayo ni kukosa faraja.
Faraja ndiyo kitu kikuu ambacho kila mtu anataka kwenye maisha, ndiyo msukumo wa kila tunachofanya.
Ukweli ni kwamba huwezi kupata faraja kama hujajipa kibali wewe mwenyewe.
Kama hujajikubali wewe mwenyewe na kuishi maisha yenye maana kwako, unakuwa huna maisha.

Tulipokuwa watoto, tulikuwa tunafanya yale tunayotaka kufanya, bila ya kujali wengine wanatuchukuliaje.
Lalini kidogo kidogo watu wazima waliokuwa wanatuzunguka wakaanza kutubadili kwa kutufanya tufanye yale tu tunayoruhusiwa kufanya.
Kupitia adhabu na zawadi, tulifundishwa kusubiri wengine watupe ruhusa na kibali ndiyo tufanye kitu.
Kwa kuwa hilo lilifanyika kwa muda mrefu, limegeuka kuwa ndiyo maisha yetu.

Sasa tumekuwa watu wazima, lakini bado tunaishi kwa mazoea yale yale ya utotoni.
Hatufanyi tunachotaka mpaka tupewe ruhusa na wengine.
Kwa bahati mbaya sana, hayupo tena mtu wa kuturuhusu au kutuzuia.
Kwa sasa ni sisi wenyewe wa kujipa ruhusa au kujizuia.
Kwa bahati mbaya, hakuna ambaye amewahi kutuambia hili.

Leo hii nakuambia ukweli ambao hujawahi kuambiwa kwa maisha yako yote.
Huhitaji kusubiri ruhusa au kibali cha mtu yeyote ndiyo uyaishi maisha unayotaka.
Hicho ni kitu ambacho kipo ndani ya uwezo wako mwenyewe.
Unajua kwa hakika unachotaka na unajua unachopaswa kufanya.
Jipe kibali sasa cha kufanya bila kuangalia wengine wanakuchukuliaje.
Hakuna anayehangaika na maisha yako kama unavyodhani.
Wengi wamevurugwa na maisha yao kama na wewe ulivyovurugwa na yako.

Usisubiri faraja hewa kwa kutaka kupewa ruhusa na wengine, hakuna mwenye nguvu hiyo tene.
Jipe faraja wewe mwenyewe kwa kujipa kibali cha kuishi maisha ambayo unayataka wewe mwenyewe.
Hivyo ndivyo kujikubali wewe mwenyewe na kuyaishi maisha yako kwa namna sahihi kwako kunavyokuwa na nguvu ya kukupa mafanikio makubwa.

Kutokujikubali ni breki ambazo zinawakwamisha wengi kuwa na maisha ambayo wanayataka.
Wewe achilia hizo breki kwa kujipa ruhusa ya kuishi vile wanavyotaka na hicho ndiyo kinakuwa chanzo cha kufanya makubwa.

💯Hatua za kuchukua leo;
1. Andika ahadi yako ya mwaka wa mafanikio 2023-2024 kwa mtiririko wa NINI, LINI, WAPI, KWA NINI, NANI, VIPI na HISIA kisha weka kwenye kundi.
2. Soma kurasa 10 za kitabu cha MTAALA WA UTAJIRI na shirikisha uliyojifunza kwenye kundi.
3. Chukua hatua kwenye yale ambayo umeshajifunza na shirikisha kwenye kundi.
4. Matokeo unayopata yashirikishe kwenye kundi.
5. Kaa kwenye mchakato sahihi wa kile unachotaka kufikia na epuka usumbufu unaokuwa kikwazo kwako.

Makala ya ukurasa wa leo ni kuhusu kuanza upya na kama ungerudia kufanya unachofanya sasa. Isome, weka maoni na nenda kachukue hatua. Fungua hapa; https://www.kisimachamaarifa.co.tz/2023/11/21/3247

Ukawe na siku bora kabisa ya leo, siku ya kujipa kibali cha kuishi vile unavyotaka ili uweze kupata faraja na mafanikio makubwa.

Kocha.
💯