3278; Mafanikio na kupendwa.
Rafiki yangu mpendwa,
Mtu tajiri kuliko wote duniani kwa zama tunazoishi sasa, Elon Musk, ndiye mtu asiyependwa zaidi.
Hilo ni jambo la kushangaza, hasa ukizingatia mambo makubwa na yenye manufaa anayokazana kufanya.
Anatengeneza magari ya kutumia umeme na hivyo kutatua changamoto ya nishati na kutunza mazingira.
Anarahisisha safari za kwenda angani na anataka sayari nyingine ziweze kuwa makazi ya binadamu ili tusiitegemee dunia peke yake.
Anazalisha nishati mbadala ya uhakika kwa kutumia mwanga wa jua ili kuhakikisha watu wanapata nishati hiyo.
Anarahisisha mawasiliano baina ya watu kwa kutoa mtandao wa intaneti wenye uhakika na unaoweza kupenyeza kila mahali duniani.
Anarahisisha mawasiliano baina ya kompyuta na ubongo ili kuwasaidia wenye magonjwa ya ubongo kuweza kuyatibu kwa kutumia teknolojia.
Analeta uhuru kamili wa kujieleza kupitia mtandao huru wa kijamii anaouendesha.
Kwa mambo hayo makubwa anayofanya, ungeweza kudhani ndiyo angekuwa mtu anayependwa zaidi kuliko wengine wote.
Lakini hivyo sivyo ilivyo.
Amekuwa ndiye mtu asiyependwa zaidi.
Hasa na wale wenye mamlaka ya kisiasa, ambao wanamwona anakuwa na mamlaka zaidi yao.
Serikali ya nchi yake imekuwa ya kwanza kumkwamisha kwenye mambo yake mbalimbali.
Makampuni mengine makubwa yamekuwa yanamhujumu moja kwa moja.
Hili siyo jambo linalotokea kwa mara ya kwanza.
Watu wote ambao wamewahi kufanikiwa sana, walikuwa pia ndiyo wasiopendwa sana.
Hili linapaswa kutukumbusha kubusu mafanikio na kupendwa, ni vitu ambavyo haviendi pamoja.
Wengi huwa wanakazana kufanikiwa, wakidhani wakishafanikiwa basi watapendwa na wengine.
Wanakuja kushangaa pale wanapofanikiwa ndiyo wanazidi kuchukiwa zaidi.
Wanashindwa kulielewa hilo na kudhani labda kuna namna wanakosea.
Ukweli ni kwamba, kuchukiwa na wengine pale unapofanikiwa siyo kosa lako.
Kuchukiwa pale unapofanikiwa ni hali ya kawaida kwenye asili ya binadamu.
Mtu anapofanikiwa kuliko wengine, huwa anaibua hisia za wivu kwa watu wengine. Wale ambao wanashindwa kuelewa mtu huyo amewezaje kufanikiwa kuliko wao.
Wanaoona wivu ni wale ambao wanaona wanastahili mafanikio hayo zaidi.
Lakini pia mafanikio huwa yanaleta hali ya watu kutaka kuchunguza zaidi kama mafanikio hayo ni halali.
Kwa kuwa kuna wengi ambao hawajafanikiwa, hawaamini kama kuna anayeweza kufanikiwa kuliko wao kwa njia sahihi.
Hivyo wanadhani kuna njia zisizo sahihi ambazo wametumia kufanikiwa.
Na mwisho, kadiri unavyofanikiwa ndivyo watu wanavyozidi kukuchukia kwa sababu unakuwa na mamlaka zaidi juu yao huku wao wakikosa mamlaka kwako.
Kwa mafanikio yako, wanakuwa wanakutegemea zaidi wewe kuliko unavyowategemea wao.
Hilo linawafanya wajisikie vibaya kwa kuona hawana namna ya kukutawala vile wanavyotaka wao.
Ni muhimu sana uyakumbuke haya wakati unayapambania mafanikio unayoyataka ili usije ukaumia pale yanapotokea.
Kwa sababu ni uhakika kwamba yatatokea, kama utapata mafanikio makubwa unayoyataka.
Kama unachotaka hasa ni kupendwa na wengi, mafanikio makubwa hayatakuletea hilo.
Chagua vyema nini unataka, kama umechagua mafanikio makubwa, kubaliana na hali ya kuchukiwa na wengi ambayo utakutana nayo.
Wewe usijali sana kuhusu hilo, badala yake kazana kufanya yale yaliyo sahihi mara zote.
Usiyumbishwe na chuki za watu wengine.
Wewe pambania kile unachokitaka hasa.
Mafanikio ndiyo kipaumbele chako kikuu, wakati chuki ndiyo kipaumbele chao.
Hivyo kila mtu ashinde mechi zake.
Kila kitu kwenye maisha kina gharama.
Na kadiri kitu kinavyokuwa kikubwa, ndivyo gharama yake inavyokuwa kubwa pia.
Usiumie pale unapokazana kufanikiwa ili watu wakukubali, halafu ndiyo wakazidi kukukataa.
Ni moja ya gharama za mafanikio unazopaswa kulipa.
Lipa gharama hizo bila kuumia na utayapata mafanikio unayoyataka kwa uhakika.
#NidhamuUadilifuKujituma
#AfyaUtajiriHekima
#KaziUpendoHuduma
#UpekeeUdadisiUbunifu
#UshirikianoUtegemeanoUwajibikaji
#BilioneaMafunzoni
#NajengaBiashara
#HakunaKingineMuhimu
#LazimaNitoboe
#NawekaKaziNifanikiwe
Ni kweli ukifanikiwa hata kidogo unaanza kutengeneza maadui hasa wale wanaoanza kukuchunguza na familia ya upande wa ndg zako na wafanyabiashara wengine pia ni mtari wa mbele kukuchukia maana umefanikiwa zaidi kuliko wao na sasa ni aibu kwao
LikeLike
Tuwe na ngozi ngumu.
LikeLike
Ukishafanikiwa watu wanashindwa kukutawala vile wawezavyo, ndiyo maana shambulio lao kubwa ni kukuchukia.
Asante sana Kocha Dr Makirita Amani.
LikeLike
Tuwajue na kuwapuuza.
LikeLike
Kuchukiwa na wengine pale unapofanikiwa sio kosa lako.Shinda mechi zako nao washinde zao.Asante kocha.
LikeLike
Kabisa, wapambane na hali zao.
LikeLike
Tena kwa jamii zetu zenye umasikini uliotukuka
Hata ukimudu mahitaji ya msingi tu chuki zinaanza
LikeLike
Kabisa yani, watu wanataka wakuone ukiteseka ndiyo wafurahi.
LikeLike
Mafanikio ni gharama, lipa kulingana na mafanikio unayoyataka
Asante
LikeLike
Ndiyo, kulipa gharama hakukwepeki.
LikeLike
Usiumie pale unapokazana kufanikiwa ili watu wakukubali, halafu ndiyo wakazidi kukukataa.
Ni moja ya gharama za mafanikio unazopaswa kulipa.
Lipa gharama hizo bila kuumia na utayapata mafanikio unayoyataka kwa uhakika.
LikeLike
Huwezi kukwepa kulipa gharama.
LikeLike
Ni vizuri kukumbuka kuwa Mafanikio na Kupendwa ni vitu ambavyo haviendi pamoja hata siku moja.
LikeLike
Havikai pamoja kabisa.
LikeLike
Mafanikio yanaibua wivu mkali kwa watu.
LikeLike
Sana, tuelewe vyema hilo.
LikeLike
Ukitaka kufanikiwa, achana na kutaka kupendwa
LikeLike
Ndiyo.
LikeLike
Kwenye mafanikio ni kuchagua,kutaka kupendwa au kutaka mafanikio,watu watakuchukia hata wa nyumbani mwako wanaweza kukuchukia tu
LikeLike
Kabisa
LikeLike