💯KCM2324040; Unachosikia.

Tumejipata, Tunaachilia Breki.

#IjumaaYaMawasiliano

Mwanamafanikio,

Mwaka wa mafanikio 2023-2024 tumejipata kwa kuchagua kufanyia kazi kwa ukubwa kitu kimoja mpaka kitupe mafanikio makubwa tunayoyataka.

Tumeachilia breki kwa kufanyia kazi maeneo sita; MALENGO, KUJIKUBALI, UWAJIBIKAJI, UBUNIFU, MAWASILIANO na UTULIVU ili kujipa uhakika wa kufanya makubwa.

0678 977 007



💯 Neno la leo; Unachosikia.

Leo ikiwa ni #IjumaaYaMawasiliano tunaona jinsi ambavyo mawasiliano siyo kile unachosikia mara ya kwanza.

Mawasiliano yamekuwa ni magumu baina ya watu kwa sababu hayakamiliki kwa usahihi.

Mara nyingi sana mtu anayesikiliza huwa hasikii kile kinachosemwa, bali anasikia kile anachotaka kusikia.

Na hiyo ni kwa sababu watu wengi wanasililiza kwa mihemko na kufanya maamuzi ya haraka kwa hisia.

Ili kuondokana na changamoto hiyo na kukamilisha mawasiliano, unapaswa kudhibiti mapokeo ya mawasiliano unayohusika.

Kama wewe ni msikilizaji, usiishie tu kusikiliza maneno peke yake, bali sikiliza na sababu zilizo nyuma ya maneno hayo. Hilo litakufanya uwaelewe watu vizuri zaidi.

Na pale wewe unakuwa mzungumzaji na wengine wasikilizaji, ni wajibu wako kuhakikisha wanakuelewa vizuri.
Hapa unapaswa kuwapa sababu ya kila unachowaeleza.
Kwa kuwapa sababu, wanaacha kutengeneza sababu zao wenyewe kwa hisia, ambazo huwa siyo sahihi.

Kwenye mawasiliano yoyote ambayo unahusika, hakikisha maana halisi ya kitu inajulikana na kueleweka na siyo watu kufanya maamuzi yao wenyewe kwenye kile walichosikia.

Mawasiliano yasiyo sahihi imekuwa ni breki inayowazuia wengi kufanikiwa, kwa kushindwa kuelewana na wengine na hivyo kukosa kile ulichokuwa unataka.
Kwa kuhakikisha watu wanaelewa maana na sababu halisi ya kila mawasiliano, inayafanya mawasiliano kukamilika vyema na kilichokusudiwa kufikiwa.

💯Hatua za kuchukua leo;
1. Andika ahadi yako ya mwaka wa mafanikio 2023-2024 kwa mtiririko wa NINI, LINI, WAPI, KWA NINI, NANI, VIPI na HISIA kisha weka kwenye kundi.
2. Soma kurasa 10 za kitabu cha MJASIRIAMALI MJANJA na shirikisha uliyojifunza kwenye kundi.
3. Chukua hatua kwenye yale ambayo umeshajifunza na shirikisha kwenye kundi.
4. Matokeo unayopata yashirikishe kwenye kundi.
5. Kaa kwenye mchakato sahihi wa kile unachotaka kufikia na epuka usumbufu unaokuwa kikwazo kwako.

Makala ya ukurasa wa leo ni kuhusu gharama za makosa. Isome, weka maoni na nenda kachukue hatua. Fungua hapa; https://www.kisimachamaarifa.co.tz/2023/12/08/3264

Ukawe na siku bora kabisa ya leo, siku ya kuelewa na kuelewesha sababu ya kila mawasiliano ili yakamilike vizuri.

Kocha.
💯