💯KCM2324046; Udadisi.
Tumejipata, Tunaachilia Breki.
#AlhamisiYaUbunifu
Mwanamafanikio,
Mwaka wa mafanikio 2023-2024 tumejipata kwa kuchagua kufanyia kazi kwa ukubwa kitu kimoja mpaka kitupe mafanikio makubwa tunayoyataka.
Tumeachilia breki kwa kufanyia kazi maeneo sita; MALENGO, KUJIKUBALI, UWAJIBIKAJI, UBUNIFU, MAWASILIANO na UTULIVU ili kujipa uhakika wa kufanya makubwa.

💯 Neno la leo; Udadisi.
Leo ikiwa ni #AlhamisiYaUbunifu tunaona jinsi ambavyo udadisi ukichukua nafasi ya hofu mtu anakuwa na ubunifu mkubwa.
Huwa inasemwa kwamba kila mtu ni mbunifu.
Na ukitaka kudhihirisha hilo, angalia pale mtu anapohitaji kufanya jambo muhimu ila amechelewa. Atakuja na njia ya tofauti ya kuweza kukamilisha hilo kwa haraka.
Wote tayari tuna ubunifu ndani yetu, lakini hofu ndiyo imekuwa inatukwamisha kudhihirisha ubunifu huo.
Pale tunapokuwa na hofu, tunakuwa tumejizuia kuchukua hatua za tofauti na zinazoweza kuleta matokeo makubwa.
Kuondokana na hili, tunapaswa kubadili hofu kwa udadisi. Kila unapokuwa na hofu juu ya kitu, igeuze hofu hiyo kuwa ni udadisi.
Unachofanya ni kujiuliza iwapo utachukua hatua kwenye kitu hicho, ni matokeo gani utafanya?
Unatumia msukumo huo kujaribu vitu vya tofauti ili kupata matokeo bora.
Usikubali tena hofu iwe kikwazo kwako kuchukua hatua na kufika kule unakotaka.
Kila unapopatwa na hofu, jua unakaribia kufanya kitu cha tofauti na ambacho hujazoea.
Geuza hofu hiyo kuwa udadisi, kwa kuwa na shauku juu ya matokeo ya tofauti yanayoweza kupatikana kwa kufanya kitofauti.
Kukosa ubunifu ni breki ambayo imewakwamisha wengi kufanya makubwa.
Njia ya kuachilia breki hiyo ni kugeuza kila aina ya hofu unayokuwa nayo kuwa udadisi.
Unapojaribu vitu vingi tofauti tofauti, kuna ambavyo vitazalisha matokeo makubwa na ya tofauti.
Na hivyo ndivyo ubunifu unavyozaliwa.
💯Hatua za kuchukua leo;
1. Andika ahadi yako ya mwaka wa mafanikio 2023-2024 kwa mtiririko wa NINI, LINI, WAPI, KWA NINI, NANI, VIPI na HISIA kisha weka kwenye kundi.
2. Soma kurasa 10 za kitabu cha MJASIRIAMALI MJANJA na shirikisha uliyojifunza kwenye kundi.
3. Chukua hatua kwenye yale ambayo umeshajifunza na shirikisha kwenye kundi.
4. Matokeo unayopata yashirikishe kwenye kundi.
5. Kaa kwenye mchakato sahihi wa kile unachotaka kufikia na epuka usumbufu unaokuwa kikwazo kwako.
Makala ya ukurasa wa leo ni kuhusu ushauri na nyakati. Isome, weka maoni na nenda kachukue hatua. Fungua hapa; https://www.kisimachamaarifa.co.tz/2023/12/14/3270
Ukawe na siku bora kabisa ya leo, siku ya kugeuza kila hofu unayokuwa nayo kuwa udadisi ili uwe na msukumo wa kuchukua hatua za tofauti na kupata matokeo makubwa.
Kocha.
💯