3261; Jikumbushe ushindi wako.

Rafiki yangu mpendwa,
Kwa changamoto na vikwazo vingi unavyokutana navyo kwenye maisha yako ya kila siku ni rahisi sana kusahau kwamba ulishapata ushindi mkubwa sana kwenye maisha yako.

Utungwaji wa mimba yako lilikuwa tukio kubwa la ushindi. Kulikuwa na mbegu nyingine za kiume zaidi ya milioni moja.
Lakini mbegu iliyokutoa wewe ndiyo iliyoibuka na ushindi wa kuweza kulirutubisha yai.

Kuzaliwa kwako ulikuwa ushindi mkubwa sana kwako. Kwani kuna mimba nyingi ambazo huwa hazifiki mwisho mzuri.

Na kubwa zaidi, kitendo cha wewe kuwa hai mpaka sasa ni ushindi mkubwa sana kwenye maisha yako.
Wapo wengi ambao walitamani saha siku kama ya leo wangekuwepo, lakini hawapo nasi.

Kitu muhimu sana ambacho nataka uondoke nacho hapa ni kujikumbusha ushindi ambao tayari umeshakuwa nao kwenye maisha yako.

Kujikumbusha ushindi ambao tayari ulishakuwa nao kunakupa nguvu ya kuendelea na mapambano hata kama utakutana na magumu.

Unapoingia kwenye jambo lolote, ingia ukiwa tayari unao ushindi. Kinachokuwa kimebaki ni wewe kuweka kazi ili kudhihirisha ushindi huo.

Unapoanza na mtazamo wa aina hiyo, mengine yote yanayobaki yanakuwa ni rahisi. Siyo urahisi wa kufanya, bali urahisi wa kupata ushindi kwa uhakika.

Kila unapofikia hali ya kuchoka na kukata tamaa, jikumbushe mfululizo wa ushindi ambao tayari umeshaupata kwenye maisha yako.

Unapoanza na ushindi, mengine yote yanawezekana kabisa.
Na huhitaji kujidanganya kwenye hili, bali unachohitaji ni kuyaangalia maisha yako binafsi na utapata ushahidi wa kutosha.

#NidhamuUadilifuKujituma
#AfyaUtajiriHekima
#KaziUpendoHuduma
#UpekeeUdadisiUbunifu
#UshirikianoUtegemeanoUwajibikaji
#BilioneaMafunzoni
#NajengaBiashara
#HakunaKingineMuhimu
#LazimaNitoboe
#NawekaKaziNifanikiwe