3265; Kazi ambayo ni mchezo kwako.
Rafiki yangu mpendwa,
Njia pekee ya kuwa mbele ya wengine na kufanya makubwa ni kupenda vitu ambavyo wengine hawavipendi.
Vitu ambavyo ni muhimu vifanyike, ila wengine hawapendi kabisa kuvifanya, huku wewe ukiwa unapenda kweli kuvifanya.
Unapata mafanikio makubwa kwenye kile ambacho kwako ni mchezo, ila kwa wengine ni kazi.
Kwako ni mchezo na unakuwa tayari kukifanya mara zote bila kusubiri kusukumwa wakati kwa wengine ni kazi ngumu ambayo hawaifanyi mpaka walazimishwe.
Wengi wanakwama kwenye kufanya yale wanayopenda zaidi kufanya kwa kudhani hawataweza kupata fedha kwenye hicho. Ukweli ni kwamba, kila kitu kina uwezo wa kuingiza fedha kama kitafanywa kwa njia sahihi.
Kinachohitajika ili shughuli yoyote iweze kukuingizia kipato ni kutatua tatizo ambalo watu wanalo na hawapo tayari kuendelea nalo.
Ushindani unakuwa mwepesi sana pale unapokuwa na msukumo mkubwa wa ndani kwenye kitu ambacho watu hawafanyi mpaka wapate msukumo mkubwa wa nje.
Wakati wengine wanajilazimisha kufanya, wewe unakuwa unajilazimisha kuacha kufanya kwa muda.
Haya yote tayari yapo ndani yako, kama huyatumii siyo kwa sababu huna, ila kwa sababu labda hujajua kama yapo au umejua na unayapuuza.
Tumia kila kilicho ndani yako kutoa thamani kubwa sana kwa watu wengine na utaweza kufanya makubwa.
#NidhamuUadilifuKujituma
#AfyaUtajiriHekima
#KaziUpendoHuduma
#UpekeeUdadisiUbunifu
#UshirikianoUtegemeanoUwajibikaji
#BilioneaMafunzoni
#NajengaBiashara
#HakunaKingineMuhimu
#LazimaNitoboe
#NawekaKaziNifanikiwe
Asante Kocha,
Nimejifunza ili ushindani uwe mwepesi kwangu, nguvu kubwa niweke kwenye msukumo wa ndani nisisubiri msukumo wa nje.
LikeLike
Vizuri
LikeLike
Tumia kila kilicho ndani yako kutoa thamani kubwa sana kwa watu wengine na utaweza kufanya makubwa.
LikeLike
Hakika
LikeLike
Kila kitu kinawezekana kukuingizia pesa kama kitafanywa Kwa njia sahihi
Asante sana
LikeLike
Kweli
LikeLike
Penda kufanya vitu ambavyo wengine hawavipendi.
LikeLike
Ndiyo
LikeLike
Kazi yangu ni kama mchezo kwangu
LikeLike
Vizuri
LikeLike
Ninaenda kufanya vile vilivyo ndani ya uwezo wangu kwa weredi mkubwa na kwa msimamo bila kuacha. Asante
LikeLike
Vizuri
LikeLike
Kila kitu kina uwezo wa kuingiza fedha kama kitafanywa kwa njia sahihi✍️
LikeLike
Hakika
LikeLike
Asante sana kwa makala nzuri
LikeLike
Karibu
LikeLike