3261; Jikumbushe ushindi wako.
Rafiki yangu mpendwa,
Kwa changamoto na vikwazo vingi unavyokutana navyo kwenye maisha yako ya kila siku ni rahisi sana kusahau kwamba ulishapata ushindi mkubwa sana kwenye maisha yako.
Utungwaji wa mimba yako lilikuwa tukio kubwa la ushindi. Kulikuwa na mbegu nyingine za kiume zaidi ya milioni moja.
Lakini mbegu iliyokutoa wewe ndiyo iliyoibuka na ushindi wa kuweza kulirutubisha yai.
Kuzaliwa kwako ulikuwa ushindi mkubwa sana kwako. Kwani kuna mimba nyingi ambazo huwa hazifiki mwisho mzuri.
Na kubwa zaidi, kitendo cha wewe kuwa hai mpaka sasa ni ushindi mkubwa sana kwenye maisha yako.
Wapo wengi ambao walitamani saha siku kama ya leo wangekuwepo, lakini hawapo nasi.
Kitu muhimu sana ambacho nataka uondoke nacho hapa ni kujikumbusha ushindi ambao tayari umeshakuwa nao kwenye maisha yako.
Kujikumbusha ushindi ambao tayari ulishakuwa nao kunakupa nguvu ya kuendelea na mapambano hata kama utakutana na magumu.
Unapoingia kwenye jambo lolote, ingia ukiwa tayari unao ushindi. Kinachokuwa kimebaki ni wewe kuweka kazi ili kudhihirisha ushindi huo.
Unapoanza na mtazamo wa aina hiyo, mengine yote yanayobaki yanakuwa ni rahisi. Siyo urahisi wa kufanya, bali urahisi wa kupata ushindi kwa uhakika.
Kila unapofikia hali ya kuchoka na kukata tamaa, jikumbushe mfululizo wa ushindi ambao tayari umeshaupata kwenye maisha yako.
Unapoanza na ushindi, mengine yote yanawezekana kabisa.
Na huhitaji kujidanganya kwenye hili, bali unachohitaji ni kuyaangalia maisha yako binafsi na utapata ushahidi wa kutosha.
#NidhamuUadilifuKujituma
#AfyaUtajiriHekima
#KaziUpendoHuduma
#UpekeeUdadisiUbunifu
#UshirikianoUtegemeanoUwajibikaji
#BilioneaMafunzoni
#NajengaBiashara
#HakunaKingineMuhimu
#LazimaNitoboe
#NawekaKaziNifanikiwe
Kuzaliwa kwangu ni ushindi mkubwa sana kwangu Na kubwa zaidi, kitendo cha mimi kuwa hai mpaka sasa ni ushindi mkubwa sana kwenye maisha yangu, kwa hivyo nitaendelea kujikumbusha ushindi ambao tayari nilisha kuwa nao, ili kunipa nguvu ya kuendelea na mapambano hata kama nitakutana na magumu, kwa hivyo nitakapokuwa naingia kwenye jambo lolote nitaingia nikiwa tayari nina ushindi. Kitakacho kuwa kimebaki ni mimi kuweka kazi ili kudhihirisha ushindi huo.
LikeLike
Safi sana, ishi kwa ushindi maana tayari wewe ni mshindi.
LikeLike
Unachohitaji ni Kuangalia maisha yako binafsi utapata ushindi wa kutosha
LikeLike
Hakika.
LikeLike
Angalia maisha Yako binafsi na utapa ushindi wa uhakika
Asante sana
LikeLike
Hakika.
LikeLike
Kila ninapoona kuchoka na kukata tamaa,nitaangalia ushindi ambao nimewahi kuupata.
LikeLike
Vizuri
LikeLike
Nikumbushe ushindi.
LikeLike
Ndiyo
LikeLike
Kujikumbusha ushindi ambao tayari ulishakuwa nao kunakupa nguvu ya kuendelea na mapambano hata kama utakutana na magumu.
LikeLike
Kabisa.
LikeLike
Kwa hakika nikiangalia nyuma naona ushindi mkubwa napata nguvu yakusonga mbele
LikeLike
Kila unapofikilia hali ya kuchoka jikumbushe ushindi uliowahi kuwa nao kwenye maisha yako
LikeLike
Kabisa
LikeLike
Nikiangalia nilipotoka, vikwazo nilivyovuka,maumivu na magumu niliyopitia na kuvuka, hakika naona ushindi mkubwa mbele yangu.
Hakuna kukata tamaa Hadi itokee.
LikeLike
Safi sana.
LikeLike
Hakika,maisha yangu,ni darasa tosha kwa mimi kuniongezea nguvu ya kupambana na kunipa matumaini ya ushindi mkubwa.
LikeLike
Vizuri
LikeLike
Asante kocha mimi ni mshindi na nimezaliwa kushinda sitakata tamaa pale napokutana na magumu na changamoto nitapambana kuzivuka changamoto ili nipate ushindi
LikeLike
Vizuri
LikeLike
Hakika mimi ni mshindi na nilizaliwa kushinda na sina shaka na ushindi Wangu.
LikeLike
Vizuri
LikeLike
Kujikubusha ushindi.
Shukrani Sana Sana kocha.🙏🙏
LikeLike
Karibu
LikeLike
Ni kweli kuwa hai mpaka sasa ni ushindi tosha na ile ya kutungwa mimi nayo ni ushindi wa nguvu sana haya mengine ni kutekeleza tu
LikeLike
Kabisa
LikeLike
Asante Kocha,
Maisha ambayo nimepitia mimi tayari ni mshindi kilichobaki ni kuweka kazi ili kudhihirisha ushindi huo.
LikeLike
Ndiyo
LikeLike
Kujikumbusha ushindi ambao tayari ulishakuwa nao kunakupa nguvu ya kuendelea na mapambano hata kama utakutana na magumu.
LikeLike
Kweli.
LikeLike
Ushindi tayari Nina kilichobaki ni kuweka kazi ili kupata matokeo.
LikeLike
Ndiyo
LikeLike