3257; Kitakachokuondoa kwenye mchezo haraka zaidi.
Rafiki yangu mpendwa,
Haya maisha ni mchezo mmoja mkubwa sana, ambao ndani yake kuna michezo mingi midogo midogo.
Kazi ni mchezo ndani ya mchezo wa maisha. Kadhalika biashara, fedha, uwekezaji, mahusiano na mengine yote tunayofanya kwenye maisha.
Kwenye michezo, pale mtu anaposhindwa huwa kunakuwa na kasumba ya kulaumu upande shindani kutumia njia zisizo sahihi au kupendelewa ndiyo maana upande huo ukashinda.
Lakini hizo huwa ni kauli za kujifariji tu, ukweli ni kwamba upande unaoshinda unakuwa umejiandaa vyema kushinda wakati upande unaoshindwa unakuwa ulishashindwa kabla hata ya kuanza.
Kwenye mchezo wa maisha, kuna kosa moja ambalo limekuwa linapelekea wengi kushindwa kabla hata hawajakutana na ushindani wa nje.
Yaani wanaingia uwanjani wakati tayari wameshashindwa.
Na hilo ndiyo limekuwa chanzo cha wengi kushindwa kwenye maisha yao.
Kosa hilo ni kukosa umakini (fokasi) kwenye kile ambacho mtu anafanya. Hili ni kosa linaloanzia ndani ya mtu mwenyewe lakini lenye nguvu ya kumtoa mtu kwenye mchezo kabisa.
Kufokasi imekuwa ni kitu kigumu kwenye zama hizi kutokana na vitu vingi vinavyolenga kunasa umakini wetu.
Kwenye muda mchache unaokuwa nao, kunakuwa na mambo mengi ambayo unataka kuyafanya.
Hilo linapelekea kuutawanya muda wako kwenye mambo mengi ila yasiyokuwa na tija.
Matokeo yake ni mtu kushindwa kuzalisha matokeo makubwa kwenye kitu chochote kile.
Kufokasi imekuwa ni kitu kigumu kwa walio wengi, kwa sababu uelewa wa watu kuhusu kufokasi ni tofauti na uhalisia wa kufokasi.
Wengi wanachoelewa kuhusu kufokasi ni kupeleka umakini wa mtu kwenye mambo yaliyo muhimu na kuachana na yasiyokuwa muhimu.
Lakini ambapo wengi wanakuja kuanguka ni pale mambo mengi yanapokuwa yote ni muhimu.
Huwa wanasema kama kila kitu ni muhimu, basi hakuna kilicho muhimu.
Maana halisi ya kufokasi ni kusema HAPANA kwenye vitu ambavyo ni muhimu, ili kupeleka umakini wako wote kwenye kitu kimoja kilicho muhimu zaidi.
Kufokasi ni kusema HAPANA kwenye vitu vingi vizuri ili kupeleka umakini wako wote kwenye kitu kimoja bora.
Hapo ndipo ugumu wa kufokasi unapoanzia, kwa sababu wengi wanakuwa hawana ujasiri wa kusema HAPANA kwenye vitu ambavyo tayari vina manufaa fulani kwao.
Kufokasi ni kuwa tayari kupoteza kabla ya kupata. Sasa kwa sababu watu wengi wana mtazamo wa uhaba, huwa hawapo tayari kupoteza hata kidogo. Kukosa utayari wa kupoteza kunawapeleka kujikosesha kupata makubwa zaidi.
Ushindi wako kwenye eneo lolote la maisha yako unaanzia kwenye uwezo wako wa kufokasi.
Ni pale unapoweza kuweka umakini wako wote kwenye kitu kimoja na kukifanya kwa ukubwa kuliko kuutawanya kwenye vitu vingi na kupata matokeo ya kawaida.
Kufokasi siyo kitu ambacho unaweza kuamua kuwa nacho au kutokuwa nacho. Bali kufokasi ni aina ya maisha ambayo mtu unachagua kuyaishi.
Bila ya kugeuza kufokasi kuwa mfumo wako mzima wa maisha, utalaghaiwa na kujikuta umeshahama kwenye yale muhimu zaidi kwako na kwenda kwenye yasiyokuwa muhimu.
Changamoto kubwa sana kwenye kufokasi ni kwamba kila mtu anawinda umakini wako.
Na wengi wa hao ambao wanafanya hivyo, wanazo mbinu za kukushawishi unase kwenye mitego yao.
Bila ya kuwa katili kwenye kusema HAPANA kwa yote yasiyokuwa muhimu kwako, hutaweza kufanya makubwa.
Ni lazima uwe tayari kusema HAPANA kwa yote yasiyokuwa muhimu kwako, hata kama kufanya hivyo kunawaumiza wengine.
Kama unajaribu kuyaishi maisha yako ili kumfurahisha kila mtu, utaishia kushindwa vibaya sana. Kwani hutawaridhisha watu wote hata ufanye nini. Lakini zaidi, utajiumiza zaidi wewe mwenyewe pale unapojaribu kuwaridhisha wengine.
Fokasi kwa kupeleka umakini wako wote kwenye kitu kimoja kilicho muhimu zaidi kwako na kusema HAPANA kwa vitu vingine vyote, hata kama vinaonekana ni muhimu.
#NidhamuUadilifuKujituma
#AfyaUtajiriHekima
#KaziUpendoHuduma
#UpekeeUdadisiUbunifu
#UshirikianoUtegemeanoUwajibikaji
#BilioneaMafunzoni
#NajengaBiashara
#HakunaKingineMuhimu
#LazimaNitoboe
#NawekaKaziNifanikiwe
Kukosa umakini fpcus ni mbaya sana
LikeLike
Nimefahamu kuwa kumbe kufocus ni kusema hapana kwa yale muhimu ili kufanya yale ya muhimu zaidi.Asante kocha
LikeLike
Karibu
LikeLike
Kabisa.
LikeLike
Fokasi kwenye kitu kimoja muhimu.
LikeLike
Ndiyo.
LikeLike
Asante sana kocha ni ukweli mtupu focus ndio sehemu muhimu sana kwenye maisha yetu,nitauza gas na vifaa vyake kwa miaka kumi bila kuacha hilo ndilo nimechagua kulifanya.
LikeLike
Safi sana, pambania hapo, kuna fursa na ukuaji mkubwa.
LikeLike
Asante Kocha,
Ili kujihakikishia ninafokasi yale ya muhimu kwangu nitaiishi kanuni ya 8O/2O; Pareto principle
LikeLike
80/20 ndipo pa kusimamia ili kufanya makubwa.
LikeLike
Nitajitahidi kuweka umakini wangu kwenye jambo moja muhimu tu.
LikeLike
Safi sana.
LikeLike
Fokasi kwenye kitu kimoja Kaa hapo Kwa muda mrefu mafanikio yatakuwa Yako
Asante sana
LikeLike
Hakika, tukae humo.
LikeLike
Kama unajaribu kuyaishi maisha yako ili kumfurahisha kila mtu, utaishia kushindwa vibaya sana. Kwani hutawaridhisha watu wote hata ufanye nini. Lakini zaidi, utajiumiza zaidi wewe mwenyewe pale unapojaribu kuwaridhisha wengine.
LikeLike
Kabisa.
LikeLike
Umakini ni muhimu sana kwenye Kila sehemu au kwenye Kila jambo unalopaswa kulifanya
Focus kwenye jambo lenye faida na lenye kuleta tija kwenye maisha
LikeLike
Kabisa.
LikeLike
Kukosa umakini ( fokasi) kwenye kile ambacho mtu anafanya.Hili ni kosa linaloanzia ndani ya mtu mwenyewe,Lkn lenye nguvu ya kumtoa mtu kwenye mchezo kabisa.
🙏🙏🙏
LikeLike
Kabisa.
LikeLike
Asante kocha kwa makala ya Leo kuanzia sasa nitafokasi kwa kupeleka umakini wangu wote kwenye kitu kimoja kilicho muhimu zaidi kwangu na kusema HAPANA kwa vitu vingine vyote ata kama vinaonekana muhimu.
LikeLike
Vizuri sana.
LikeLike
kujaribu kuwaridhisha wengine ni kujiumiza wewe mwenyewe.
LikeLike
Kabisa.
LikeLike
ni kweli wengi tunashindwa kutimiza malengo kwasababu ya kukosa focus kwenye kile tunachofanya
LikeLike
Tuepuke sana hilo.
LikeLike
Kutaka kumfurahisha Kila mtu ni kujiumiza Mimi mwenyewe, nasema hapana hata kama niyawafanya wajisikie vibaya. Siwezi kufanikiwa na kuwa na focus kama nitataka kumfurahisha Kila mtu
LikeLike
Kabida.
LikeLike
Nitasema hapana kwa chochote ambacho hakina mchango kwenye mafanikio yangu
LikeLike
Safi.
LikeLike
Huu ni ujumbe muhimu!!
LikeLike
Ndiyo
LikeLike
Bila ya kugeuza kufokasi kuwa mfumo wangu mzima wa maisha nitalaghaiwa na kujikuta nimeisha hama kwenye yale muhimu zaidi kwangu na kwenda kwenye yasiyo kuwa muhimu. Bila yakuwa katili kwenye kusema HAPANA kwa yote yasiyo kuwa muhimu kwangu sitaweza kufanya makubwa. Ni lazima niwe tayari kusema HAPANA kwa yote yasiyo kuwa muhimu kwangu ,hata kufanya hivyo kuna waumiza wengine. Nitafokasi kwa kupeleka umakini wangu wote kwenye kitu kimoja kilicho muhimu zaidi kwangu na kusema HAPANA kwa vitu vingine vyote hata kama vinaonekana ni muhimu.
LikeLike
Hakika
LikeLike
Ili nisishindwe kwenye maisha haya nitafokasi kwa kusema HAPANA kwenye vitu vingi vizuri ili kupeleka umakini wote kwenye kitu kimoja bora.
LikeLike
Ndiyo.
LikeLike