3255; Uhakika wa ushindi.
Rafiki yangu mpendwa,
Kuna watu ambao wana uhakika wa ushindi kwenye maisha yao.
Siyo kwa sababu mambo yanakuwa rahisi ila kwa sababu wao wanakuwa wagumu kiasi kwamba hakuna kinachoweza kuwazuia kufanikiwa.
Maisha yanaweza kuwachelewesha.
Maisha yanaweza kuwachanganya.
Lakini ile nia yao ya ushindi haifi kamwe.
Ni nia hiyo ndiyo inayoendelea kuwasukuma mpaka kupata ushindi mkubwa.
Nia kubwa ya ushindi wanayokuwa nayo ndiyo inawapa msukumo wa kuchukua hatua kubwa bila kuchoka.
Kuchukua hatua kubwa bila ya kuchoka kunawakutanisha na fursa mbalimbali ambazo zinachangia kwenye mafanikio wanayoyataka.
Watu hao wanapopata mafanikio makubwa, kwa nje inaonekana kama ni rahisi.
Inaweza kuonekana pia ni kama bahati.
Lakini ambacho wengi hawaoni ni yale yanayokuwa yanaendelea nyuma ya pazia kwa kipindi kirefu kabla ya mafanikio hayo.
Haijalishi mtu anakuwa anapotia magumu na changamoto nyingi kiasi gani, swala la kupata ushindi halifutiki kwenye fikra zao.
Wanajua kwa hakika kwamba watapata ushindi na hilo kwao linakuwa swala la muda tu.
Je wewe ni uhakika kiasi gani umejiwekea kwenye kupata ushindi unaoutaka?
Umejitoa kiasi gani kwenye kufanya kwa mwendelezo bila ya kuacha?
Unakabilianaje na magumu na changamoto unazokutana nazo?
Majibu sahihi ya maswali hayo ndiyo yanakupa picha ya uhakika wa mafanikio kwako.
#NidhamuUadilifuKujituma
#AfyaUtajiriHekima
#KaziUpendoHuduma
#UpekeeUdadisiUbunifu
#UshirikianoUtegemeanoUwajibikaji
#BilioneaMafunzoni
#NajengaBiashara
#HakunaKingineMuhimu
#LazimaNitoboe
#NawekaKaziNifanikiwe
Ushindi ni lazima kwa kua sijaona chochote cha kunizuia na hapa sasa naeleekea kufanya mikakati ile migumu ambayo yatapelekea mimi kutelezea kwenye ushindi
Ushindo kwangi ni lazima ntapambania hadi niupate na kuendelea kwenda juu zaidi
LikeLike
Safi sana, hakuna kushindwa.
LikeLike
Kuchukua hatua kubwa bila kuchoka na kwa mwendelezo ndiyo kunawakutanisha watu na fursa mbalimbali ambazo zinachangia kwenye mafanikio wanayo yataka.
LikeLike
Hakika.
LikeLike
Ushindi ni lazima licha ya kuwa na changamoto mbalimbali.
Asante sana Kocha Dr Makirita Amani
LikeLike
Ndiyo.
LikeLike
Haijalishi nini nitapata mafanikio makubwa ninayoyataka ama nitakufa nikiwa nayapambania.
LikeLike
Kabisa, unakutana na mafanikio kwenye mapambano.
LikeLike
Nimejitoa kufa na kupona Ili kupata ninachokitaka
Mtazamo chanya siku zote kuwa magumu ni fursa ya kukua
Nakuja mgumu kuliko magumu yenyewe
LikeLike
Safi sana, kujitoa ni muhimu ili kupata kile unachotaka.
LikeLike
ushindi ni lazima upatikane sababu changamoto ndiyo zinazanifanya ni zidi kuchukua hatua kubwa zaidi na kuweka nia zaidi ya ushindi bila kuchoka
LikeLike
Hakika.
LikeLike
Asante Kocha,
Ninatambua nikikaa kwenye mchakato sahihi na kwa msimamo, ushindi ni swala la muda tu.
LikeLike
Kabisa.
LikeLike
Kabiliana na magumu na mwisho wa siku ushindi utakuwa wako.
Asante
LikeLike
Kabisa.
LikeLike
“Maisha yanaweza kuwachelewesha.
Maisha yanaweza kuwachanganya.
Lakini ile nia yao ya ushindi haifi kamwe.
Ni nia hiyo ndiyo inayoendelea kuwasukuma mpaka kupata ushindi mkubwa.”
LikeLike
Kabisa.
LikeLike
Uhakika wa ushindi ni 100%
LikeLike
Hilo halina ubishi.
LikeLike
Nina uhakika pasipo na shaka nitapata ushindi mkubwa ninaoutaka kwa kua Nina nia thabiti ushindi kwangu ni swala la muda tu nitapambana mwanzo mwisho adi nipate ushindi.
Katika safari yangu ya kutafuta ushindi nitakutana na magumu na changamoto mbalimbali nitapambana na kukabiliana nazo ili nifikie ushindi mkubwa bila kukata tamaa.
LikeLike
Safi sana na kila la kheri.
LikeLike
USHINDI NI WA KWANGU LAZIMA NIUPATE HATA YANGEKUJA MAMBO YA KUKATISHA TAMAA KIASI GANI NITAPAMBANA MPAKA NIPATE
Je wewe ni uhakika kiasi gani umejiwekea kwenye kupata ushindi unaoutaka?
MINA UHAKA ASILIMIA MIA MOJA
Umejitoa kiasi gani kwenye kufanya kwa mwendelezo bila ya kuacha?
SIJIHURUMII NAPAMBANA KUFA KUPONA
Unakabilianaje na magumu na changamoto unazokutana nazo?
MAGUMU YAKIJA NAFURAHI KWASABABU YANANIKOMAZA, NAANGALIA CHANZO CHA MAGUMU NAJIFUNZA KUTOKANA NA MAGUMU HAYO, NA KISHA NATAFUTA NJIA YA KUTOKEA
LikeLike
Safi sana, kaa humu kwa uhakika. Ushindi ni lazima.
LikeLike
Ile picha kubwa ya mafanikio niliyonayo ndiyo inanifanya nisikatishwe tamaa na lolote gumu linalokuja mbele yangu kwani najua kwenye gumu linanifanya nijione nafanya kitu cha tofauti na hivyo ndivyo ukuaji unaotakiwa kingine ndio njia sahihi ya kuelekea kwenye mafanikio yangu makubwa. 🙏
LikeLike
Vizuri sana.
LikeLike
Bila kujali changamoto ninazopitia Nia yangu ya kufanikiwa bado iko pale pale.
LikeLike
Safi sana.
LikeLike
Kupata ushindi ni uhakika ni swala la muda tu kama tutaendelea kufanya kwa msimamo kwa muda mrefu bila kuacha.
LikeLike
Kabisa.
LikeLike
Hapa kunahitajika kitu zaidi ya hamasa. NIDHAMU KALI YA KUAMUA NA KUFANYA BILA KUACHA
LikeLike
Kabisa.
LikeLike
Ushindi kwangu ni wa uhakika wala sina mashaka, changamoto ninazokutana nazo kwangu ni fursa ya ukuaji
LikeLike
Safi na kila la kheri.
LikeLike