3258; Ambayo wengine hawafanyi.
Rafiki yangu mpendwa,
Watu wamekuwa wanalalamika kwenye zama hizi ushindani umekuwa mkali sana kwenye jambo lolote.
Hiyo ni kwa sababu kuna watu wengi wanaokuwa wanafanya kila jambo.
Ni kweli kwamba kuna watu wengi wanaokuwa wanafanya chochote ambacho mtu umechagua kufanya.
Lakini siyo kweli kwamba ushindani ni mkali.
Tena kinyume cha hilo ndiyo ukweli, kwamba kadiri watu wengi wanavyokuwa wanafanya kitu, ndivyo ushindani unavyokuwa mdogo.
Kinachopelekea ushindani kushuka pale watu wengi wanapofanya kitu ni ile tabia ya kuigana na kufuata mkumbo.
Watu huwa wanapenda kuiga kile kinachofanywa na wengi kwa kuona ndiyo kitu sahihi kufanya.
Matokeo yake wote wanaishia kupata matokeo yanayofanana.
Kama unataka kujenga mafanikio makubwa kwenye maisha yako, fanya kile kinachofanywa na wengi, lakini kifanye kwa namna ambayo hao wengi hawakifanyi.
Angalia yale mambo ambayo wengi wamekuwa hawapendi kuyafanya kwa sababu ya ugumu wake, kisha wewe yafanye hayo.
Ni kwa njia hiyo ndiyo unaweza kutoa thamani kubwa zaidi na kupata matokeo ya tofauti na wengine.
Tuchukue mfano wa biashara ili tuweze kuelewana vizuri.
Kutokana na urahisi wa watu kuingia kwenye biashara, hata kama hawana mtaji mkubwa au eneo la kufanyia biashara, watu wamekuwa wanaona ushindani ni mkali.
Kwa kuwa watu wanaweza kutumia mitandao ya kijamii kama ndiyo maduka yao, wengi wanafanya hivyo.
Pamoja na urahisi huo, bado wengi hawapati matokeo makubwa. Hiyo ni kwa sababu wanafanya vitu rahisi na vinavyofanywa na kila mtu.
Kwenye huu mfano wetu wa kufanya biashara kwa kutumia mitandao ya kijamii, wengi huwa wanaposti bidhaa zao kisha kusubiri wateja wawatafute.
Wanafurahi pale wanapoona kile walichoposti kimeonekana na wengi.
Lakini mauzo, ambayo ndiyo kitu muhimu zaidi hayawi ya kuridhisha.
Sasa basi, kama mtu ataingia kwenye biashara hiyo hiyo ya kuuza vitu kwa mtandao na kufanya kwa utofauti, atapata matokeo makubwa zaidi.
Badala ya kusubiri wateja waje, mtu anachukua hatua ya kuwafikia kule walipo na kuwajulisha kuhusu uwepo wa biashara na hata kuwashawishi kununua.
Kwa mtu kwenda hatua ya ziada, kuwatembelea wateja au kuongea nao kwenye simu ataweza kufanya makubwa zaidi.
Kupata matokeo ya tofauti na yale ambayo wengi wanapata, angalia ni vitu gani ambavyo wengi hao wanakwepa kuvifanya kisha vifanye kwa uhakika na ubora wa hali ya juu.
Vitu hivyo ndiyo vimeshikilia mafanikio yako.
Ndiyo vitu vitakavyokutenganisha na ushindani mkubwa na kukufanya uwe wa kipekee.
Fanya yale ambayo wengine hawatafanyi na utaweza kupata matokeo ambayo wengine hawayapati.
Hayo ndiyo matokeo yanayokutenga na ushindani na kukupa mafanikio makubwa.
#NidhamuUadilifuKujituma
#AfyaUtajiriHekima
#KaziUpendoHuduma
#UpekeeUdadisiUbunifu
#UshirikianoUtegemeanoUwajibikaji
#BilioneaMafunzoni
#NajengaBiashara
#HakunaKingineMuhimu
#LazimaNitoboe
#NawekaKaziNifanikiwe
Ni kweli ushindani ni mdogo sana.
LikeLike
Hakika
LikeLike
Nafanya Yale magumu ambayo wengine hawafanyi Ili kupata matokeo makubwa
LikeLike
Vizuri.
LikeLike
Ili upate matokeo ya tofauti, unapaswa kufanya yale ambayo wengine hawako tayari kufanya.
Asante sana Kocha Dr Makirita Amani.
LikeLike
Ndiyo
LikeLike
Kupata matokeo ya tofauti na yale ambayo wengi wanapata, angalia ni vitu gani ambavyo wengi hao wanakwepa kuvifanya kisha vifanye kwa uhakika na ubora wa hali ya juu.
LikeLike
Hakika
LikeLike
Nitafanya ambayo wengi hawafanyi ili kuepuka ushindani
LikeLike
Vizuri
LikeLike
Asante kocha.
Umeniongezea kitu kikubwa
LikeLike
Karibu
LikeLike
Ni kweli yale ambayo wengine hawafanyi ndiyo yanatofautisha watu
LikeLike
Hakika
LikeLike
Fanya ambayo wengine hawafanyi na utapata matokeo ambayo hawayapati
Asante sana
LikeLike
Hakika
LikeLike
Asante Kocha,
Nimejifunza ili nipate matokeo ya tofauti na wengine ninapaswa kufanya kwa uhakika na ubora wa hali ya juu yale ambayo wao wanakwepa kuyafanya.
LikeLike
Karibu.
LikeLike
Kufanya kwa upekee na utofauti
LikeLike
Ndiyo
LikeLike
Asante sana kocha, nitajitahidi kufanya kila ninachojihusisha nacho kwa utofauti.
LikeLike
Kila la kheri.
LikeLike
Asante Kocha kwa hilo. ni muhimu kuweka upekee kwenye biashara zetu
LikeLike
Hakika
LikeLike
Kwa kuwa nataka kujenga mafanikio makubwa kwenye maisha yangu, nitafanya kile kinachofanywa na wengi lakini kwa namna ya tofauti. nitaangalia yale ambayo wengi wamekuwa hawapendi kuyafanya kwa sababu ya ugumu wake na mimi kuyafanya.
LikeLike
Ndiyo
LikeLike