💯KCM2324038; Ukuu.
Tumejipata, Tunaachilia Breki.
#JumatanoYaUwajibikaji
Mwanamafanikio,
Mwaka wa mafanikio 2023-2024 tumejipata kwa kuchagua kufanyia kazi kwa ukubwa kitu kimoja mpaka kitupe mafanikio makubwa tunayoyataka.
Tumeachilia breki kwa kufanyia kazi maeneo sita; MALENGO, KUJIKUBALI, UWAJIBIKAJI, UBUNIFU, MAWASILIANO na UTULIVU ili kujipa uhakika wa kufanya makubwa.

💯 Neno la leo; Ukuu.
Leo ikiwa ni #JumatanoYaUwajibikaji tunaona jinsi ambavyo gharama ya ukuu ni uwajibikaji.
Watu wengi wanataka ukuu kwenye maisha yao, yaani mafanikio makubwa yanayowafanya kuwa juu ya wengine.
Lakini pia watu wengi huwa wana tabia ya kulalamika na kulaumu wengine pale mambo yanapokwenda tofauti na matarajio yao.
Haishangazi kwa nini wengi hao huwa hawaupati ukuu wanaoutaka.
Ni kwa sababu ukuu na kulalamika havijawahi kwenda pamoja.
Gharama ya ukuu ni uwajibikaji.
Kama unataka mafanikio makubwa sana.
Kama unataka wengine wakuheshimu.
Kama unataka kuwa mfano mzuri kwa wengine.
Unahitajika kulipa gharama moja kubwa.
Gharama hiyo ni uwajibikaji.
Unapaswa kuwajibika kwa hali ya juu sana ndiyo uweze kupata matokeo makubwa unayoyataka.
Lazima ushike hatamu ya kila unachofanya na maisha yako kwa ujumla.
Kama kuna kitu hakijatokea, unajua wazi ni wewe mwenyewe uliyekisababisha na siyo mwingine yeyote.
Unapowalalamikia na kuwalaumu wengine unakuwa umewapa nguvu na mamlaka juu yako.
Unapochagua kushika hatamu na kuwajibika unakuwa umebakisha vitu hivyo ndani yako.
Kama kweli unautaka ukuu na mafanikio makubwa,
Anza kwa kulipa gharama kubwa iliyo mbele yako, ambayo ni kuwajibika.
Wajibika kwa kila kitu kinachokuhusu.
Hata kama kuna sababu zinazoshawishi kabisa kuna namna wengine wamechangia kwako kushindwa, bado ni wewe ndiye unayewajibika.
Ukikubali uwajibikaji wa hali ya juu kiasi hicho, hakuna kitakachoweza kukuzuia kufikia ukuu unaoutaka.
Kutokuwajibika imekuwa ni breki inayowazuia wengi kufanya makubwa.
Kubali uwajibikaji kamili wa kila unachojihusisha nacho na utaweza kufanya makubwa sana.
💯Hatua za kuchukua leo;
1. Andika ahadi yako ya mwaka wa mafanikio 2023-2024 kwa mtiririko wa NINI, LINI, WAPI, KWA NINI, NANI, VIPI na HISIA kisha weka kwenye kundi.
2. Soma kurasa 10 za kitabu cha MJASIRIAMALI MJANJA na shirikisha uliyojifunza kwenye kundi.
3. Chukua hatua kwenye yale ambayo umeshajifunza na shirikisha kwenye kundi.
4. Matokeo unayopata yashirikishe kwenye kundi.
5. Kaa kwenye mchakato sahihi wa kile unachotaka kufikia na epuka usumbufu unaokuwa kikwazo kwako.
Makala ya ukurasa wa leo ni kuhusu utabiri mzuri wa tabia za watu. Isome, weka maoni na nenda kachukue hatua. Fungua hapa; https://www.kisimachamaarifa.co.tz/2023/12/06/3262
Ukawe na siku bora kabisa ya leo, siku ya kuwajibika kwa kila kitu kwenye maisha yako ili kufikia ukuu unaoutaka.
Kocha.
💯