3272; Bora na sahihi.
Rafiki yangu mpendwa,
Moja ya njia pendwa kwa wengi kupata mafanikio makubwa kwenye maisha ni kuwa bora sana kwenye kile wanachofanya kiasi kwamba wanatafutwa na wengi wenye uhitaji.
Ni pale mtu anapokuwa anatafutwa na wengi ndiyo anaweza kutoza gharama kubwa na bado watu wakawa tayari kulipa.
Hii ni njia ya uhakika ya kuthaminiwa na kulipwa zaidi. Lakini pia ni njia ngumu na ambayo nafasi zake ni chache. Kwa sababu kwenye kila tasnia kunaweza kuwa na watu wachache tu ambao ndiyo bora sana. Kama ambavyo kila nchi ina raisi mmoja na kila shirika lina mkurugenzi mmoja.
Hivyo kama utasubiri mpaka uwe bora kuliko wote ndiyo ufanikiwe, utajikwamisha kwenye mengi.
Uzuri ni kwamba kuna njia nyingine ya kujenga mafanikio makubwa kwenye maisha yako bila kushindana wala kujilinganisha na wengine.
Njia hiyo ni kufanya kilicho sahihi mara zote.
Ukiweza kufanya kilicho sahihi mara zote, utapata mafanikio makubwa hata kama wewe siyo bora kuliko wengine wote.
Kwa kuwapa watu kile wanachotaka mara zote, kutimiza matarajio yao na kwenda hatua ya ziada kiasi cha kuwashangaza itawafanya wakutegemee zaidi wewe kuliko wengine.
Kwa kuweka juhudi kwenye kile unachofanya na kuhakikisha kipato kinachoingia ni kikubwa kuliko kinachotoka ndiyo njia sahihi ya kujenga biashara itakayokuwa na mafanikio makubwa.
Kinachowakwamisha wengi kwenye maisha siyo kutokuwa na akili wala kutokujua wanachopaswa kufanya.
Bali kushindwa kufanya kile kilicho sahihi mara zote bila kuacha, hasa pale matokeo yanapokuwa hayaonekani haraka.
Watu huwa wanakata tamaa haraka pale wanapokuwa hawaoni matokeo waliyotegemea.
Lakini pia watu huwa wanachoka kurudia rudia kufanya kitu kile kile hata kama kinawapa matokeo mazuri.
Kuchoka na kukata tamaa haraka vimekuwa vinawatoa watu kwenye njia sahihi na kwenda kuwahangaisha kwenye mambo yasiyo na manufaa kwao kupata kile wanachotaka.
Kwa chochote unachofanya, jua ni vitu gani sahihi kufanya, kisha vifanye hivyo kwa msimamo bila kuacha.
Usihangaike sana na kuwa bora kuliko wengine, wewe kazana kufanya kilicho sahihi mara zote.
Kufanya kilicho sahihi kutakupa matokeo ya uhakika mara zote.
Lakini pia inaweza kupelekea wewe kuwa bora kuliko wengine, japo haikuwa ndiyo sababu kuu ya wewe kufanya.
Kwa kuweka umakini wako kwenye kile kilicho sahihi na kuepuka usumbufu usikutoe hapo, utaweza kufanya makubwa sana.
#NidhamuUadilifuKujituma
#AfyaUtajiriHekima
#KaziUpendoHuduma
#UpekeeUdadisiUbunifu
#UshirikianoUtegemeanoUwajibikaji
#BilioneaMafunzoni
#NajengaBiashara
#HakunaKingineMuhimu
#LazimaNitoboe
#NawekaKaziNifanikiwe
Usihangaike sana na kuwa bora kuliko wengine, wewe kazana kufanya kilicho sahihi mara zote.
LikeLike
Ni rahisi zaidi kufanya kilicho sahihi kuliko kuhangaika kuwazidi wengine.
LikeLike
Asante sana kocha. Nitafanya kilichosahihi mara zote
LikeLike
Vizuri.
LikeLike
Kufanya kilicho sahihi kutakupa matokeo ya uhakika mara zote.✍️
LikeLike
Ndiyo
LikeLike
Kufanya kilicho sahihi mara zote ni muhimu kuliko hata kuhangaika kuwazidi wengine.
LikeLike
Kabisa
LikeLike
Fanya Kwa uhakiki mara zote mwisho utakuwa Bora kuliko wote
Asante
LikeLike
Ndiyo
LikeLike
Nitafanya kilicho sahihi na kuepuka usumbufu mwingine wwte.
LikeLike
Vizuri
LikeLike
Asante kocha kwa msisitizo huu mkubwa kuchukua kwenye kuchukua hatua maishani
LikeLike
Karibu
LikeLike