💯KCM2324031; Machaguo.
Tumejipata, Tunaachilia Breki.
#JumatanoYaUwajibikaji
Mwanamafanikio,
Mwaka wa mafanikio 2023-2024 tumejipata kwa kuchagua kufanyia kazi kwa ukubwa kitu kimoja mpaka kitupe mafanikio makubwa tunayoyataka.
Tumeachilia breki kwa kufanyia kazi maeneo sita; MALENGO, KUJIKUBALI, UWAJIBIKAJI, UBUNIFU, MAWASILIANO na UTULIVU ili kujipa uhakika wa kufanya makubwa.

💯 Neno la leo; Machaguo.
Leo ikiwa ni #JumatanoYaUwajibikaji tunaona jinsi ambavyo unawajibika kwa machaguo unayofanya kwenye maisha yako.
Upo hapo ulipo leo kutokana na machaguo uliyoyafanya siku za nyuma.
Na machaguo unayoyafanya leo, ndiyo yanayojenga matokeo ya kesho.
Huo ndiyo mzunguko utakaoenda nao kwa kipindi chote cha maisha yako.
Huwa ni rahisi kutafuta watu wa kuwalaumu na kuwalalamikia kwenye matokeo tunayokuwa tumeyapata.
Tunawaona watu hao wanakuwa na mchango mkubwa kwenye matokeo hayo.
Lakini tunakuwa tumesahau kwamba sisi ndiyo tuliofanya machaguo makuu ambayo ndiyo yametufikisha tulipofika.
Hakuna yeyote aliyetulazimisha kufanya chochote.
Ni machaguo yetu wenyewe ndiyo yanakuwa yamechangia kwenye matokeo tunayokuwa tumeyapata.
Tunapaswa kuwajibika kwenye matokeo yote tunayoyapata, kwa kuangalia ni machaguo gani yaliyoleta matokeo hayo.
Ni kupitia kuwajibika ndiyo tunaweza kuona fursa za kuboresha zaidi machaguo yetu na hatua tunazochukua.
Ukikwepa kuwajibika, jua pia umekwepa mafanikio makubwa unayotaka kuyapata.
Hivyo usikubali kabisa kulalamika au kulaumu wengine kwa chochote kile kwenye maisha yako.
Wajibika kwa kila kitu kwenye maisha yako na utaweza kupata mafanikio makubwa.
💯Hatua za kuchukua leo;
1. Andika ahadi yako ya mwaka wa mafanikio 2023-2024 kwa mtiririko wa NINI, LINI, WAPI, KWA NINI, NANI, VIPI na HISIA kisha weka kwenye kundi.
2. Soma kurasa 10 za kitabu cha MTAALA WA UTAJIRI na shirikisha uliyojifunza kwenye kundi.
3. Chukua hatua kwenye yale ambayo umeshajifunza na shirikisha kwenye kundi.
4. Matokeo unayopata yashirikishe kwenye kundi.
5. Kaa kwenye mchakato sahihi wa kile unachotaka kufikia na epuka usumbufu unaokuwa kikwazo kwako.
Makala ya ukurasa wa leo ni kuhusu uhakika wa ushindi. Isome, weka maoni na nenda kachukue hatua. Fungua hapa; https://www.kisimachamaarifa.co.tz/2023/11/29/3255
Ukawe na siku bora kabisa ya leo, siku ya kuwajibika kwa machaguo uliyofanya huko nyuma na kukufikisha hapo ulipo leo na kufanya machaguo mazuri leo ili siku zijazo ziwe bora zaidi.
Kocha.
💯