3254; Farasi wa kuchonga.
Rafiki yangu mpendwa,
Kama umewahi kuwaona watoto wakiwa kwenye mchezo ambao wamepanda farasi wa kuchonga, wanakuwa na furaha sana.
Wanaona wakiwa wamepanda farasi anayekwenda mbio, lakini kiuhalisia hakuna mahali wanakuwa wameenda.
Mbio zinakuwa nyingi, lakini wanakuwa wamebaki pale pale.
Hivyo pia ndivyo watu wazima wengi wanavyoshindwa kwenye maisha.
Wanaonekana wakiwa ni wachapa kazi sana, lakini hakuna hatua ambazo wanakuwa wanapiga kwenye kile wanachofanya, iwe ni kazi au biashara.
Wanaweza kuwa wanawahi kufika maeneo yao ya kazi kila siku na kuchelewa kutoka.
Wakawa pia wanafanya kazi kwenye siku zote saba za wiki bila hata kupumzika.
Miaka inakwenda na hakuna hatua kubwa wanazopiga, wanakuwa wanazidi kurudi nyuma kadiri muda unavyokwenda mbele.
Mwisho wanashindwa kabisa, kama wapo kwenye biashara inakufa na kama wameajiriwa wanaikosa kazi.
Mtu akiwaangalia watu hawa kwa nje anashindwa kabisa kuelewa nini kimewatokea.
Kwa sababu wanaonekana kuwa ni wachapa kazi sana, waliojitoa hasa.
Lakini inakuwaje wameshindwa vibaya kiasi hicho?
Kitu ambacho kwa nje hakionekani ni kwamba watu hao wanakuwa wametingwa na kazi ambazo ni feki.
Kazi ambazo hazina mchango kwao kupiga hatua kubwa.
Zinaweza kuonekana ni kazi za kuwachosha, lakini haziwapi fursa ya kupiga hatua zaidi.
Na hiyo ndiyo dhana ya farasi wa kuchonga kwa watu wazima.
Wanajiona wametingwa kweli kweli, lakini hakuna mahali wanaenda.
Kwenye ajira ni mtu kuhangaika na majukumu ambayo ni ya kusukuma karatasi kwenda mbele.
Haya ni majukumu ambayo hayana matokeo makubwa na mapya kwenye taasisi ambayo mtu anafanya kazi.
Bali ni majukumu ya kawaida tu, ambayo yanafanya mtu asionekane ni mvivu, lakini hayaleti matokeo yoyote mapya na makubwa.
Kwenye hali ya kawaida, watu hao wataendelea kuwa na kazi, siyo kwa sababu wana mchango kwenye taasisi, bali kwa sababu kuwafukuza inakuwa gharama kwa taasisi kuliko kubaki nao.
Hivyo licha ya kuwa mzigo, bado unakuwa unaweza kuvumilika.
Ni kwenye nyakati ngumu ambapo taasisi haiwezi tena kubeba mizigo ndiyo watu wa aina hiyo wanapoteza kazi zao.
Pale taasisi inapokuwa na sababu za msingi za kupunguza watu, wanaoanza kuondolewa ni wale ambao wanaonekana kufanya sana kazi, lakini hawana mchango kwenye ukuaji wa taasisi.
Kwenye biashara, farasi wa kuchonga ni pale mtu anapohangaika na majukumu ambayo hayana mchango wa moja kwa moja kwenye kuingiza kipato.
Hapa mtu anatingwa na majukumu mengi yaliyopo kwenye biashara, lakini yanakuwa hayaleti kipato moja kwa moja.
Kwa nyakati ambazo ni nzuri kibiashara, bado biashara inaweza kubaki hai, kwa sababu wateja wanaokuwepo wanaendelea kununua.
Wananunua siyo kwa sababu ya maajabu yoyote, bali kwa sababu wameshazoea kununua.
Ni mpaka pale yanapotokea mabadiliko yanayowaathiri wateja na wakashindwa kununua kama walivyokuwa wamezoea ndipo biashara inaathirika sana.
Athari hizo ndizo zinazoua biashara nyingi.
Lakini kifo kinakuwa kilianza muda mrefu, kilichotokea ni kumalizia tu.
Njia ya kuondokana na farasi wa kuchonga ni kutumia kanuni ya 80/20.
Kwa kanuni hiyo unahakikisha unaweka kipaumbele kikubwa kwenye majukumu yenye tija kuliko majukumu ya kawaida.
Asilimia 80 ya juhudi zako unaweka kwenye majukumu yanayoleta matokeo makubwa kama ni kwenye kazi au kuleta kipato moja kwa moja kwenye biashara.
Unapokuwa na majukumu 10 ya kutekeleza, 8 yanapaswa kuwa yale yanayoleta matokeo makubwa na mawili yanayoleta matokeo ya kawaida.
Unapokuwa na masaa 10 ya kufanya kazi, masaa 8 yanapaswa kuwa ya majukumu makubwa na masaa mawili ya majukumu ya kawaida.
Kufanya kwa namna nyingine yoyote, tofauti na hapo ni kuchagua kupanda farasi wa kuchonga.
Ufajiona upo mbio sana, unafanya kazi sana, lakini unakuwa umebaki pale pale, hakuna mahali unakuwa unaenda.
Achana na kazi feki na fanya kazi halisi zenye mchango mkubwa.
Kwenye ajira fanya majukumu yanayoleta matokeo makubwa na ya tofauti.
Kwenye biashara fanya zaidi matokeo yanayoleta wateja wapya na kukuza zaidi mauzo.
Muda ni wako, nguvu ni zako na umakini ni wako.
Ni wewe utachagua kama utapeleka rasilimali hizo kwenye farasi wa kuchonga au farasi halisi.
Swali muhimu kwako kujiuliza, kutafakari na kushirikisha hapa ni hili; ni farasi gani feki ambao umewapanda kwa muda mrefu na kukwama eneo moja bila kukua?
Ni farasi gani halisia ambao umechagua kuwapanda sasa ambao watakupeleka kwenye matokeo makubwa zaidi?
Shirikisha majibu yako kwenye maoni hapo chini.
#NidhamuUadilifuKujituma
#AfyaUtajiriHekima
#KaziUpendoHuduma
#UpekeeUdadisiUbunifu
#UshirikianoUtegemeanoUwajibikaji
#BilioneaMafunzoni
#NajengaBiashara
#HakunaKingineMuhimu
#LazimaNitoboe
#NawekaKaziNifanikiwe
Wakati mwingine kwenye kazi najikuta nafanya majukumu ambayo hayana mchango wa moja kwa moja kwenye majukumu yangu ila ni ambayo viongozi wangu wanaamini naweza kuyatekeleza.Hii naiona kama farasi feki kwani yananiweka bize na mwisho wa siku hayana matokeo yoyote.
Ila kwenye biashara najitahidi kufanya majukumu kama kujenga timu kuwasiliana na wateja na kutembelea kitu ambacho naona ni farasi halisi katika ukuaji wa biashara.
LikeLike
Vizuri sana, epuka farasi wa kuchonga kwenye biashara yako.
Na kwenye kazi, shauriana na viongozi wako namna bora ya kutumia muda wako ili kuzalisha matokeo makubwa.
LikeLike
Farasi wa kuchonga: kusukumana na ndugu na hata familia kwenye majukumu ambayo ni wajibu wao na wana uwezo wa kuyakabili. Nimeamua kushuka kutoka farasi huyu feki. Farasi wangu halisia ni kukuza biashara ya ufugaji Kuku na kilimo cha mboga na matunda, kukuza akiba na uwekezaji, kuwa na furaha muda wote.
LikeLike
Umefanya maamuzi bora kabisa, yasimamie.
LikeLike
Farasi wa kuchonga. Ni pale unapobeba mzigo mkubwa wa majukumu ambayo hayana tija yoyote wala hayana faida zaidi ya kukutia hasara na kukurudisha nyuma zaidi
Farasi wakutembea nae ni yule anayeweza kukutoa hatua nyingine na kukupeleka hatua nyingine. Fanya majukumu ambayo yanaleta matokeo mazuri mazuri kwenye biashara, fuatilia wateja saka wateja wapya Kila siku
LikeLike
Vizuri sana John, nenda na farasi halisi na siyo wa kuchonga.
LikeLike
Farasi feki niliyepanda ni kuweka nguvu kwenye majukumu rahisi yanayoweza kufanywa na wengine.
Farasi halisi kwa sasa ni kuweka nguvu kubwa kwenye mauzo na kwenye kuajiri watu sahihi.
LikeLike
Kupambania mauzo na kuajiri watu sahihi ni mambo ambayo ukiyawekea nguvu yataleta matokeo makubwa sana.
LikeLike
Kupanda farasi halisi ni kutumia kanuni ya 80/20 itapunguza mambo yasio na msingi na kudeal na mambo yenye kuleta matokeo mazuri
Asante sana
LikeLike
Siri kuu ya uzalishaji na ufanisi ni kutumia vizuri kanuni ya 80/20.
LikeLike
Farasi Feki ni kufurahia projrct zinakuja kwa wingi bila kuhakiki kiwa faida ya kwenye karatasi itakuja kweli baadae wateja wanabadilika hata kati kati ya project.
Farasui halisi nahakikisha napata faida na nahkikisha mteja anaelewa na kufuata makubaliano nikiona tu kuna sintofahamu naibua hoja mara moja na nikiona hamna maslahi nipo tayari kusimamisha project mara moja.
LikeLike
Umegusa angle muhimu sana ambayo kwenye biashara za huduma wengi wanaipuuza.
Imezoeleka mteja kuchagua mfanyabiashara gani wa kununua kwake.
Lakini inasahaulika kwamba hata biashara ina wajibu wa kuchagua mteja gani itamuuzia.
Kumuuzia kila mtu ni kutafuta matatizo makubwa.
LikeLike
“Muda ni wako, nguvu ni zako na umakini ni wako.
Ni wewe utachagua kama utapeleka rasilimali hizo kwenye farasi wa kuchonga au farasi halisi.”
LikeLike
Ndiyo uzuri wa hizo rasilimali muhimu, una uhuru wa kuzitumia vile unavyotaka.
LikeLike
Asante sana kocha
Farasi feki ni kuhangaika na majukumu rahisi ambayo kila mtu anaweza kufanya na hayazalishi matokeo makubwa.
Farasi halisi ni majukumu muhimu yanayonayoleta ukuaji katika biashara kama vile masoko na mauzo jukumu langu ni kuweka umakini katika mauzo na masoko ili biashara yangu ikue.
LikeLike
Vizuri, pambana na farasi halisi.
LikeLike
Farasi Feki ambao nimepanda sasa kuhangaika na Kelele za watu badala.
Farasi halisi ambae nampanda sasa ni kusaka wateja wapya na kupigia simu wateja wa kamili kila siku.
LikeLike
Vizuri.
LikeLike
Kutingwa na kazi feki ambazo hazina mchango wowote katika malengo yako ni sawa na lujiandaa kuiua boashata hiyo
LikeLike
Kabisa.
LikeLike
Farasi feki niliyependa ni kuendelea kuwafikiria watendaji wasiotimiza majukumu yao na Farasi wa kumpanda ni kupambana kutafuta wateja na kutafuta wafanyakazi bora watakaosababisha biashara ikue
LikeLike
Wateja na timu bora humo ndipo pa kukaa kwa uhakika.
LikeLike
Farasi wa kuchongwa ni wengi sana kuliko walio halisi.
LikeLike
Kabisa.
LikeLike
Farasi feki kutofanya vitu kwa umakini na weledi,
Farasi sahihi kukaa kwenye mchakato wa mauzo, kujifunza na kuchukua hatua sahihi
LikeLike
Tukae kwenye farasi halisi na kuachana na feki.
LikeLike