💯KCM2324032; Kinzani.

Tumejipata, Tunaachilia Breki.

#AlhamisiYaUbunifu

Mwanamafanikio,

Mwaka wa mafanikio 2023-2024 tumejipata kwa kuchagua kufanyia kazi kwa ukubwa kitu kimoja mpaka kitupe mafanikio makubwa tunayoyataka.

Tumeachilia breki kwa kufanyia kazi maeneo sita; MALENGO, KUJIKUBALI, UWAJIBIKAJI, UBUNIFU, MAWASILIANO na UTULIVU ili kujipa uhakika wa kufanya makubwa.

Kuna vifungo vya kujitakia ambavyo vinakukwamisha usifanikiwe. Mojawapo ni uraibu wa mitandao ya kijamii, hii imewafanya wengi sana kuwa watumwa. Pata kitabu cha EPUKA UTUMWA WA KIDIJITALI uweze kurudisha uhuru wako. Wasiliana sasa na 0678977007



💯 Neno la leo; Kinzani.

Leo ikiwa ni #AlhamisiYaUbunifu tunaona jinsi ambavyo ubunifu unatokana na mawazo kinzani ambayo mtu anakuwa nayo.

Akili zetu binadamu huwa zina uwezo mkubwa sana kuliko ambavyo tunautumia.

Moja ya uwezo huo mkubwa ni kushikilia mawazo kinzani kwa wakati mmoja. Yaani unakuwa na mawazo mawili yanayokinzana lakini unaenda nayo yote mawili.

Ni kupitia kushikilia mawazo hayo yanayokinzana ndiyo ubunifu huwa unaliwa.
Ule mgogoro unaotokana na mawazo kinzani anayokuwa nayo mtu ndiyo unazalisha ubunifu wa kipekee.

Hili la kushikilia mawazo kinzani kwa wakati mmoja siyo rahisi. Wengi huwa hawawezi kulifanyia kazi.
Ndiyo maana wanapojikuta wakiwa kwenye hali inayowapa mawazo yanayokinzana na kile ambacho tayari wanaamini, huwa wanapuuza mawazo hayo mapya na kukaa kwenye kile ambacho tayari wanaamini.

Vitu vyovyote ambavyo watu wamevishikilia kwa imani kali kiasi cha kupuuza mawazo kinzani huwa havina ubunifu kwa watu hao.
Mfano ni dini, ushirikina, itikadi, michezo na vingine vya aina hiyo.

Kwa upande wa pili, vitu kama sayansi na tafiti mbalimbali vimekuwa vinakuja na ubunifu mpya kila wakati.
Hiyo ni kwa sababu ya mazingira yanayokuwepo, ambayo yanaruhusu mawazo kinzani kuwepo kwa wakati mmoja.

Mazoea ni mazuri kwenye kutekeleza kile kinachopaswa kufanyika.
Lalini ili kuja na vitu vipya, ubunifu haukwepeki.
Na hapo lazima mtu uwe tayari kuwa na mawazo kinzani kwa muda mrefu.

Ubunifu ni moja ya njia za kuachilia breki ambazo zimekuwa kikwazo kwa wengi kupiga hatua kubwa kwenye maisha yao.
Wewe anza kwa kushikilia mawazo kinzani kwenye fikra zako na ona jinsi yote yalivyo na manufaa.
Hapo unafungua nafasi ya mawazo hayo kinzani kuzalisha kitu cha tofauti kabisa.

💯Hatua za kuchukua leo;
1. Andika ahadi yako ya mwaka wa mafanikio 2023-2024 kwa mtiririko wa NINI, LINI, WAPI, KWA NINI, NANI, VIPI na HISIA kisha weka kwenye kundi.
2. Soma kurasa 10 za kitabu cha MTAALA WA UTAJIRI na shirikisha uliyojifunza kwenye kundi.
3. Chukua hatua kwenye yale ambayo umeshajifunza na shirikisha kwenye kundi.
4. Matokeo unayopata yashirikishe kwenye kundi.
5. Kaa kwenye mchakato sahihi wa kile unachotaka kufikia na epuka usumbufu unaokuwa kikwazo kwako.

Makala ya ukurasa wa leo ni kuhusu njia mbili za kuyaendea maisha. Isome, weka maoni na nenda kachukue hatua. Fungua hapa; https://www.kisimachamaarifa.co.tz/2023/11/30/3256

Ukawe na siku bora kabisa ya leo, siku ya kushikilia mawazo kinzani kwenye fikra zako ili uweze kuja na ubunifu mpya.

Kocha.
💯