3283; Athari za wengine.
Rafiki yangu mpendwa,
Kwa msingi, kila kitu kwenye asili ni nishati.
Na utofauti wa vitu huwa unaanzia kwenye aina na kiwango cha nishati kilicho ndani yake.
Vitu vyote, viumbe hai na visivyo hai vina nishati ndani yake.
Hivyo basi, hata mchango au athari ya kitu kwa vitu vingine inatokana na nishati inayotoka ndani ya kitu hicho.
Mtu au kitu kinakuwa na mchango mzuri kama kinatoa nishati chanya kwa wengine
Na pia kinakuwa na mchango mbaya kama kinatoa nishati hasi.
Tutaangalia zaidi hili kwa upande wa watu kwa sababu ndiyo kuna umuhimu zaidi.
Kuna watu ukiwa nao unatoka ukiwa unajisikia vizuri, ukiwa na matumaini makubwa na msukumo wa kwenda kufanya makubwa zaidi.
Hao ni watu ambao wanatoa nishati chanya na ambayo inakuwa kichocheo kizuri kwako.
Halafu kuna watu ambao ukiwa nao unatoka ukiwa unajisikia vibaya, unakata tamaa na kukosa msukumo wa kwenda kufanya makubwa.
Hao ni watu ambao wanatoa nishati hasi na ambayo inakuwa kikwazo kwako.
Nishati ambayo mtu anatoa huwa inatokana na mtazamo wanaokuwa nao, kiwango chao cha kujiamini na utayari wa kuchukua hatua.
Wenye mtazamo hasi, wasiojiamini na kutokuwa tayari kuchukua hatua huwa wanatoa nishati hasi.
Wakati wenye mtazamo chanya, wanaojiamini na kuwa tayari kuchukua hatua huwa wanatoa nishati chanya.
Wajibu wako mkubwa kwenye maisha ni kuhakikisha unazungukwa na watu wanaotoa nishati chanya ili wawe kichocheo kwako kufanya makubwa zaidi.
Epuka sana wale wanaotoa nishati hasi, kwa sababu watakukwamisha.
Usije ukajidanganya kwamba unaweza kuwabadili wenye nishati hasi, au unaweza kuwa nao na wasikuathiri.
Nishati hasi hata kidogo tu, inatosha kuvuruga kabisa nishati chanya unayokuwa nayo.
Ni sawa na kuwa na asali nyingi halafu ukaweka tone la sumu, yote inakuwa hatari.
Mafanikio yako yanaathiriwa sana na wale unaowapa nafasi kwenye maisha yako.
Wakague vizuri watu, hasa kwenye nishati wanazotoa ili usije kuwapa nafasi watu wanaokukwamisha.
Lakini pia kwa upande wa pili, hakikisha wewe mwenyewe unatoa nishati chanya muda wote.
Maana usije ukawa unawakimbia wengine, wakati wewe mwenyewe ndiyo tatizo kuu.
#NidhamuUadilifuKujituma
#AfyaUtajiriHekima
#KaziUpendoHuduma
#UpekeeUdadisiUbunifu
#UshirikianoUtegemeanoUwajibikaji
#BilioneaMafunzoni
#NajengaBiashara
#HakunaKingineMuhimu
#LazimaNitoboe
#NawekaKaziNifanikiwe
Je natoa nishati gani?Na wale wanaonizunguka wanatoa nishati gani?
LikeLike
Maswali muhimu sana kuzingatia.
LikeLike
Kuwa makini na watu,,,angalizo na mimi niwe natoa nishati chanya nisijekimbia watu bure
LikeLike
Ndiyo
LikeLike
Kaa na watu chanya lakini wewe usiwe unatoa nishati hasi
Asante
LikeLike
Ndiyo
LikeLike
Mafanikio yako yanaathiriwa sana na wale unaowapa nafasi kwenye maisha yako.
LikeLike
Kabisa
LikeLike
Nitaendelea kuzungukwa na watu wanao zalisha nishati chanya kwa nia ya kuendelea kupata msukumo wa kupiga hatua kubwa kwenye maisha yangu
LikeLike
Vizuri
LikeLike
Kweli ni swala la kujipima wewe kabka ya kukimbia wengine huenda wewe ndiyo una nishati hasi ndiyo wengine wakukimbie
Ukweli ni kwamba unapaswa kutoa nishati chanya na pia ukae na watu wenye kutoa nishati chanya pia
LikeLike
Kabisa
LikeLike
Huwezi kutoa kile ambacho huna.
Ili uwe mtu wa nishati chanya unapaswa kuwa na chanya kuzungukwa na watu chanya.
Na kuathiri wengine na nishati chanya uliyonayo.
Asante sana Kocha Dr Makirita Amani kazi nzuri unayoendelea kuifanya.
LikeLike
Hakika
LikeLike
Napaswa nijikague mimi kwanza kama natoa nishati chanya au hasi,isije ikawa nataka watu chanya wakati mimi mwenyewe ni tatizo.
LikeLike
Hakika
LikeLike