3290; Unachoshindana nacho.
Rafiki yangu mpendwa,
Watu wengi wamekuwa wanalalamikia ushindani kuwa mkali na kuwa kikwazo kwao kufanikiwa kwenye biashara.
Wanaona kama isingekuwa ushindani basi wangekuwa wamepiga hatua kubwa sana.
Lakini huo siyo ukweli.
Kama kuna ushindani pekee ambao unawakwamisha watu kwenye biashara basi ni uvivu na uzembe.
Uvivu na uzembe ndiyo vikwazo vikubwa kwa biashara nyingi kufanikiwa.
Uvivu ni kujua kinachopaswa kufanywa, lakini kutokukifanya.
Na uzembe ni kufanya kitu kwa makosa, huku mtu akiwa anajua kabisa jinsi ya kufanya kwa usahihi.
Biashara yoyote ile inaweza kupata mafanikio makubwa sana kama itafanya vitu viwili kwa ukubwa na msimamo; kuwa na wateja wengi na kuwafuatilia wateja hao kwa uhakika.
Hakuna ushindani wowote unaoweza kuizuia biashara kuwafikia wateja wengi.
Wala ushindani hauwezi kuzuia biashara isiwe na ufuatiliaji wa karibu na uhakika wa wateja.
Kwa sababu ya uvivu na uzembe, biashara nyingi hazifanyi hayo mawili kwa weledi mkubwa. Lakini pia watu hawapendi kujiona wao ni wavivu na wazembe, ndiyo maana lawana zitapelekwa kwa wengine wengi ila siyo kwa mtu mwenyewe.
Chukua mfano ni mara ngapi kwenye biashara wateja wamekuambia wakiwa tayari watakutafuta. Je ni mara ngapi wateja hao wamekutafuta kweli?
Hata kwa upande wa pili, ukiwa kama mteja, ni mara ngapi umekuwa unawaambia wauzaji utawatafuta ukiwa tayari. Lakini mpaka sasa bado hujamtafuta.
Unajionea hapo jinsi uvivu na uzembe vilivyo na athari kubwa kwenye mafanikio ya mtu.
Wewe acha kutumia sababu za nje kwenye hayo.
Badala yake angalia ndani yako ni kwa namna gani umekuwa unajikwamisha wewe mwenyewe.
Jinasue kwenye mkwamo huo kwa kuwa tayari kuweka juhudi kubwa kwenye kile unachokifanya ili kupata matokeo makubwa.
Usiwe mvivu wala mzembe,
Chapa kazi sana, utavuka mengi unayoyaona ni kikwazo.
#NidhamuUadilifuKujituma
#AfyaUtajiriHekima
#KaziUpendoHuduma
#UpekeeUdadisiUbunifu
#UshirikianoUtegemeanoUwajibikaji
#BilioneaMafunzoni
#NajengaBiashara
#HakunaKingineMuhimu
#LazimaNitoboe
#NawekaKaziNifanikiwe
Ni kweli hakuna zaidi ya uvivu na uzembe maana tukiweka kazi tunafanikiwa na kuweka sababu pembeni
LikeLike
Ndiyo
LikeLike
“Uvivu ni kujua kinachopaswa kufanywa, lakini kutokukifanya.
Na uzembe ni kufanya kitu kwa makosa, huku mtu akiwa anajua kabisa jinsi ya kufanya kwa usahihi.”
LikeLike
Ndiyo
LikeLike
Ni uvivu na uzembe ndio vinavyokwamisha ukuaji wa biashara.
LikeLike
Kabisa.
LikeLike
Hakika uvivu na uzembe havina nafasi ktk maisha yangu,maana ni kikwazo cha ukuaji wowote kwenye maisha
LikeLike
Ndiyo
LikeLike
Chapa kazi Sana utavuka vikwazo unavyooona.
🙏🙏🙏
LikeLike
Uhakika
LikeLike
Acha uvivu na uzembe utapata mafanikio makubwa
Asante sana
LikeLike
Kweli
LikeLike
Uvivu na uzembe ndiyo vikwazo vikubwa kwa biashara nyingi kufanikiwa.
LikeLike
Ndiyo
LikeLike
Naacha uvivu na uzembe
LikeLike
Vizuri
LikeLike
Uvivu na uzembe ndio vikwazo vikubwa kwa biashara nyingi kufanikiwa. Nitatengeneza wateja wengi na kuwafuatilia kwa uhakika na kwa msimamo na mafanikio ni lazima
LikeLike
Kila la kheri.
LikeLike
Nitaacha Uvivu na Uzembe kuanzia Leo ili nifanye makubwa.
LikeLike
Vizuri
LikeLike