3281; Tatizo ni kujidanganya.
Rafiki yangu mpendwa,
Kitu kimoja kinachowakwamisha watu wengi sana wasipate kile wanachotaka ni kujidanganya wao wenyewe.
Wanakuwa wameanza kwa kuwadanganya wengine, mpaka wanafikia kujidanganya wao wenyewe.
Uzuri ni kwamba, matokeo huwa hawadanganyi, yanaweka kila kitu dhahiri kabisa.
Matokeo ambayo yanapatikana ndiyo ukweli wenyewe, bila ya kujali mtu anasema nini.
Mara nyingi sana unakuta mtu anasema anafanya vitu fulani, lakini matokeo yanakuwa tofauti kabisa na vile ambavyo yangekuwa kama kweli angekuwa anafanya.
Hapo unajua dhahiri ya kwamba mtu huyo anawadanganya wengine na kujidanganya yeye mwenyewe pia.
Kwenye maisha, hakuna kitu kibaya kama kujidanganya wewe mwenyewe.
Kwa sababu huwa ni shimo ambalo ni gumu sana mtu kutoka akishaingia.
Ni bora kujiambia ukweli kabisa.
Kama hupati matokeo ambayo unataka kupata, kuwa mkweli kwako wewe mwenyewe, ni wapi umekuwa unawadanganya wengine na hata kujidanganya wewe mwenyewe?
Bila ya kuwa mkweli kabisa kwako mwenyewe, utahangaika sana lakini utakuwa unarudi pale pale ulipoanzia.
Na mbaya zaidi itakuumiza sana wewe mwenyewe, kwa sababu unakuwa unajua unapojidanganya.
Kwa nje watu wanaweza kukuonea huruma, kwa kuwa unaonekana kuweka juhudi kubwa lakini matokeo unayopata ni madogo.
Lakini kwa ndani unajua ni wapi unapodanganya.
Kama hupati matokeo makubwa unayoyataka, wewe mwenyewe unajua dhahiri ni wapi unapodanganya.
Hilo litakuumiza kwa maisha yako yote, bila kujali wengine wanakuchukuliaje.
Ni vyema ukaamua kuwa mkweli kabisa kwako wewe mwenyewe.
Itakuumiza, lakini itakuweka kwenye njia sahihi ya kupata kile unachotaka.
Mafanikio makubwa na uongo huwa haviwezi kwenda pamoja.
Unaweza kuwadanganya kwa nje, lakini ndani yako ukweli utakuwa dhahiri na utakuumiza sana.
Chagua kuwa mkweli kwenye mambo yako yote, hata kama hutapata matokeo uliyokuwa unayataka, utakuwa huru kuliko ungekuwa unajidanganya.
#NidhamuUadilifuKujituma
#AfyaUtajiriHekima
#KaziUpendoHuduma
#UpekeeUdadisiUbunifu
#UshirikianoUtegemeanoUwajibikaji
#BilioneaMafunzoni
#NajengaBiashara
#HakunaKingineMuhimu
#LazimaNitoboe
#NawekaKaziNifanikiwe
Chagua kuwa mkweli kwenye mambo yako yote, hata kama hutapata matokeo uliyokuwa unayataka, utakuwa huru kuliko ungekuwa unajidanganya
LikeLike
Kabisa
LikeLike
Ni kweli ni vizuri kuwa mkweli kwsko wewe mwenyewe na wengine pia
LikeLike
Ndiyo
LikeLike
Ukweli unaniwekea huru, nitasema kweli siku zote, nitakuwa mkweli kabisa kwangu na kwa wengine…. Kweli kama njia kuu ya kunipa uhuru
LikeLike
Kila la kheri
LikeLike