💯KCM2324041; Makini.

Tumejipata, Tunaachilia Breki.

#JumamosiYaUtulivu

Mwanamafanikio,

Mwaka wa mafanikio 2023-2024 tumejipata kwa kuchagua kufanyia kazi kwa ukubwa kitu kimoja mpaka kitupe mafanikio makubwa tunayoyataka.

Tumeachilia breki kwa kufanyia kazi maeneo sita; MALENGO, KUJIKUBALI, UWAJIBIKAJI, UBUNIFU, MAWASILIANO na UTULIVU ili kujipa uhakika wa kufanya makubwa.



💯 Neno la leo; Makini.

Leo ikiwa ni #JumamosiYaUtulivu tunaona jinsi ambavyo bila ya utulivu mkubwa huwezi kufanya kazi makini.

Kazi yoyote makini inakutaka mtu uweke kila ulichonacho kwenye kazi hiyo. Unatakiwa kuweka muda, nguvu na umakini wako wote kwenye kazi hiyo.

Hilo litawezekana kama tu mtu utakuwa na utulivu mkubwa.
Kama mtu atakuwa amevurugwa na yupo kwenye usumbufu unaomnyima utulivu, hataweza kufanya kazi makini.

Ni muhimu sana kwako kutenga muda tulivu kila siku kwa ajili ya kukamilisha majukumu yako makubwa na muhimu.

Ukiweza kutenga angalau masaa mawili kwa siku ya kufanya kwa umakini mkubwa lile jukumu kuu kwako, utapiga hatua kubwa sana kulinganisha na wengine ambao hawatengi muda tulivu.

Kwenye zama tunazoishi sasa, usumbufu umekuwa mkubwa na unaadamana na sisi kila tunapoenda. Hiyo ni kwa sababu chanzo kikuu cha usumbufu ni simu janja tunazokuwa nazo kwa muda mrefu.

Hivyo moja ya mambo ya kufanya ili kupata utulivu ni kuwa mbali na simu pale unapohitaji kukamilisha kazi kwa umakini mkubwa.
Kama huwezi kutenga muda mfupi wa kupeleka umakini wako wote kwenye jukumu kuu na kuwa mbali na simu, huna maisha.

Kukosa utulivu imekuwa breki ambayo inawazuia wengi kujenga mafanikio wanayoyataka. Watu wanakuwa wamehangaishwa sana na usumbufu kiasi cha kuchoka na kushindwa kukamilisha yale muhimu na yenye tija.
Wewe ondokana na hilo kwa kutenga muda tulivu na kuutumia kufanya makubwa.

💯Hatua za kuchukua leo;
1. Andika ahadi yako ya mwaka wa mafanikio 2023-2024 kwa mtiririko wa NINI, LINI, WAPI, KWA NINI, NANI, VIPI na HISIA kisha weka kwenye kundi.
2. Soma kurasa 10 za kitabu cha MJASIRIAMALI MJANJA na shirikisha uliyojifunza kwenye kundi.
3. Chukua hatua kwenye yale ambayo umeshajifunza na shirikisha kwenye kundi.
4. Matokeo unayopata yashirikishe kwenye kundi.
5. Kaa kwenye mchakato sahihi wa kile unachotaka kufikia na epuka usumbufu unaokuwa kikwazo kwako.

Makala ya ukurasa wa leo ni kuhusu kazi ambayo ni mchezo kwako. Isome, weka maoni na nenda kachukue hatua. Fungua hapa; https://www.kisimachamaarifa.co.tz/2023/12/09/3265

Ukawe na siku bora kabisa ya leo, siku ya kutenga muda tulivu wa kutekeleza majukumu makuu yanayokufikisha kwenye malengo makubwa uliyonayo.

Kocha.
💯