3259; Akili ya kuvuka barabara.
Rafiki yangu mpendwa,
Kwenye maisha huwa kuna vitu ambavyo kila mtu mwenye akili timamu anatakiwa kuwa anavijua, hata kama hajafundishwa au hana akili kubwa ya kuving’amua.
Vitu hivyo vinakuwa vinahitaji mtu kutumia tu akili ya kawaida (common sense) kuvielewa na kuvifanyia kazi.
Kwa maneno mengine huwa tunaita hii akili ya kawaida ni akili ya kuvuka barabara. Huhitaji kufundishwa na kukumbushwa kila mara kwamba kabla ya kuvuka barabara lazima uangalie pande zote mbili. Na kama kuna chombo kinachokuja kwa kasi na kipo karibu, unasubiri kwanza kipite ndiyo uweze kuvuka.
Watu wengi wanaoshindwa kwenye maisha huwa wanadhani mtu unahitaji kuwa na akili kubwa sana kufanikiwa. Lakini wapo watu wengi wenye akili kubwa sana na hawana mafanikio makubwa.
Kumbe basi, mafanikio makubwa kwenye maisha yanatokana na matumizi ya akili ya kawaida.
Hiyo ina maana kwamba kama mtu amekuwa anaweza kuvuka barabara bila ya kugongwa na vyombo vya usafiri, ana uwezo wa kutosha kupata mafanikio makubwa.
Kuna akili nyingi za kawaida kwenye maisha, hapa tunakwenda kuangalia tatu ambazo unapaswa kuziishi muda wote, bila ya kusahau wala kusubiri kukumbushwa.
Ya kwanza ni siri kuu ya mafanikio kwa ujumla, ambayo inasema usigundue tairi upya.
Ili ufanikiwe kwenye maisha, waangalie wengine kisha uchukue hatua sahihi.
Kama unaowaangalia wamefanikiwa, angalia nini wamefanya mpaka wakafanikiwa, kisha fanya kama wao.
Na kama unaowaangalia wameshindwa, angalia nini wamefanya mpaka wakashindwa, kisha usifanye kama wao.
Hii ni akili ya kawaida ambayo ukiweza kuitumia kwa uhakika utaweza kufanikiwa sana.
Usiongeze mbwembwe, wewe waangalie wengine na chukua hatua.
Chochote zaidi ya hapo unakuwa unajipoteza wewe mwenyewe.
Ya pili ni siri kuu ya mafanikio kwenye kazi, ambayo inasema usikubali yeyote akuzidi kwenye kazi na kujifunza.
Jifunze kuliko wengine wote na fanya kazi kuliko wengine wote.
Haijalishi una akili ndogo au kubwa kiasi gani, kama utayageuza maisha yako kuwa darasa la kujifunza na ukajifunza kuliko wengine wote, utaweza kutatua mengi.
Na kama popote ulipo na chochote unachofanya wewe ndiye unayechapa kazi zaidi ya wengine, lazima utazalisha matokeo makubwa kuliko wengine.
Kama wengine wanafanya kazi masaa 8 kwa siku, wewe ukafanya kazi masaa 16 kwa siku, kama unachofanya ni sahihi na unakifanya kwa usahihi, utaweza kuzalisha mara mbili yao, hata kama wamekuzidi akili.
Jifunze kuliko wengine na fanya kazi kuliko wengine mara zote na hayupo atakayekukaribia kwa matokeo unayozalisha.
Ya pili ni siri kuu ya mafanikio kwenye biashara, ambayo inasema uhitaji uwepo na faida ipatikane.
Watu huwa wanahangaika sana ni biashara gani wafanye na waifanyeje ili wafanikiwe. Akili ya kawaida kabisa kwenye mafanikio ya biashara ni kuanza na uhitaji ambao tayari watu wanao. Kitu ambacho tayari kinawaumiza watu na wanatafuta suluhisho lake ila hawajalipata.
Kisha unaangalia uwezo na wingi wa watu hao wenye uhitaji kuona kama unaweza kufanya mauzo makubwa na ukabaki na faida nzuri. Kama hilo linawezekana basi unayo biashara nzuri na hupaswi kuhofia chochote, hata ushindani.
Lakini kama unaingia kwenye biashara ambayo uhitaji haupo au ni wa kutengeneza na/au wenye uhitaji hawawezi kumudu kulipia suluhisho unalowapa, hakuna namna hiyo biashara itaweza kufanikiwa.
Unaweza kutumia nguvu nyingi na ukapata matokeo mazuri, lakini huwa siyo ya kudumu, pale tu unapoacha kuweka nguvu nyingi na biashara pia inashuka.
Unapojikuta kwenye changamoto yoyote kwenye maisha yako, kabla hujahangaika na mambo makubwa, jiulize ni akili gani ya kawaida ambayo hujaifanyia kazi.
Matatizo mengi kwenye maisha yetu huwa yanaanzia kwenye kupuuza akili za kawaida na siyo kwenye kukosa akili kubwa.
Zingatia sana akili za kawaida na utakuwa umekamilisha asilikia 95 ya mafanikio yako. Asilimia 5 inayokuwa imebaki ndiyo inahitaji akili zaidi ya kawaida, ambayo inakuwa rahisi ukishakuwa umetumia vyema akili ya kawaida.
#NidhamuUadilifuKujituma
#AfyaUtajiriHekima
#KaziUpendoHuduma
#UpekeeUdadisiUbunifu
#UshirikianoUtegemeanoUwajibikaji
#BilioneaMafunzoni
#NajengaBiashara
#HakunaKingineMuhimu
#LazimaNitoboe
#NawekaKaziNifanikiwe
Nitahakikisha kwanza natumia akili ya kawaida kabla ya kuhangaika kutumia akili kubwa.
LikeLike
Vizuri sana.
LikeLike
Mafanikio makubwa ni kutumia akili ya kawaida TU
Asante sana
LikeLike
Karibu
LikeLike
Akili ya kujua kipi ukifanya utafanikiwa na ukifanye, na kipi ukifanya utafeli na ukiache.
Inatosha kuleta mafanikio makubwa
LikeLike
Kabisa.
LikeLike
asante sana kocha upo sahihi sana kwa wakati wote
LikeLike
Karibu
LikeLike
Unapojikuta kwenye changamoto yoyote kwenye maisha yako, kabla hujahangaika na mambo makubwa, jiulize ni akili gani ya kawaida ambayo hujaifanyia kazi.
Matatizo mengi kwenye maisha yetu huwa yanaanzia kwenye kupuuza akili za kawaida na siyo kwenye kukosa akili kubwa.
LikeLike
Hakika
LikeLike
Asante Kocha,
Kweli, ukiitumia akili ya kawaida kikamilifu, akili kubwa itajijenga yenyewe kwani akili ndogo ndiyo msingi wa akili kubwa.
LikeLike
Kabisa.
LikeLike
Asante sana kocha kwa somo hili
LikeLike
Karibu
LikeLike
Akili ya kawaida Kaz ya nguvu na kugeuza Maisha Yangu darasa.
Asante sana Kocha
LikeLike
Karibu
LikeLike
Hakika akili ya kawaida ni kila kitu, nimekuwa nikihangaika kutafuta akili kubwa kumbe hii niliyonayo ni msingi mkuu wa mafanikio yangu. Asante sana kocha.
LikeLike
Akili ya kawaida ikitumika kwa ukamilifu wake, mtu unafanya makubwa sana.
LikeLike
Mara zote nitatumia akili ya kawaida kabla ya kutumia akili ya kubwa
LikeLike
Vizuri sana.
LikeLike
Ni kweli anza na suluhisho la watu ndipo uweze kupata cha kuealetea wanapata shisa ya maji vuta maji kwanza na uweze kuwauzia kwa kuwaunfanishia
LikeLike
Kabisa.
LikeLike
Akili za kuvukia barabara.
LikeLike
Ndiyo zinazohitajika ili kufanikiwa.
LikeLike
Akili ya kawaida inatuambia tuangalie vile vinavyotuzunguka au vile tulivyonavyo na tuvitumie kuliko kuangalia mbali
LikeLike
Ndiyo
LikeLike
Nitakapo jikuta kwenye changamoto yoyote kwenye maisha yangu kabla sijahangaika na mambo makubwa nijiulize ni akili gani ya kawaida ambayo sijaifanyia kazi. Matatizo mengi kwenye maisha yangu huwa yanaanzia kwenye kupuuza akili za kawaida na siyo kukosa akili kubwa. Nitazingatia sana akili za kawaida na nitakuwa nimekamilisha asilimia 95ya mafanikio yangu. Asilimia 5 inayokuwa imebaki ndiyo inahitaji akili zaidi ya kawaida ambayo inakuwa rahisi ni kisha kuwa nimeitumia vyema akili ya kawaida.
LikeLike
Vizuri
LikeLike
Mafanikio makubwa kwenye maisha yanatokana na matumizi ya akili ya kawaida. Na Matatizo mengi kwenye maisha yetu huwa yanaanzia kwenye kupuuza akili ya kawaida na siyo kwenye kukosa akili kubwa.
LikeLike
Hakika
LikeLike