KCM23240256; Hisia.

Tumejipata, Tunaachilia Breki.

#IjumaaYaMawasiliano

Mwanamafanikio,

Mwaka wa mafanikio 2023-2024 tumejipata kwa kuchagua kufanyia kazi kwa ukubwa kitu kimoja mpaka kitupe mafanikio makubwa tunayoyataka.

Tumeachilia breki kwa kufanyia kazi maeneo sita; MALENGO, KUJIKUBALI, UWAJIBIKAJI, UBUNIFU, MAWASILIANO na UTULIVU ili kujipa uhakika wa kufanya makubwa.

Hitaji muhimu la kufanikiwa kwenye maisha ni kuwa na ushawishi mkubwa kwa wengine. Kitabu cha CHUO CHA MAUZO kinakujengea uwezo mkubwa wa ushawishi. Kipate sasa 0752 977 170.

 Neno la leo; Hisia.

Leo ikiwa ni #IjumaaYaMawasiliano tunaona umuhimu wa kuwasilisha vyema hisia zetu kwa wengine.

Mawasiliano ya wengi yamekuwa hayakamiliki kwa sababu wamekuwa wanakazana kuwasilisha tu mawazo yao.
Wanahangaika kuwafanya watu wasikie kile wanachosema na kuona wanachomaanisha.

Lakini zoezi hilo huwa halina matokeo mazuri, kwa sababu watu wanakuwa wagumu kuelewa.
Na hata kama wataelewa, huwa wanasahau haraka na kurudi kwenye mazoea ya nyuma.

Ili mawasiliano yakamilike, siyo tu mawazo yanapaswa kuwasilishwa kwa usahihi, bali na hisia pia.
Mawasiliano yanakuwa yamekamilika pale mtu anapoelewa kile alichokuwa anaeleweshwa na kuwa na hisia ambazo mweleweshaji anakuwa nazo.

Maamuzi yetu sisi binadamu huwa tunayafanya kwa hisia kwanza kisha kuyahalalisha kwa mantiki.
Hivyo kama unataka kueleweka haraka, gusa hisia za watu.
Hisia zinawafanya waelewe haraka na hata kukumbuka kwa muda mrefu zaidi.

Uzuri wa hisia ni kitu ambacho kinaambukizwa. Hivyo kwa hisia zozote ambazo unataka mtu awe nazo ili kukuelewa vizuri, unapaswa kuwa nazo wewe kwanza wakati unawasiliana naye.
Kadiri unavyokuwa na hisia hizo kwa ukali wakati unamwelewesha mtu kitu, ndivyo na yeye anavyoambukizwa hisia hizo na kuelewa haraka.

KUJITAMBUA KIHISIA NI MUHIMU ILI UWEZE KUWASILISHA VIZURI MAWAZO YAKO NA HISIA ZAKO KWA WATU WENGINE.
Mawasiliano yanakuwa hayajakamilika kama hayajagusa hisia ya mtu.
Ukitaka ueleweke haraka na watu wakumbuke kitu kwa muda mrefu, wasilisha kwao kwa hisia kali.
Hisia huwa zinaambukizwa na zina nasa kwa kuda mrefu zaidi.

Mawasiliano sahihi na yaliyokamilika ni moja ya njia muhimu ya kuondoa breki ambazo zinawazuia wengi kupata mafanikio makubwa.

Hatua za kuchukua leo;
1. Andika ahadi yako ya mwaka wa mafanikio 2023-2024 kwa mtiririko wa NINI, LINI, WAPI, KWA NINI, NANI, VIPI na HISIA kisha weka kwenye kundi.
2. Soma kurasa 10 za kitabu cha MTAALA WA UTAJIRI na shirikisha uliyojifunza kwenye kundi.
3. Chukua hatua kwenye yale ambayo umeshajifunza na shirikisha kwenye kundi.
4. Matokeo unayopata yashirikishe kwenye kundi.
5. Kaa kwenye mchakato sahihi wa kile unachotaka kufikia na epuka usumbufu unaokuwa kikwazo kwako.

Makala ya ukurasa wa leo ni kuhusu gharama ambazo tayari unazilipa. Isome, weka maoni na nenda kachukue hatua. Fungua hapa; https://www.kisimachamaarifa.co.tz/2023/11/24/3250

Ukawe na siku bora kabisa ya leo, siku ya kukamilisha mawasiliano kwa hisia kali ili kueleweka kwa uhakika.

Kocha.