💯KCM2324024; Uhuru.

Tumejipata, Tunaachilia Breki.

#JumatanoYaUwajibikaji

Mwanamafanikio,

Mwaka wa mafanikio 2023-2024 tumejipata kwa kuchagua kufanyia kazi kwa ukubwa kitu kimoja mpaka kitupe mafanikio makubwa tunayoyataka.

Tumeachilia breki kwa kufanyia kazi maeneo sita; MALENGO, KUJIKUBALI, UWAJIBIKAJI, UBUNIFU, MAWASILIANO na UTULIVU ili kujipa uhakika wa kufanya makubwa.

Kila kitu kwenye maisha huwa kina kanuni yake ambayo ikitumika inaleta mafanikio. Hivyo pia ndivyo ilivyo kwenye kila siku yako. Kuna kanuni ambayo ukiijua na kuifuata, itakupa matokeo makubwa. Kitabu cha KANUNI YA SIKU YA MAFANIKIO ndiyo unachohitaji ili uwe na siku za mafanikio. Kipate sasa kwa kuwasiliana na 0752 977 170



💯 Neno la leo; Uhuru.

Leo ikiwa ni #JumatanoYaUwajibikaji tunaona jinsi ambavyo uhuru unakuja na gharama ya uwajibikaji.

Kila mtu anapenda kuwa na uhuru kwenye maisha yake.
Aishi vile anavyotaka yeye na kufanya yale anayotaka, bila ya kushurutishwa na yeyote.

Lakini watu wengi huwa hawajui kwamba uhuru huwa unakuja na gharama ambayo lazima mtu ailipe.
Na gharama kubwa sana ya uhuru ni uwajibikaji.

Upo huru kabisa kuishi vile unavyotaka wewe, kwa kufanya unayojipangia mwenyewe.
Lakini sasa, unapopata matokeo, usianze kutafuta watu wa kuwalaumu.
Matokeo yoyote unayoyapata, yawe mazuri au mabaya ni wewe unawajibika nayo.

Ukianza tu kuyakataa matokeo unayoyapata kwa kutafuta wengine wa kuwalaumu, hapo unakuwa umejinyima uhuru unaotaka kuwa nao.
Pale unapokataa kuwajibika, ndiyo unakuwa umejivua uhuru unaotaka kuwa nao.

Yeyote au chochote unachokuwa unakilalamikia kwa matokeo unayoyapata ndiyo kinakuwa kimeshikilia uhuru wako.
Unapoacha kabisa kuwalalamikia wengine na kushika hatamu ya maisha yako wewe mwenyewe ndiyo unakuwa huru.

SHUJAA NI MTU ANAYEELEWA KWAMBA UHURU UNAAMBATANA NA UWAJIBIKAJI.
Hivyo anawajibika kwa kila kitu kwenye maisha yake.
Halaumu wala kulalamika.
Anaangalia amechangiaje kwenye matokeo aliyopata, kisha anaboresha hatua anazochukua.

Kitu kimoja ambacho watu wengi huwa hawakielewi ni kwamba vitu vingi kwenye maisha huwa havikwepeki.
Bali vinaweza kuhamishwa kutoka mahali pamoja na kwenda pengine.

Uwajibikaji haukwepeki kwenye maisha.
Ni labda utachagua kujiwajibisha wewe mwenyewe na hapo kujiweka kwenye nafasi ya kufanya makubwa.
Au utawajibishwa na wengine na hapo kutumika kukamilisha makubwa ya hao wengine.

Chagua kwa usahihi unataka kuwa upande upi, kisha wajibika kwenye huo upande.
Kukosa uwajibikaji ni breki ambayo imewazuia wengi wasipate mafanikio makubwa.
Wewe wajibika, jiwajibishe mwenyewe na utaweza kufanya makubwa.

💯Hatua za kuchukua leo;
1. Andika ahadi yako ya mwaka wa mafanikio 2023-2024 kwa mtiririko wa NINI, LINI, WAPI, KWA NINI, NANI, VIPI na HISIA kisha weka kwenye kundi.
2. Soma kurasa 10 za kitabu cha MTAALA WA UTAJIRI na shirikisha uliyojifunza kwenye kundi.
3. Chukua hatua kwenye yale ambayo umeshajifunza na shirikisha kwenye kundi.
4. Matokeo unayopata yashirikishe kwenye kundi.
5. Kaa kwenye mchakato sahihi wa kile unachotaka kufikia na epuka usumbufu unaokuwa kikwazo kwako.

Makala ya ukurasa wa leo ni kuhusu kuendelea kufanya licha ya ugumu wa mwanzo. Isome, weka maoni na nenda kachukue hatua. Fungua hapa; https://www.kisimachamaarifa.co.tz/2023/11/22/3248

Ukawe na siku bora kabisa ya leo, siku ya kujiwajibisha ili uweze kuwa huru na kupata matokeo makubwa unayoyataka.

Kocha.
💯